Askofu Bagonza: Ushindi wa kishindo ni kaburi la maendeleo Afrika

Askofu Bagonza: Ushindi wa kishindo ni kaburi la maendeleo Afrika

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
USHINDI WA KISHINDO NI KABURI LA MAENDELEO AFRIKA

Tumemaliza Uchaguzi. Walioshinda wamepata asilimia 84 (urais) na bunge asilimia 99. Huu ni ushindi wa kishindo au kishindo cha ushindi?

Tukubaliane: Tuna watu wengi ni waaminifu kwa sababu hawana cha kuiba au wanaogopa kukamatwa. Serikali nyingi ziko hivyo. Zinahitaji kusimamiwa, kuchunguzwa, kukosolewa ili zifanye vizuri. Hata katika ulimwengu wa Imani, uwepo wa shetani ni msingi wa jitihada za kufundisha uadilifu.

Marekani wamemaliza Uchaguzi wao. Urais umeenda kwa chama Cha Democrat kwa kupata viti 306 dhidi ya 232 vya Trump (electoral colleges).

Bungeni (Cogress), Democrat wamepata viti 232 dhidi ya 197 vya Republican.

Kwenye Senate Republican wamepata viti 50 dhidi ya 48 vya Democrat. Viti 2 bado kuchaguliwa.

Kwa hiyo Rais mteule Biden atakuwa Ikulu bila kuwa na wingi wa kutisha wa wabunge na kwenye Senate chama pinzani ndicho kina viti 2 zaidi ya chama tawala. Hali hii inaweza kubadilika baada ya miaka miwili utakapofanyika Uchaguzi mdogo wa baadhi ya majimbo ya Bunge na senate. Kwenye uchaguzi huo, Biden anaweza kukosa wingi kwenye bunge na senate. Kwa nini?

1. Wamarekani hawapendi kuweka mayai yote kikapu kimoja (urais, ubunge na useneta). Ukipewa urais unanyimwa ama wabunge au maseneta ili ujifunze kushirikiana na wapinzani kwa kutumia hoja siyo bunduki.

2. Check and balance (kuwajibishana) ni msingi maamuzi ya kila kitu. Hata kwenye vyombo vya habari ni lazima kikisemwa kitu sharti upande wa pili uwekwe ili wasomaji/ wasililizaji wajue pande mbili na kuamua wenyewe.

Kimantiki, ushindi wa kishindo chaweza kuwa chanzo cha mdororo wa Maendeleo katika bara letu linalopenda sana neno NDIYO. Tabia ya kuchukia maoni tofauti inadumaza utundu, ugunduzi, na ubunifu. Badala yake dhana ya NDIYO inakomaza kukariri, woga, utii usio na dhamiri na kuondoa uendelevu(sustainability) katika maamuzi mengi. Mfumo wa Elimu ndilo jiko la kupika Taifa linalohoji au linaloimba NDIYO kwa kila kitu.

Mfungwa katika mfumo wa NDIYO akiwekewa mkate na funguo za gereza akaambiwa achague moja, atachagua mkate.

Mfungwa katika gereza la KWA NINI, akiwekewa hivyo viwili, anaweza akahoji kwa nini si vitatu badala ya KUCHAGUA kama alivyoelekezwa.

Zawadi ya mfungwa ni Uhuru si sabuni ya kuoga akiwa gerezani. Kumwachia huru mfungwa ni sawa na kumweka huru Askari magereza anayemlinda. Hiyo ndiyo faida kuu ya Uhuru. Unanufaisha pande zote.
 
kuna mtu kashinda kila alichokipanga
  1. Kuwa Rais kwa hila
  2. Kuua upinzani
  3. Malaika kushuka na kuzima mitandao
  4. Matajiri kuishi kama mashetani (anapora mali zao kwa kubambikwa kesi za "UHUJUMU UCHUMI")
  5. kupora
  6. Kupachika ndugu zake kwenye kila nafasi nzurinzuri
ONGEZA MENGINE


 
USHINDI WA KISHINDO NI KABURI LA MAENDELEO AFRIKA

~Tumemaliza Uchaguzi. Walioshinda wamepata asilimia 84 (urais) na bunge asilimia 99. Huu ni ushindi wa kishindo au kishindo cha ushindi?

TUKUBALIANE

~Tuna watu wengi ni waaminifu kwa sababu hawana cha kuiba au wanaogopa kukamatwa. Kama wangepata cha kuiba na wakawa hawana wasimamizi wangeiba tu. Uaminifu haupimwi kwa kutoiba tu bali kwa kuwa na cha kuiba lakini ukashinda jaribu la kuiba.

~Serikali nyingi ziko hivyo. Zinahitaji kusimamiwa, kuchunguzwa, kukosolewa ili zifanye vizuri. Hata katika ulimwengu wa Imani, uwepo wa shetani ni msingi wa jitihada za kufundisha uadilifu.

~Marekani wamemaliza Uchaguzi wao. Urais umeenda kwa chama Cha Democrat kwa kupata viti 306 dhidi ya 232 vya Trump (electoral colleges).

~Bungeni (Cogress), Democrat wamepata viti 232 dhidi ya 197 vya Republican.

~Kwenye Senate Republican wamepata viti 50 dhidi ya 48 vya Democrat. Viti 2 bado kuchaguliwa.

~Kwa hiyo Rais mteule Biden atakuwa Ikulu bila kuwa na wingi wa kutisha wa wabunge na kwenye Senate chama pinzani ndicho kina viti 2 zaidi ya chama tawala.

~Hali hii inaweza kubadilika baada ya miaka miwili utakapofanyika Uchaguzi mdogo wa baadhi ya majimbo ya Bunge na senate. Kwenye uchaguzi huo, Biden anaweza kukosa wingi kwenye bunge na senate. Kwa nini?

1. Wamarekani hawapendi kuweka mayai yote kikapu kimoja (urais, ubunge na useneta). Ukipewa urais unanyimwa ama wabunge au maseneta ili ujifunze kushirikiana na wapinzani kwa kutumia hoja siyo bunduki.

2. Check and balance (kuwajibishana) ni msingi maamuzi ya kila kitu. Hata kwenye vyombo vya habari ni lazima kikisemwa kitu sharti upande wa pili uwekwe ili wasomaji/ wasililizaji wajue pande mbili na kuamua wenyewe.

~Kimantiki, ushindi wa kishindo chaweza kuwa chanzo cha mdororo wa Maendeleo katika bara letu linalopenda sana neno NDIYO. Tabia ya kuchukia maoni tofauti inadumaza utundu, ugunduzi, na ubunifu. Badala yake dhana ya NDIYO inakomaza kukariri, woga, utii usio na dhamiri na kuondoa uendelevu(sustainability) katika maamuzi mengi. Mfumo wa Elimu ndilo jiko la kupika Taifa linalohoji au linaloimba NDIYO kwa kila kitu.

~Mfungwa katika mfumo wa NDIYO akiwekewa mkate na funguo za gereza akaambiwa achague moja, atachagua mkate.

~Mfungwa katika gereza la KWA NINI, akiwekewa hivyo viwili, anaweza akahoji kwa nini si vitatu badala ya KUCHAGUA kama alivyoelekezwa.

~Zawadi ya mfungwa ni Uhuru si sabuni ya kuoga akiwa gerezani. Kumwachia huru mfungwa ni sawa na kumweka huru Askari magereza anayemlinda. Hiyo ndiyo faida kuu ya Uhuru. Unanufaisha pande zote.

Bishop PhD, Kalikawe Lwakalinda Bagonza
K.K.K.T-Karagwe.
 
Mzee Bagonza maombi yake yote kwa Lissu ili awe Rais yamegonga mwamba.
Bagonza nlimuonya kwamba yeye ni kiongozi wa tasisi kubwa nchini, sasa kwakuwa amejichagulia upande wa kushabikia ataumia sana.

Alikuwa akipanda kwenye jukwaa kwa Lisu anasema uchaguzi huu ni kati ya mungu aliemuokoa Lisu na risasi 16 na wa Mungu wa Magu alieondoa korona kwa maombi.

Bagonza mpaka leo haamini kama Mungu ni mkubwa kuliko corona. Ndio maana mimi nakonaga kale kajamaa hata hirizi katakuwa nazo. Ndio maana wakati wenzie wameungana na Magu kufunga kwa maombi yeye aliungana na shetani akafunga makanisa.

Wahaya wana shida sana, kwa dharau zile za Bagonza kisa ule udokta wake, basi yeye kwake Mungu si lolote mbele ya phd yake.
 
Back
Top Bottom