Ila tukijaga hapo kwenye kuingizwa microchip ndo nachekaga kufa[emoji23][emoji23][emoji23]
Me angekua mume wangu hiyo aibu hata siiwezi aisee
Mambo haya huwa yanaanzaga taratibu na Leo hii babu zetu wa enzi za miaka 1880s wakifufuka wakayaona haya ambayo leo hii tunayafanya kwa kushabikia kila kitu tunacholetewa ni aibu kubwa
Hatua moja ndio mwanzo wa hatua nyingine.
Ukoloni wa kifikra ni ukoloni mbaya sana bora hata ukoloni wa kuichumi unaweza kushindia magimbi na ukaendelea kuishi.
Tunatawaliwa na mataifa ya nje kwa sababu ya ujinga wetu wa kufikiri kwamba sisi si chochote mbele yao na hata vizazi vyetu vitarithi hii tabia ya fikra za kitumwa na imefikia hatua hakuna tena tegemeo baina yetu sio viongozi au wananchi.
Jiulize nchi ya China iliwachanja wananchi wake karibia watu bilioni moja plus ili kufanikiwa kudhibiti korona.
Serikali haina mbinu za kukabiliana na korona kilichobaki ni kuimba wimbo wa chanjo wakati wananchi wengi wakionekana kuzipinga
Watafute mbinu zingine za kukabiliana na korona sio kushabikia chanjo huku hatua za mwanzo za kukabiliana na korona hazizingatiwi
Huko mashukeni, vyuoni, vyombo vya usafiri, viwanja vya michezo,masokoni, sherehe, matamasha, ziara ya viongozi, makongamano n.k yanaendelea Kama kawaida Sasa hii ni serikali au sirikali