Uchaguzi 2020 Askofu Gwajima atangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Kawe

Kama Msukuma na Kibajaji wameingia mjengoni tena zaidi ya mara moja ndo uone ajabu kwa Gwajima?
 
Ukiona kiongozi wa dini anaanza kugombea nafasi za kisiasa changanya na zako
 
Hilo la kwanza nakubaliana na wewe la pili hapana pesa tayari anayo
 
Uchaguzi wa mwaka huu hautegemei sanduku la kura
 
Katika watu niliokuwa natamani siku moja aingie bungeni ni Gwajima.

Anakuaga na point sana za maswala mbalimbali yahusuyo nchi coz ana exposure kubwa ya nje.
Hizo point zake unafikiri zinatakiwa kwenye siasa! Pale alipo kama mchungaji yeye ndiye kiongozi na hakuna wa kumpinga, akisema wote wanaitikia Amen. Kwenye siasa kwanza atakuwa chini ya chama cha siasa ambacho kina uongozi; ni lazima sasa yeye ndiye aseme Amen vinginevyo.

Pili ajue kuwa atakapozungumza kuna watakaomwambia hapo siyo, jambo ambalo kwake hakulizoea.
Mimbari ya kidini ni tofauti sana na mimbari ya kisiasa!
 
Labda tunajifariji tunaojaribu kumbeza huyu Baba Askofu, Achilia mbali tunayosikia kumhusu yeye, lakini ukweli kabisa, iwe mvua liwe jua, Mdee Kwa heri
 
Amemrahisishia Halima Mdee kazi asante sana.
 
Viongozi wa dini na wale wa kisiasa wanafanana katika jambo moja kuu, ambalo ni kuishi kwa jasho la mlalahoi. Tangu enzi na enzi, mlalahoi amefungwa nira za siasa na dini (unyonyaji uliohalalishwa).

Kiongozi anayetafuta madaraka ya kidini na kisiasa kwa wakati mmoja ni mlafi anayepaswa kuogopwa kuliko ukoma. Kwa mustakabali mwema wa nchi, CCM ikiwa ni chama kilichoshika hatamu za uongozi, kina umuhimu wa kutowahusisha viongozi wa dini kwenye siasa zake, ikiwa ni njia ya kupunguza unyonywaji wa wanyonge.

Mchungaji Gwajima analo jukwaa (kanisa lake) la kuzungumzia na kutetea haki, hivyo kutafuta tena jukwaa la kisiasa (ubunge) siyo muhimu kwa mtu asiye na tamaa ya madaraka.
 
Kwa hiyo Chops kitakuwa kina paki pale Mjengoni kwa nje ama wapi.?Nitakuwa miongoni mwa wageni.Sikh ya kuapishwa nipande japo Helikopita

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…