#COVID19 Askofu Gwajima: Baadhi ya viongozi walioonekana wakichanjwa, wame-fake ili kuwahadaa wananchi

#COVID19 Askofu Gwajima: Baadhi ya viongozi walioonekana wakichanjwa, wame-fake ili kuwahadaa wananchi

"Baadhi ya viongozi walioonekana wakichanjwa, wame-fake ili kuwahadaa wananchi. Inapofika mahali pa kuilinda Tanzania dhidi ya majanga, simuogopi mtu yeyote, siogopo kitu chochote hatuchanjwi"

Askofu Josephat Gwajima akizungumza kanisani kwake leo.!

My Take
Hii imevuka mipaka. Lakini mambo haya hayatokei bahati mbaya. Samia Suluhu umemuonea sana Mh.Mbowe acha upigwe tu mpaka utie akili.
CCM na Serikali yake inamuogopa sana Askofu Rashid Gwajima ameishika pabaya wamebakia kubweka bweka tu lakini hawana cha kumfanya kwani Gwajima ana 'watu'
 
Nchi ya ajabu sana, rais anatukanwa wazi wazi lakini kwa kuwa anayefanya hivyo ni askofu inachukuliwa poa tu lakini angekuwa sheikh au muislam tu tayari tungesikia kapewa kesi ya ugaidi au kapotea kabisa.
Mimi ni mwanaCCM,naheshimu maoni ya mtu.
Sasa wewe ndugu yangu,kwenye hicho kinachosemwa kuwa kasema Gwajima,tusi alilotukanwa Rais ni lipi?
Kuna tusi kweli hapo?
Au uchochezi tu!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi nimechanjwa na kwa siku 3 kutokea nilipochanjwa nilikuwa na headache ya hatari kuweza kufanya lolote. Hata kutembelea JF tu ilikuwa kwa mbinde.

SSH aliendelea na shughuli zake?!

Nimeongea na wenzangu wengi bado sijaweza kuwa na kanzidata ya kutosha kabla ya kumrukia ki Gwajiboy.

Kuna habari kuwa serikalini walishapata Pfizer mapema tu.

Simwungi mkono Gwajiboy kuhamasisha watu wasichanjwe, ila kwenye kuchanjwa wakuu hawa Gwajiboy anaweza kuwa na point.

Cc: Jumbe Brown BAK
Mie nimedungwa na niliendelea na kazi kama kawa sehemu nilodungwa ilikuwa na maumivu siku mbili basi
 
Gwajima anatukuna viongozi waliochanja live live.Huyu anatakiwa adhibitishe kauli au apigwe kipigo cha bilioni 7.5 hadi akili zikae sawa.
 
..mimi sijaiona video.

..lakini kama kinachoripotiwa ni kweli basi Gwajima amevuka mpaka.

..kudai kwamba viongozi wamechomwa chanjo feki ili kuwalaghai wananchi ni tuhuma nzito.

..na kama tuhuma hizo si za kweli basi Gwajima atakuwa amekashifu na kutukana.
Siyo kwamba hao viongozi wamejifanya kuchanjwa na siyo kuchomwa chanjo feki? Au kuna chanjo feki zimeingizwa nchini?
 
Uhuru ni wa maoni sio facts, huwezi kusema soda za Coca Cola zina sumu halafu useme ni uhuru wa maoni.

Kusema viongozi wamechoma chanjo feki ni factual matter. Akitakiwa athibitishe ataweza?
Yule Afisa Elimu wa Arusha anawakilisha viongozi wa serikali walioigiza kichanja
 
Siyo kwamba hao viongozi wamejifanya kuchanjwa na siyo kuchomwa chanjo feki? Au kuna chanjo feki zimeingizwa nchini?

..Gwajima anatakiwa atoe ushahidi.

..Hizi ni tuhuma nzito kutolewa na Mheshimiwa mbunge.

..Kwenye post yako umetumia alama ya kuuliza. Maana yake huna uhakika.

..Gwajima alitakiwa apige " mkwaju " kiasi kwamba hakuna mtu atakayetumia alama ya kuuliza.
 
Mimi ni mwanaCCM,naheshimu maoni ya mtu.
Sasa wewe ndugu yangu,kwenye hicho kinachosemwa kuwa kasema Gwajima,tusi alilotukanwa Rais ni lipi?
Kuna tusi kweli hapo?
Au uchochezi tu!?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi si sio mwana CCM mwenzako tena ukome kunitajia tajia hayo mavyama yenu, kama ungesoma hata michango ya wengine pia na kama ungekuwa na akili timamu usingeniuliza upuuzi.
 
Nchi ya ajabu sana, rais anatukanwa wazi wazi lakini kwa kuwa anayefanya hivyo ni askofu inachukuliwa poa tu lakini angekuwa sheikh au muislam tu tayari tungesikia kapewa kesi ya ugaidi au kapotea kabisa.
CCM wanajua wanachofanya. Yaani hapo wananchi waache katiba mpya waelekeze nguvu kwa Gwajima
 
Na kimiss sana kile Chuma cha 'Mjeremani' kilikuwa hatar jiddah!

Mabalozi leo hii wanaenda Mahakamani kisutu, Amnest International inaipa maelekezo Serikali huru?

Kweli Tulipoteza Hariri March, 17

..mbona balozi wa Ujerumani alimtoa Tundu Lissu lockup?

..mbona balozi, tena mwanamke, alimsindikiza Lissu mpaka airport alikopanda ndege?

..yule ubabe ilikuwa ni kwetu Watz, akitishwa na mabeberu alikuwa akinywea.
 
Mimi si sio mwana CCM mwenzako tena ukome kunitajia tajia hayo mavyama yenu, kama ungesoma hata michango ya wengine pia na kama ungekuwa na akili timamu usingeniuliza upuuzi.
Ukiishia kusoma comment matusi utayakuta. Ni kama wewe ulinitusi hapa.
Haya na wewe ni maoni yako.

Watapima tu hapa kati ya mimi na wewe nani si timamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie nimedungwa na niliendelea na kazi kama kawa sehemu nilodungwa ilikuwa na maumivu siku mbili basi

Ndiyo maana nasema ningali nina huisha kanzidata yangu.

1. Severe headache
2. Loss of sense of balance
3. Body malaise
4. Kusikia kiu mfululizo
5. Mwili kuhisi baridi

Kwa siku 3 sikuweza kufanya lolote.

Ya wale wakuu kwenye uzinduzi imekuwa ikinizunguka mawazoni.

Maendeleo yote kuhusiana na kupata chanjo kimsingi niliyaweka hapa:

#COVID19 - Chanjo - Mrejesho: Wizara tambueni changamoto hizi

Comment #37 inahusika zaidi.
 
"Baadhi ya viongozi walioonekana wakichanjwa, wame-fake ili kuwahadaa wananchi. Inapofika mahali pa kuilinda Tanzania dhidi ya majanga, simuogopi mtu yeyote, siogopo kitu chochote hatuchanjwi"

Askofu Josephat Gwajima akizungumza kanisani kwake leo.!

My Take
Hii imevuka mipaka. Lakini mambo haya hayatokei bahati mbaya. Samia Suluhu umemuonea sana Mh.Mbowe acha upigwe tu mpaka utie akili.
Kimeumana katika kujenga mnara wa Babeli!
 
Back
Top Bottom