bazl
JF-Expert Member
- Jul 29, 2018
- 446
- 599
Kwani huko anakoenda hatorudisha? Mkataba wa mkopo ulisema ni lazma afanye kazi serikalini? Huko anakoenda anaenda kuwahudumia wachina?Mimi nadhani tunalo tatizo la tafsiri. Badala ya kuhukumu tungemuuliza alikuwa na maana gani. Mimi nilivyomuelewa ni kwamba kama amesomeshwa na serikali anapokuwa na mawazo ya kuondoka arudishe kwanza gharama maana huo mi mkopo suo hisani halafu aondoke.
Vinginevyo hizo Kampuni binafsi zinazomchukua ziingie gharama ya kurudisha hilo deni waendelee naye vinginevyo wafungiwe hadi wamerudisha.
Ingekuwa kusomeshwa na serikali mi hisani suo mkopo basi huo ujumbe wa Askofu unasimama vinginevyo amepotoka kidogo maana hata kanisa likimkopesha mtu lazima arudishe mkopo.