Uchaguzi 2020 Askofu Gwajima atangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Kawe

Hebu acha mzaha! Gwajima ana hofu ya Mungu? hivi kwanini huwa mnalichezea hivyo jina la Mungu? yaani anavyokusanya misukule pale ubungo tayari unamwita Gwajima ana hofu ya Mungu? Hebu tupinge.....Gwajima akipitishwa na CCM hawezi kushinda jimbo lolote hapa Dar es Salaa, hawezi! Kama amewapiga upofu wafuasi wake sio sisi wapiga kura wa Kawe!
 
Haya mambo yamekatazwa ktk maandiko ,huwezi kutumikia mabwana wawili. Siamini Ngwajima yupo tayari kumwadu mwanadamu badala ya Muumba pekee.

Katika hilo hafuati maandiko, na ni sawa tu
 
Nakumbuka aliwahi kusema yeye hahitaji kuwa mbunge wala mkuu wa mkoa maana cheo alichonacho ni kikubwa kulinganisha na hivyo vya kisiasa. Leo tena imekuaje?
 
Kama ulivyo mpumbavu wewe kwa mbowe
 
Nikajua anakuja kugombea huku nyumbani Koromije atusaidie kuondoa kero yeye anahangaika na jimbo ambalo lina mbunge shupavu.
Wajameni wajameni.!!
Alima mdee hawez kusimama na gwajima huu ndio ukwel gwajima anaongea Sana
 
Unawajua waumini wa Gwajima lakini.... ni zile typ za ulipo tupo!

Hukuona walivyokua wanamtetea kipindi cha ile video?

Yaani Gwajima Akiwaambia vaa kijani wote watavaa!
Akiwaambia vaaa kaki wote watavaa!

Yani sijui kawalisha nini Aisee!
 

Mkuu, uweke akiba ya maneno.

Safari hii miss Mdee ana mtihani.

Zengwe lishaundwa hapo kuna moshi mweupe na mzito juu ya Kawe.

Kawe na Kigamboni kwa sasa ni majimbo ya kimkakati.
 
Dunia ina mambo.

Kikatiba yuko sahihi kabisa.

Kiuhalisia hata ccm hawawezi kumpitisha labda viti maalum.

Hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kumpigia kura gwajima kua mbunge wake.
Viti maalum labda avae sketi
 
Gwajima alisema yeye ni zaidi ya mbunge na kwamba hana mpango wa kugombea ubunge imekuwaje tena mbona amekuwa mtu wa kauli mbili!
kama sijasahau aliwahi sema yeye ni zaidi ya rais yaan rais ni cheo kidogo sana kwake
 
Yaani Ubunge wa sasa ni hatari CCM watakusanya fedha kwenye kuchukua form just imagine ubungo wagombea 20,kibamba wamefika 17!! Nashangaa Kitila kakaidi maagizo ya JIWE anagombea Ubungo ina maana anapiga chini ukatibu mkuu WM.


Jamaa amukubali kutishika na mikwala ya Migulu Mchemba?! [emoji3][emoji3][emoji3]

Kumbe sometimes mikwala inasaidia !

Eti mamba kwenye kina sijui nini na nini. [emoji3][emoji3]

Hadithi za kungulu mwoga kukimbiza mabawa yake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…