Askofu Bagonza: Tume Huru, Mgombea Huru na kumbukumbu ya Kuzaliwa TANU

AFRIKA KUSINI

ASKOFU MKUU, Mfaniseni Sigisbert Ndwandwe, akiongoza watumishi wa Bwana walioingia mtaani kupinga udhalimu wa kaburu wa Afrika Kusini

field_image_Sigi_Desmond_Simeon-1024x796-768x597.jpg
Sasa sio wakati wa maandamano ni wakati wa kushawishi kwa hoja na mazungumzo mpaka unapatikana muafaka.
Mungu aendelee kuilinda Tanzania kwa maadui wa ndani na wa nje.
 
Hoja nzuri sana hii kwa bahati mbaya imetolewa na MTU

Ingetolewa na taasisi ingewashawishi nyingi
 
LITAKUWAJE SENSITIVE WKT U R NOT SURE??
Nimejaribu kusoma trend ya baadhi ya maaskofu katika kutoa kauli zao, nimepata jibu la nini kinachowasibu, naweza nisiwe sahihi ila ni jambo very sensitive.
 
Awe mstali wa mbele kwenye maadamano huku akiwa ameshika limsalaba na kimkufu shingoni na kikofia kichwani labda vitamtetea !!!
 
TUME HURU na MGOMBEA HURU

2020 ni mwaka wa Uchaguzi. Kama huchaguliwi basi unachagua. Kama hupigiwi kura na hupigi kura lazima kuna sababu inayokuzuia. Kuna watu wengi wanaruhusiwa kupiga kura lakini hawaruhusiwi kupigiwa kura. Wana haki ya kuongozwa tu lakini hawaruhusiwi kuongoza. Katiba yetu haitaki kujishighulisha na tatizo hilo. Una haki ya kupiga kura lakini huruhusiwi kupigiwa kura.

Vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi huu, vimetanguliza tamaa ya kupata madaraka bila kujali kundi kubwa linalopiga kura lakini haliruhusiwi kupigiwa kura. Hii ni kasoro kubwa sana.

Baba wa Taifa katika hotuba yake ya kustaafu uenyekiti wa CCM mwezi Agosti 1990, alituonya hivi:

"Lakini ni vizuri nikasema pia kwamba kwa maoni yangu hatuwezi tukaamua kuacha mfumo wa Demokrasia ya Chama Kimoja na tukajaribu mfumo wa Demokrasia ya Vyama vingi, kwa matumaini ya kwamba tukikuta kuwa mfumo huo hautufai, basi tutarudia tena Demokrasia ya Chama Kimoja. Tutajidanganya, haiwezekani na ni vigumu kabisa. Ukimwacha mkeo ukaoa mke mwingine na ukagundua kuwa huyu wa pili ni balaa, ni vigumu kumrudia mkeo wa kwanza. Demokrasia ya Vyama vingi, ikitushinda, mfumo ambao ni rahisi kufuatia utakuwa ni udikteta wa mtu mmoja au utawala wa kijeshi.”

Unabii wa Baba wa Taifa unaelekea kutimia. Ndani ya vyama vingi vya siasa kuna changamoto nyingi sana na demokrasia ndani ya vyama vyote ina hali mbaya sana. Viwango vya umakini vimeshuka sana katika vyama vyote. Katika miaka ya hivi karibuni kumejitokeza jambo la ajabu ambalo ni la kuwakatisha kabisa tamaa wananchi kushiriki katika mchakato wa uchaguzi. Kiwango cha wanasiasa kuhama vyama vyao na kusababisha ukiukwaji wa katiba na ustaarabu wa kitanzania kinatisha. Wanasiasa wengi wamekuwa wanahangaika miaka nenda rudi kutoka chama X kwenda Y na kutoka chama Y kwenda X. Idadi ya wapiga kura inaweza kushuka sana kwa sababu ya kukosekana kwa umakini katika kuhama na kupokea. Aidha, watu wengi sasa wanaamini upigaji kura si muhimu kama kuhesabu kura.

Changamoto hii inadhihirisha mambo mawili ambayo yamekuwa kilio cha Watanzania kwa muda mrefu bila mafanikio:

1. Hitaji la kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi

2. Mgombea Huru.

Bunge letu limeishavunjwa. Hakuna fursa ya kudai mabadiliko ya katiba ya kuruhusu hivi vitu muhimu kwa ajili ya afya demokrasia na amani ya nchi yetu. Na haya hayawezi tena kupatikana bila wananchi kuonyesha kwa vitendo kuyahitaji. Duniani kote njia moja ya kufikisha kilio cha watu ni kupitia maandamano ya Amani. Na Watanzania vile vile hawana historia ya kufanya vurugu kudai haki zao. Mfano mzuri ni Uhuru wetu wa 1961 ambao tuliupata bila kumwaga damu.

Pendekezo langu kwa Watanzania wote wanaoitakia mema nchi hii na kutaka kuona Demokrasia ya Vyama Vingi inastawi ni kuitikia wito wa kudai haki hizi mbili kwa njia ya amani.

Tarehe 7 ya mwezi wa 7 ni siku ya Saba Saba. Hii tarehe ina historia yake kuhusiana na kuanzishwa kwa chama cha ukombozi cha TANU. Chama hicho kilichoizaa CCM kinasifika kwa kuleta uhuru kwa amani. Siku hiyo kila mtanzania avae shati/gauni/koti/suruali/kofia/viatu/soksi/tai/ nyeupe kama ishara ya kuienzi amani ya taifa. Na amani ya kweli na endelevu katika Taifa letu ni kuunga mkono uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi na mgombea huru katika chaguzi zetu.

Vyama vyote vya siasa vinaalikwa kuunga mkono kampeini hii. Mnufaika mkuu wa kampeini hii ni Mama Tanzania. Ushindi wa mezani, ushindi unaotokana na kasoro za kujaza fomu na utumwa wa kukitumikia chama kuliko nchi ni kasoro kubwa katika chaguzi zetu.

Mama Tanzania ni yetu sote!! Mungu Ibariki Tanzania!!

Mwana kulitafuta na kulipata

Kalikawe Lwakalinda Bagonza
Watumie walengwa hela wanunue hizo nguo! Maana nyinyi CHADEMA mnatabia yakufanya vimiradi vidogo vidogo kuwachuna wafuasi wenu! Hukumsikia Lissu anachangisha mchango wa kugombea urais? Wewe naona umejiandaa kuuza vitu vyeupo! Mnatafuta hela za kampeni au ni zako?
 
Ni kweli...wajinga siyo rahisi kumuelewa..watamuunga mkono...watadhani Yuko sahihi..werevu watamuelewa kuwa huyu anatumika kuleta machafuko ndani ya nchi...uzuri ni kuwa Kama wapo watakaoandamana hawatazidi Mia moja
Hatafika wawili!
 
Yaani CCM kuongoza milele kwa kuiba kura kama kule Zanzibar ndio amani? Yaani hawa watawala ni kama wameroga. Mnaamini kabisa kuwa bila wao eti nchi hii itakosa amani. Mbona kuna amani Zambia, Uganda, Malawi, Swaziland, Botswana... Kuna CCM na Magufuli huko pia? Acheni ushamba wenu.
Hii ni Tanzania siyo nchi hizo
 
Ni kweli...wajinga siyo rahisi kumuelewa..watamuunga mkono...watadhani Yuko sahihi..werevu watamuelewa kuwa huyu anatumika kuleta machafuko ndani ya nchi...uzuri ni kuwa Kama wapo watakaoandamana hawatazidi Mia moja
Wee embu ficha ujinga wako yaan kudai tume huru ni kuleta machafuko
 
Sasa Baba Askofu kuna mambo mengi ya kuhubiri we kila siku ni siasa tuu...shuka madhabauni ingia jukwaani kugombea.
 
Ni kweli...wajinga siyo rahisi kumuelewa..watamuunga mkono...watadhani Yuko sahihi..werevu watamuelewa kuwa huyu anatumika kuleta machafuko ndani ya nchi...uzuri ni kuwa Kama wapo watakaoandamana hawatazidi Mia moja
Machafuko ya kudai haki kwa mungu wa Chato.
 
Wee embu ficha ujinga wako yaan kudai tume huru ni kuleta machafuko
Ndiyo...
Wewe ndiye mjinga nambari want..mjinga na mpumbavu pia..kwani iliyopo ni tume huru...unaimbishwa wimbo wa kinachoitwa tume huru na mabeberu na wewe kwa ujinga na upumbavu wako unakubali
 
TUME HURU na MGOMBEA HURU

2020 ni mwaka wa Uchaguzi. Kama huchaguliwi basi unachagua. Kama hupigiwi kura na hupigi kura lazima kuna sababu inayokuzuia. Kuna watu wengi wanaruhusiwa kupiga kura lakini hawaruhusiwi kupigiwa kura. Wana haki ya kuongozwa tu lakini hawaruhusiwi kuongoza. Katiba yetu haitaki kujishighulisha na tatizo hilo. Una haki ya kupiga kura lakini huruhusiwi kupigiwa kura.

Vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi huu, vimetanguliza tamaa ya kupata madaraka bila kujali kundi kubwa linalopiga kura lakini haliruhusiwi kupigiwa kura. Hii ni kasoro kubwa sana.

Baba wa Taifa katika hotuba yake ya kustaafu uenyekiti wa CCM mwezi Agosti 1990, alituonya hivi:

"Lakini ni vizuri nikasema pia kwamba kwa maoni yangu hatuwezi tukaamua kuacha mfumo wa Demokrasia ya Chama Kimoja na tukajaribu mfumo wa Demokrasia ya Vyama vingi, kwa matumaini ya kwamba tukikuta kuwa mfumo huo hautufai, basi tutarudia tena Demokrasia ya Chama Kimoja. Tutajidanganya, haiwezekani na ni vigumu kabisa. Ukimwacha mkeo ukaoa mke mwingine na ukagundua kuwa huyu wa pili ni balaa, ni vigumu kumrudia mkeo wa kwanza. Demokrasia ya Vyama vingi, ikitushinda, mfumo ambao ni rahisi kufuatia utakuwa ni udikteta wa mtu mmoja au utawala wa kijeshi.”

Unabii wa Baba wa Taifa unaelekea kutimia. Ndani ya vyama vingi vya siasa kuna changamoto nyingi sana na demokrasia ndani ya vyama vyote ina hali mbaya sana. Viwango vya umakini vimeshuka sana katika vyama vyote. Katika miaka ya hivi karibuni kumejitokeza jambo la ajabu ambalo ni la kuwakatisha kabisa tamaa wananchi kushiriki katika mchakato wa uchaguzi. Kiwango cha wanasiasa kuhama vyama vyao na kusababisha ukiukwaji wa katiba na ustaarabu wa kitanzania kinatisha. Wanasiasa wengi wamekuwa wanahangaika miaka nenda rudi kutoka chama X kwenda Y na kutoka chama Y kwenda X. Idadi ya wapiga kura inaweza kushuka sana kwa sababu ya kukosekana kwa umakini katika kuhama na kupokea. Aidha, watu wengi sasa wanaamini upigaji kura si muhimu kama kuhesabu kura.

Changamoto hii inadhihirisha mambo mawili ambayo yamekuwa kilio cha Watanzania kwa muda mrefu bila mafanikio:

1. Hitaji la kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi

2. Mgombea Huru.

Bunge letu limeishavunjwa. Hakuna fursa ya kudai mabadiliko ya katiba ya kuruhusu hivi vitu muhimu kwa ajili ya afya demokrasia na amani ya nchi yetu. Na haya hayawezi tena kupatikana bila wananchi kuonyesha kwa vitendo kuyahitaji. Duniani kote njia moja ya kufikisha kilio cha watu ni kupitia maandamano ya Amani. Na Watanzania vile vile hawana historia ya kufanya vurugu kudai haki zao. Mfano mzuri ni Uhuru wetu wa 1961 ambao tuliupata bila kumwaga damu.

Pendekezo langu kwa Watanzania wote wanaoitakia mema nchi hii na kutaka kuona Demokrasia ya Vyama Vingi inastawi ni kuitikia wito wa kudai haki hizi mbili kwa njia ya amani.

Tarehe 7 ya mwezi wa 7 ni siku ya Saba Saba. Hii tarehe ina historia yake kuhusiana na kuanzishwa kwa chama cha ukombozi cha TANU. Chama hicho kilichoizaa CCM kinasifika kwa kuleta uhuru kwa amani. Siku hiyo kila mtanzania avae shati/gauni/koti/suruali/kofia/viatu/soksi/tai/ nyeupe kama ishara ya kuienzi amani ya taifa. Na amani ya kweli na endelevu katika Taifa letu ni kuunga mkono uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi na mgombea huru katika chaguzi zetu.

Vyama vyote vya siasa vinaalikwa kuunga mkono kampeini hii. Mnufaika mkuu wa kampeini hii ni Mama Tanzania. Ushindi wa mezani, ushindi unaotokana na kasoro za kujaza fomu na utumwa wa kukitumikia chama kuliko nchi ni kasoro kubwa katika chaguzi zetu.

Mama Tanzania ni yetu sote!! Mungu Ibariki Tanzania!!

Mwana kulitafuta na kulipata

Kalikawe Lwakalinda Bagonza
Hii dhana ya nchi yetu kupata uhuru bila kumwaga damu huwa siielewi kabisa? Hivi zile damu za kina mkwawa na zile zilizomwagika kwenye maji maji war zilikuwa kwa ajiri ya kudai Nini? Askofu hivi kiongozi wa misri wakati ule Mungu anataka kuwatoa watu wake utumwani alikuwa nani vile? Je yule kiongozi na huyu yesu wa burigi kuna tofauti? Please siku moja tupe mada juu ya wawili hawa
 
Ndiyo...
Wewe ndiye mjinga nambari want..mjinga na mpumbavu pia..kwani iliyopo ni tume huru...unaimbishwa wimbo wa kinachoitwa tume huru na mabeberu na wewe kwa ujinga na upumbavu wako unakubali
Wee kweli zuzu tume huru imejaa makada wa lumumba tupu ,tume huru iwe na wajumbe mchanganyiko vyama pinzani viingie humo
 
Magufuli na viongozi wenzako acheni DOUBLE STANDARDS mtaligawanya Taifa na kuhatarisha amani, upendo na Umoja uliopo..!!

Akizungumza Sheikh Ponda anakamatwa ila wakizungumza kina Askofu wala hawasumbuliwi
 
Back
Top Bottom