Uchaguzi 2020 Askofu Gwajima: Anayetakiwa kuchechemea ili CCM tushinde, atachechemea...

Uchaguzi 2020 Askofu Gwajima: Anayetakiwa kuchechemea ili CCM tushinde, atachechemea...

Gwajima yupi? Huyu mbaguzi wa kikabila na aliewaahidi waislaam kugeuza Miskiti kuwa sunday school?

Hivi mnapoteza muda kujadili mtu mwenye itikadi za kibaguzi?
 
mwaka huu kawe pamenoga sana!
Gwajima kanogesha mchezo.....
 
Huyu naye asituchoshe
Hawezi kujifananisha na Halima
Halima kakomaa kisiasa sasa wewe umekomaa ushamba na udwanzi


Maajabu ya CHADEMA mtu ambaye hajakomaa kisiasa walimuweka chimbo NYETI KAMATINI yule mtu wa jalalani wakamsafisha.

Mpaka kijana mwenzetu MNYIKA akakaa kimyaa.

Angarau sasa anapumua.
 
Mfananano wa Bi. KIDUDE na Halima Mdee

Wote hawakuolewa/hajaolewa.

Wote hawakuwa na watoto.

Pia kusema neno Bi Kidude sio lazima amaanishe yule Marehemu msanii, tusubiri ufafanuzi wake.
 
Huyu askofu uchwara kala maharage ya wapi?

Kwanini anamtumia Bi kidude kuwatusi wengine?

Anamfahamu vizuri marehemu Bi kidude kweli? An icon of swahili music!

Yaani kwake mtu kuwa Bibi kidude ni tusi?
Hahahaaaa...... Hajamtendea haki rip!
 
Mechi kali na tamu katika ligi ya mwaka huu ambazo hupaswi kuzikosa ni hizi za kundi B kati ya:
1. Mdee vs Gwajima
2. Heche vs Waitara
3. Sugu vs Tulia
4. Lema vs Gambo

Na kiingilio ni bure. Viwanja vitafurika katika mechi hizo. Yaani Tanzania kipindi cha uchaguzi mkuu ni burudani kuliko ya Olimpics! Ni furaha tupu. Refree ni NEC na Linsemen ni IGP akisaidiwana yule wa Akiba.

Mechi ambazo wala hazihitaji hata kuzitazama kwa sababu mshindi anajulikana, tena kwa goli 100 kwa nunge, ni zile za Kundi A.
 
Yaani huyu Gwajima kapotea njia Bora angeendelea na kazi yake ya kura Kondoo tu huku kachemka
IMG_20200821_175230.jpg
IMG_20200821_175244.jpg
 
Askofu Josephat Gwajima amesema kuwa yule Bi. Kidude wa Chadema ni halali yake na kazi ya kumshinda ataifanya law hakika.

Amemueleza Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu kuwa wasiwe na wasiwasi kwani ugoro umeingia puani sasa ni mwendo wa chafya tu.

Ameyasema hayo akitoa neno katika mkutano wa Kampeni wa Makamu wa Rais, katika Uwanja wa Mwembeyanga Temeke.View attachment 1559570
Mbona huyu askofu anatumia maneno ya mipasho kama sio kiongozi wa dini
 
Back
Top Bottom