Askofu Dkt. Bagonza amshukia Lugola kwa kumfananisha Magufuli na Yesu. Asema hii laana lazima itafune mtu na Taifa

Askofu Dkt. Bagonza amshukia Lugola kwa kumfananisha Magufuli na Yesu. Asema hii laana lazima itafune mtu na Taifa

Kwa sasa ni lazima umtumikie kafiri ili upate mradi wako, Baba askofu yeye haogopi kupotezwa!?
 
Anaandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
___________
Kufuru haina kinga. Kwa Wakristo, dhambi isiyosameheka katika Agano Jipya ni kumkufuru Roho Mtakatifu. Na katika Agano la Kale ni ibada ya sanamu (idolatry). Amri ya kwanza aliyopewa Musa inasema, "Mimi ni Bwana Mungu wako, usiwe na miungu mingine" (Kutoka 20:3-6).
_
Kufuru haina kinga duniani wala mbinguni. Ghadhabu ya Mungu iko wazi katika vitabu vyake vyote.

Tuzitendee haki kumbukumbu zetu;

1. Mwaka 2005 mjinga mmoja alitumia uhuru wake vibaya huko Denmark. Akachora katuni yenye kumdhihaki Mtume Muhammad (S.A.W). Dunia nzima iliwaka moto.

2. Yohana 1 : 12
Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; 2010 mpuuzi mwingine huko Marekani akachoma moto Quran tukufu. Hakuna jiwe lililosalia juu ya jiwe.

3. Mwaka 2012 huko Mbagala utoto ukavuka mipaka. Msahafu ukakojolewa. Amani yetu ilitoweka kwa muda. Majivu yakawa majivu.

4. Huko Sumbawanga, msimu wa uchaguzi kama huu, ulimi wa mmoja uliteleza. Akaufananisha UTATU mtakatifu na mafiga matatu ya chama chake. Hapakutosha. Mzee Pinda (mtu wa amani), ana cha kusimulia mpaka leo.

Mungu wetu hafananishwi. Mungu wetu halinganishwi. Mungu wetu hashindanishwi. Ni ibada ya sanamu kupenda kitu kingine kuliko unavyompenda Mungu wako. Ni ibada ya sanamu kuchukia kitu kingine kuliko unavyomchukia shetani. Ni ibada ya sanamu kumlinganisha Muumbaji na uumbaji wake.

Hatumtendei haki Mungu kumlinganisha na aliowaumba. Hatuwatendei haki wale tuwapendao kwa kuonesha kuwa tunawapenda kuliko tunavyompenda aliyewaumba.
P
Walinzi na waangalizi wa imani (viongozi wa dini), kama hatuwezi kukemea hili (la Lugola) basi angalau tuchukie na tuonekane kweli tumechukizwa.!
I
Huyu sijui Askofu aliupataje biblia inasema Ktk Yohana 1 : 12
Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; (Yohana 1:12)Yesu ni mwana wa Mungu, kuna ubaya gani kujifananisha na Yesu? Kitabu cha mwanzo kinasema tumeumbwa kwa mfano wa Mungu (Mwanzo 1:27)
Mwanzo 1 : 27
Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba., Kwani kuna ubaya gani kusema ninafanana na Mungu? Mungu anachozuia kujitukuza (Isaya 42:8) Isaya 42 : 8
Mimi ni Bwana; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu. Askofu asome biblia. Mungu ibariki Tanzania
 
Hawa itakuwaje maana yake wamejifananisha na yesu na mpaka tukiangalia filamu zao tuna waita yesu
willem-dafoe-the-last-temptation-of-christ-1988-1517933613.jpg
mainnn.jpg
2b9b89f78bf4755e50e901f988c7aa75.jpg
bb.PNG
 
Attachments

  • bb.PNG
    bb.PNG
    425.6 KB · Views: 1
Anaandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
___________
Kufuru haina kinga. Kwa Wakristo, dhambi isiyosameheka katika Agano Jipya ni kumkufuru Roho Mtakatifu. Na katika Agano la Kale ni ibada ya sanamu (idolatry). Amri ya kwanza aliyopewa Musa inasema, "Mimi ni Bwana Mungu wako, usiwe na miungu mingine" (Kutoka 20:3-6).
_
Kufuru haina kinga duniani wala mbinguni. Ghadhabu ya Mungu iko wazi katika vitabu vyake vyote.

Tuzitendee haki kumbukumbu zetu;

1. Mwaka 2005 mjinga mmoja alitumia uhuru wake vibaya huko Denmark. Akachora katuni yenye kumdhihaki Mtume Muhammad (S.A.W). Dunia nzima iliwaka moto.

2. Mwaka 2010 mpuuzi mwingine huko Marekani akachoma moto Quran tukufu. Hakuna jiwe lililosalia juu ya jiwe.

3. Mwaka 2012 huko Mbagala utoto ukavuka mipaka. Msahafu ukakojolewa. Amani yetu ilitoweka kwa muda. Majivu yakawa majivu.

4. Huko Sumbawanga, msimu wa uchaguzi kama huu, ulimi wa mmoja uliteleza. Akaufananisha UTATU mtakatifu na mafiga matatu ya chama chake. Hapakutosha. Mzee Pinda (mtu wa amani), ana cha kusimulia mpaka leo.

Mungu wetu hafananishwi. Mungu wetu halinganishwi. Mungu wetu hashindanishwi. Ni ibada ya sanamu kupenda kitu kingine kuliko unavyompenda Mungu wako. Ni ibada ya sanamu kuchukia kitu kingine kuliko unavyomchukia shetani. Ni ibada ya sanamu kumlinganisha Muumbaji na uumbaji wake.

Hatumtendei haki Mungu kumlinganisha na aliowaumba. Hatuwatendei haki wale tuwapendao kwa kuonesha kuwa tunawapenda kuliko tunavyompenda aliyewaumba.

Walinzi na waangalizi wa imani (viongozi wa dini), kama hatuwezi kukemea hili (la Lugola) basi angalau tuchukie na tuonekane kweli tumechukizwa.!
Rubbish ,ondoeni picha kwenye nyumba zenu za yule jamaa aliejifanya yesu kwa kumuigiza na picha hizo ndio zimegeuka mapambo ya nyumba zenu,hilo Bagonza halioni ?,aache ujinga wake,Lugola yuko sawa kabisa
 
Udikiteta ni Nini???
Nafikiri unajua udikteta ni nini manake huwezi kujikomboa kutoka udikteta kama huujui. Ni mfumo wa utawala ambapo kiongozi anahodhi madaraka na kuamrisha walio chini yake wafanye atakavyo yeye bila mjadala au ushirikishwaji wa wengine. Ni matumizi ya nguvu ya dola kuwadhibiti watu/umma kwa faida ya kiongozi aliyeko madarakani. Inasikitisha sana kwamba tunaye mtu kama huyu kwenye taifa letu lililokuwa linaheshimika kwa demokrasia.
 
Kwa theolojia ya kisiasa kange yuko right jesus of chato and Jesus of Nazareth
Mungu ametuumba kwa sura na mfano wake hivyo binadamu anamwakilisha mungu na ukimpenda binadamu umempenda MUNGU

Hivyo ufananisho yesu ni Mungu kwa mantiki ya kiteolojia isipokuwa ukiongeza maneno mengine yenye mrengo wa kushusha heshima yaMungu
 
Halafu bagonza sio mwema kiasi cha kuwanyooshea wengine vidole.
Bangoza ninWakili wa Kristo, ni Wakili wa Biblia. Wewe ndiebunaejua sio mwema kwa Wakristo tunajua maana ya askofu na maana yake katika kanisa. Endelea kuwaza ujuavyo ila sisi tuajua ni mpakwa mafuta wa bwana...
 
Kweli kiongozi mkubwa wa kidini askofu. Kuna Mambo ya wanasiasa wanajitafutia laana wenyewe. Kwanza Magufuli hajamtuma huyo kenge. Kaamua mwenyewe kukufuru hakutumwa anatafuta Jimbo tuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Alitakiwa akemee aliyefananishwa na yesu,mbona kule kilosa mkoani Morogoro yule mtumishi aliye kichana kitabu cha koroan ,licha ya mtuhumiwa kupelekwa mahakamani,lakini yesu wa Tanzania alitangaza kumfukuza kazi.
 
Bagonza angemfananisha "jamaa" na mtume "mwamadi" hivi kweli WAislamu wangekaa kimya mpaka muda huu ?
 
Back
Top Bottom