Askofu Benson Bagonza (PhD) azungumzia kilichoitwa “Kongamano la Viongozi wa Dini” Dar es Salaam

Askofu Benson Bagonza (PhD) azungumzia kilichoitwa “Kongamano la Viongozi wa Dini” Dar es Salaam

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Anaandika Baba Askofu Rev. Dr. Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe kuhusu kilichoitwa Kongamano la Viongozi wa Dini


Watu wengi wameniuliza sana kuhusu kongamano la viongozi wa DINI. Siwezi kumjibu kila mtu peke yake. Maoni yangu ni haya:

1. Hakuna DINI inayoiwakilisha nyingine. Wasikilizeni walioenda. Msiwapuuze ambao hawakwenda maana nao wana DINI zao.

2. Nyakati za uchaguzi huwa kuna kutumiana. DINI kuitumia serikali au serikali kuitumia DINI. Lakini Mungu yuko pande zote na hatumwi wala hatumiwi bali ANATUMA.

3. Taifa linaunganishwa na kamati za AMANI na HAKI. Waandaaji wa kongamano wamesema hili ni Kongamano la AMANI. Wanaotaka HAKI wasubiri jingine.

4. Uchaguzi maana yake ni kuchukua kimoja kati ya vingine. Tusichukiane kwa mtu kuutumia Uhuru wake kuchagua anachopenda. Kila mtu aheshimu uchaguzi wa mwenzake. Tuache kuhukumu wengine kwamba wanachanganya DINI na SIASA. Kongamano hili halijachanganya DINI na maharage.

5. DINI si mali za viongozi, Vyama si mali ya viongozi na Serikali si mali ya viongozi. Lakini vyote (DINI, vyama na serikali) havimmiliki Mungu. Hata hivyo Kongamano limemtanguliza Mungu. Inapendeza, lakini wakumbuke:

- Mungu halindwi, analinda
- Mungu habebwi, anabeba
- Mungu haamrishwi, anaamrisha
- Mungu hamilikiwi, anamiliki
- Mungu si tukio ni mchakato.

Haya ni maoni yangu, nawe una yako. Uwe na AMANI katika Mambo yako Kama nilivyo na AMANI na Mambo yangu!
 
Hii hoja namba 3 kwangu mimi nimeielewa sana:

3. Taifa linaunganishwa na kamati za AMANI na HAKI. Waandaaji wa kongamano wamesema hili ni Kongamano la AMANI. Wanaotaka HAKI wasubiri jingine.
 
Na haya ndio matumizi sahihi ya PhD

Sio wengine wanaPhD za kuungaunga wakiulizwa wamepataje wanakuwa wakali na kukimbilia kuteka watu na kuwapoteza
Tutakukumbuka Ben Saanane
 
Wengine wapo busy kuzindua sera ya vijana

Wengine wapo busy kukusanya viongozi wa dini kutakatisha mapungufu yao na kukusanya wasanii vijana wengi wao maskini ati kupewa dili ya kuimba kwenye kampeni zao - malipo ya muda mfupi!!
 
Yaani wanatafuta Kila kinachoweza kushikiwa kujaribu kupindisha ukweli halisi Kuwa Magu anakubarika🤔! Nawaonea huruma saana! Kinachopiga kura siyo PhD! Kamuulize Dr. Makyembe alivyomjibu yule mjumbe juu ya mtihani wa STD 7 bila kujua wapiga kura walio wengi waligalagazwa na mtihani huo!

Sasa wapiga kura hao ndio wameshamkubali Magu, na ninyi mnaojiita wapinzani huwa mnaamini ktk nguvu ya umma na Kuwa sauti ya wengi ni ya Mungu so ndio eeh! Subirini mwaka huu October mtakavyoiona na kuisikia, na kui'feel' hiyo nguvu na sauti ya umma ikiwaadhibu🤔!
 
Back
Top Bottom