PreGE2025 Askofu Gwajima ajibu mapigo. Asema Gwajimanization ni kusema ukweli hata kama hauwapendezi walioko madarakani

PreGE2025 Askofu Gwajima ajibu mapigo. Asema Gwajimanization ni kusema ukweli hata kama hauwapendezi walioko madarakani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Giza na Nuru havibishani na kushindana, Gwajima mnamchongea kichwa yake inajaa kwa sifa anazopewa na soon jina lake litasahaulika.
jina litasahaulikaji mtu anayetetea wananchi waTanganyika wanaouawa na kunyanyasika nchini mwao kisa kikundi fulani kinachong'ang'ania madaraka.
 
Kauli hii iungwe mkono

IMG_20250531_183808_864.jpg
 
Gwajima yuko sahihi.

Nimekuwa nikijiuliza hivi huyu Rais ni nani hasa ambaye amekuwa akimshauri mambo yake? Hivi kulikuwa na sababu gani hasa ya yeye Rais wa nchi kujibu ile Hoja ya Askofu Gwajima kwa namna ile aliyojibu?? Kulikuwa na sababu yoyote ile ya msingi KWA yeye kujibu Hoja nzito za Gwajima kwa kutoa lugha ya taarabu, mipasho na kejeli namna ile? Kwa nini Rais huyu ameshindwa kabisa kusoma alama za nyakati???

Suala hili la Watu kutekwa, kuteswa, kupotezwa, kubakwa, kulawitiwa au kuuawa wakiwa mikononi mwa Maaskari wa Majeshi ya Serikali ni vitendo vibaya sana kupita kiasi. Hakuna Mtu hata mmoja ambaye tunatarajia kwamba anaweza kuunga mkono vitendo viovu vya uhalifu mbaya wa namna hii, isipokuwa Waovu wenyewe wanaotekeleza vitendo hivi. Rais wa nchi alipaswa aidha kuungana na Askofu Gwajima au angechagua kukaa kimya kuliko kujitokeza hadharani na kuunga mkono uhalifu kwa kupingana na Askofu Gwajima ambaye anaonekana kwamba anapinga uhalifu huu. Mimi binafsi bado sijajua bayana Rais hasa amekumbwa na tatizo gani. Namshauri ajaribu kufanya utafiti wake wa kina kabisa kuhusiana na kisa/suala la kuuawa kwa aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa India, Mama Indira Ghandi pamoja na mienendo yake Mama huyo miezi michache kabla ya siku ya kuuawa kwake.
Uko sahihi kbs, ila ulichosahau ni kuwa yule ni mwanamke, Tena mwanamke wa pwani nje ya urais!
 
Hero wako ni nani, Samia? Unamtetea kwa sababu ya sera zake, au pesa, cheo, mamlaka aliyokupa kuwapiga, kuwatesa kwa pesa.

Unamtetea kwa madaraka aliyokupa kuwauwa Watanzania wanaopenda haki.

kuwaumiza wanaotetea haki hata za vizazi vyako vyote vinavyokuja? Kama sisi Nyerere alivyotupigania tukapata Taifa huru.
So your hero ni Gwajima?
 
Wakuu,

Anaandika Askofu Gwajima masaaa kadhaa baada ya Rais Samia kumpa vitasa hadharani.

Nyie huyu baba ana ujasiri!

"Gwajimanization ni ujasiri usiotetereka wa kusema ukweli, haijalishi ukweli huo ni mchungu au hauwapendezi walioko madarakani. Ni dhamira thabiti ya kutetea maslahi ya Taifa kuliko maslahi binafsi na ni kuinua sauti kwa uthubutu mkubwa bila kuyumba kiasi cha kuisababisha ivume ndani ya himaya za mamlaka na kutikisa misingi ya ufisadi na dhuluma"

View attachment 3351939
"
Gwajima amesahau kwamba yeye mwenyewe amedhulumu hali za watu anaelewa kwamba huo ubunge hakushinda , halafu anajifanya mtu wa Mungu
 
Hivi kiongozi akiongelea masuala yanayoendelea au kutokea nchini, hasa mabaya au ya hovyo bila kujali itikadi yake anakua anaongelea serikali au chama tawala? Kwasababu naona watu wanahaha huko juu.
 
Hivi kiongozi akiongelea masuala yanayoendelea au kutokea nchini, hasa mabaya au ya hovyo bila kujali itikadi yake anakua anaongelea serikali au chama tawala? Kwasababu naona watu wanahaha huko juu.
Mkuu hoja yako ni muhimu.
Kwanini tuna kiongozi?
Kwanini tumemuweka pale?
Kutetea nini? Mafisadi, uhuni?
 
Hueweleki, umekunywa, konyagi ngapi, umelipwa kiasi gani kutukana?
Huwezi kuelewa kwasababu huna huo upeo wa kuelewa

I am pro Tz, ninaiangalia Kwa upanga zaidi ya U-chakandumuz wako

Sina chama na Naamini on Falsafa za Alina Nyerere na wenzake

I will never respect watu aina ya gwajiboy who swing based on what is in there for them

Now go play with you fellow kids
 
Mkuu hoja yako ni muhimu.
Kwanini tuna kiongozi?
Kwanini tumemuweka pale?
Kutetea nini? Mafisadi, uhuni?
Nani kamuweka kiongozi pale? Wewe? Una huo uwezo?

The damage of disrespecting structures is bigger thwt short term flaws

DONT think watu wamelala

Watu wako kazini to fix issues
 
Mkuu hoja yako ni muhimu.
Kwanini tuna kiongozi?
Kwanini tumemuweka pale?
Kutetea nini? Mafisadi, uhuni?
Ndio nashangaa, tuna viongozi ambao hawawezi kukemea au kuhoji serikali kisa tu wapo chama kimoja. Kazi yao ni kusifia na kujikomba komba hata kama nchi inaenda gizani. Wanasahau kuwa wao ni wawakilishi wa wananchi kwa serikali.
 
Huwezi kuelewa kwasababu huna huo upeo wa kuelewa

I am pro Tz, ninaiangalia Kwa upanga zaidi ya U-chakandumuz wako

Sina chama na Naamini on Falsafa za Alina Nyerere na wenzake

I will never respect watu aina ya gwajiboy who swing based on what is in there for them

Now go play with you fellow kids
Angalia watu gani wanauza maliasili za Taifa. Unatetea wahuni wote.

Usingepewa pesa, cheo, kazi kutetea uovu nafsi yako isingejikita kuwatesa Watanganyika, kuwadhulumu haki zao, kutetea uovu, uonevu, haki ya kuishi.
 
Wakuu,

Anaandika Askofu Gwajima masaaa kadhaa baada ya Rais Samia kumpa vitasa hadharani.

Nyie huyu baba ana ujasiri!

"Gwajimanization ni ujasiri usiotetereka wa kusema ukweli, haijalishi ukweli huo ni mchungu au hauwapendezi walioko madarakani. Ni dhamira thabiti ya kutetea maslahi ya Taifa kuliko maslahi binafsi na ni kuinua sauti kwa uthubutu mkubwa bila kuyumba kiasi cha kuisababisha ivume ndani ya himaya za mamlaka na kutikisa misingi ya ufisadi na dhuluma"

View attachment 3351939
"
This is Gwaji boy I know
 
Ndio nashangaa, tuna viongozi ambao hawawezi kukemea au kuhoji serikali kisa tu wapo chama kimoja. Kazi yao ni kusifia na kujikomba komba hata kama nchi inaenda gizani. Wanasahau kuwa wao ni wawakilishi wa wananchi kwa serikali.
Chama ni nini? Ni umoja kusimamia maslahi ya wengi.

Tanzania chama kinasimamia maslahi ya Rais, ufisadi, utekaji, ubakaji, ulawiti. Nyerere asingekubali huu uhuni.
 
Unaangalia watu gani wanauza maliasili za Taifa. Unatetea wahuni wote.

Usingepewa pesa, cheo, kazi kutetea uovu nafsi yako ingekuwa kuwatesa Watanganyika haki?
Sijawahi kuwatesa wqtanganyika Sina hoyo nguvu wala nafasi

Tatizo huna hoja

Now what is your main hoja?
 
Back
Top Bottom