Leo nimekaa nikaiskiliza video nzima ya Askofu Gwajima Youtube kitu nilichogundua ni kwamba Gwajima ana chuki binafsi kwa Rais Samia but ametumia kigezo tu cha chanjo kupitisha chuki zake.
Point kubwa aliyozungumza Gwajima ni kwamba tukichanjwa tunaweza kuwa tumewekewa chip na wazungu wakawa wanatuvcontrol wanavyotaka, mara baada ya muda tunaweza kuwa mazombi, mara chanjo ni mpango wa shetani na taasisi yake.
Mara nyingi alikuwa anakomaa kumu attack mtu japo alikuwa hataji lakini kwa akili ya kawaida utaelewa. Gwajima ametoa lugha za kashfa kwamba wanaoruhusu chanjo akili zao wameweka likizo. Mara anadai wamelipwa hela, mara anasema ni taasisi za mashetani.
Gwajima akawaambia waumini wake kuna watu wanawaambia mchome ila wao hawachomi wanachoma maji. Mwisho wa siku kamaliza kwa kusema ataombea wote wanaochoma wafe aliyechomwa afe anayechoma afe, hata atakayechoma maji afe.
Hii ni chuki ya wazi wazi, Gwajima hana point za msingi juu ya kupinga chanjo wala hana point za kisayansi anaongea upotoshaji, lakini kubwa inaonekana anamchukia sana Rais Samia.
Kama Gwajima anajua mabeberu wanampango wakutumaliza basi, angewaambia waumini wake wasikanyage tena hospitali maana kule ndio zimejaa dawa za kibeberu.