Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni kweli ushoga siyo sababu kabsa ya marekani kumkataa Daud Bashite, ebu watetezi wa uovu wa Bashite oneni aibu acheni ujinga acheni kuja na visingizio vya kijinga jingaMsikimbilie kwenye ushoga.Uganda wamepitisha sheria kali kabisa kuusiana na ushoga na hawajafungiwa ndio kwanza wameongezewa na funding kutoka PEPFAR, Tusisingizie hivyo vitu sababu ni demokrasia na involvement yake kwenye issue za kuminya demokrasia pamoja na "credible information" walizonazo kuhusiana na uhusika wake kwenye mambo hayo.
Kwani wanayotendewa wapinzani kule Uganda yana tofauti gani na wanayo mtuhumu Makonda?Ki ukweli Ushoga haupendezi na zaidi ya 99% hawaukubali ushoga.Ila kwa ujumbe ule wa US hakuna mahali nimeona ushoga. Alafu nikivuta picha jinsi Raisi wa Uganda alivyoweka vikwazo juu ya ushoga basi yeye ndo angekuwa wakwanza kuguswa na hii adha.
Kushika kaa la moto huku wajitetea sio la moto anae dhuriaka ni mshikaji.
Ingependeza tujadili waliyo yataja alafu tupinge kwa hoja kuwa wamemuonea sio kuleta dhahania
Sasa kama Uganda wanafanya ndiyo Daud Bashite afanye na yeye? Kwa kuwa Uganda hawajasemwa na marekani ni ruksa Daud Bashite aendelee kuwatesa watu?Kwani wanayotendewa wapinzani kule Uganda yana tofauti gani na wanayo mtuhumu Makonda?
Ina maana wamarekani hawayaoni ya Uganda?
Hawakumsikia Bobi Wine ambae alipelekwa Marekani akiwa kwenye Wheelchair?
HapanaSasa kama Uganda wanafanya ndiyo Daud Bashite afanye na yeye? Kwa kuwa Uganda hawajasemwa na marekani ni ruksa Daud Bashite aendelee kuwatesa watu?
Unamshangilia nani? Pom nini? Malawiti hawa! Shauri yako. Ukiona mtu anamshangilia mmarekani kwa Afrika, ujue ufahamu uko hoi. Hakuna nchi iliyosaidiwa na US ktk Africa hii na ikaendelea. Sitegemei chochote chema toka US!Gwamanywa endelea kujitoa ufahamu tu....Habari ya Mjini ni MIKE POMPEO kumla BAN BASHITE kwa KUUA WATU.
Kuwanyima watu haki ya kuishi ni hao mashoga ndiyo wanaopiganiwa tatizo mnaongea hisia zenu na siyo uhalisiajohnthebaptist, Na kuhusu kuwanyima binadamu wenzake haki ya kuishi Gamanywa hajaiona kaona ushoga tu, huyu ndiyo hao hao akina Bulldozer.
Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe nawe hata hujui unachangia nini. Nimeamua kukupuuza tu.Kuwanyima watu haki ya kuishi ni hao mashoga ndiyo wanaopiganiwa tatizo mnaongea hisia zenu na siyo uhalisia
Raia yupi,shoga?Haki za shoga zilindwe,zipi,za kuingiliwa kinyume na maumbile!Mungu anawaona na laana iko juu yenu.Ngozi nyeusi ni laana!!
Eti hawa ndio viongozi wa kiroho wanaotakiwa kuona haki za raia zinalindwa na kuiheshimiwa!!
Askofu Gamanywa ambaye ni mjumbe wa kamati ya amani na juzikati aliliombea taifa pale Ikulu katika utiaji saini mkataba wa Barrick na Serikali amesema Marekani inamuonea Makonda.
Askofu Gamanywa amesisitiza kuwa ushoga ni katazo mbele za Mungu na ni dhambi isiyosameheka.
Gamanywa amedai kuwa Makonda ni kiongozi hodari, shujaa na mwenye uthubutu na kwamba hapa Tanzania hakuna mtu mwenye ubavu wa kuikemea Marekani kama alivyofanya Makonda.
Askofu Gamanywa ameitaka Marekani ijitafakari juu ya uamuzi wake usio wa haki.
Source: Ibadani BCIC - Mbezi jogoo
Huyu askofu mjasiliadini type ya mwamposa,Askofu Gamanywa ambaye ni mjumbe wa kamati ya amani na juzikati aliliombea taifa pale Ikulu katika utiaji saini mkataba wa Barrick na Serikali amesema Marekani inamuonea Makonda.
Askofu Gamanywa amesisitiza kuwa ushoga ni katazo mbele za Mungu na ni dhambi isiyosameheka.
Gamanywa amedai kuwa Makonda ni kiongozi hodari, shujaa na mwenye uthubutu na kwamba hapa Tanzania hakuna mtu mwenye ubavu wa kuikemea Marekani kama alivyofanya Makonda.
Askofu Gamanywa ameitaka Marekani ijitafakari juu ya uamuzi wake usio wa haki.
Source: Ibadani BCIC - Mbezi jogoo
Kuna madhehebu mengine tena yanajiita kongwe hayawezi kukemea ushoga hadharani kwa kuwa ushoga tayari upo ndani ya madhehebu yao kongwe.Kwanza ukijua ni dhehebu gani analiongoza huwezi kuwa na maswali juu ya kauli yake
Sent using Jamii Forums mobile app
Wale wanaotumiwa na chadema siku hizi wako wapi?
Mheshimiwa sana pompelo atuambie kitendo cha kumuua General wa vita kule iran ilikua sahii , au yeye hana haki ya kuishi?Wapendwa maaskofu mnao tafuta mkate wenyu wa kila siku, Muogopeni Mungu!!! Usishabikie tu kumtetea DAB kwa sasa hivi. Jua kwamba, tatizo sio yeye kutoenda US, tatizo ni je, ametambua yaliyo andikwa kwenye ile barua ya Pompeo?? Msomeeni, msaidieni aielewe. Kama kaja kwenu kusema kuwa, ameonewa kwa kuichukia dhambi mwambieni kuwa; Barua ya Mr. Pompeo imesema mengi sana makubwa ya kutisha kuwa yeye RC wa Darisalama anatenda maovu. Mfano; Atiii; Anazuia haki za watu wengine kuishi. Sio kuishi kwa raha zao za kishoga bali kuishi yaani anawakatisha uhai.
Mh Baba askofu, naomba nenda tu ukatubu. Hao waumini ulio wadanganya leo hii ni wengi mno. Ukawaambia ati DAB amenyimwa kuingia US kwa sababu ya kuipinga dhambi ya ushoga. No, hiyo si kweli hata kidogo. Askofu nakusahihisha. Usiangukie mtego huu. We ni mtu wa maana sana ila ukifanya mchezo utajidhalilisha. Tutakuona kama Msaka tonge.