Uchaguzi 2020 Askofu Gwajima: Naimudu Kawe. Mimi sio kilaza, nilienda Marekani mwaka jana na nimeshaandika vitabu 5 kwa kijapani, vipo Amazon

Uchaguzi 2020 Askofu Gwajima: Naimudu Kawe. Mimi sio kilaza, nilienda Marekani mwaka jana na nimeshaandika vitabu 5 kwa kijapani, vipo Amazon

Jamaa ana akili copywright kama Bashite na kama kuna tofauti basi ni ndogo ndogo sana lakini naamini ukipima DNA zao nafikiri zitakuwa chain moja
Nikichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Kawe nitaweka Ambulance kwenye kila Kata, watu wangu watakimbizwa hospitalini kwa haraka na jambo hili ni jepesi halihitaji Manispaa wala halihitaji Serikali"- Josephat Gwajima.
 
Mkuu Mstaafu, The Retired, kwanza its good to know, kuwa wewe ni mwana Kawe mwenzangu na ni kweli Kawe ina changamoto nyingi na uhitaji wa ambulance sii miongoni mwa changamoto za Kawe...
P
Ambulance ina umuhimu, tena sana, lkn kwa mtu anayejitambua, acha hawa lumpen proletariats, class unconscious people, huwezi kumshawishi akupe kura kwa vile utaleta ambulance KAWE! Kwa Dar na foleni zake na poln ya Kawe, si kitu chenye ushawishi mkubwa kumgeuza mtu IMANI akupe kura!

I can imagine unapeleka ambulance Kalebezo ambako kwenda hospitali ya wilaya Ukerewe kwa mgonjwa mahututi/mja mzito it can have an impact kwa mazingira ya vijijini kutoka kwenye dispensary! Siyo mjini kama Kawe! Do you see my point!?
 
Kinachompa ushindi Gwajima ni ahadi zake kwa sisi wakazi wa kawe ikiwemo ambulance comrade

Ni kweli kabisa, akishinda ubunge muombe akununulie madaftari ili uende elimu ya jioni ukajifunze kuandika kwa usahihi, huku ukijikita zaidi kwenye somo la matumizi ya koma na nukta.
 
Unajidanganya, Kawe hatuhitaji ambulance. Kwanza ambulance zinatupeleka wapi na zitabeba wangapi kwa popln ya Kawe? Kila mgonjwa wa Kawe akiugua ataipata wapi? and by the way wanaugua wangapi a day in Kawe kuwa kipaumbele chao ziwe ambulance?...
Anajua wazi kuwa huduma za afya ni hafifu wananchi wanasumbuliwa na maradhi kwani kila siku wanafurika kwa manabii ili waponywe, hivyo usimlaumu kwa kufichua chama chake kimeshindwa kuboresha huduma za afya badala yake kinajenga majengo ya zahanati na kudhani ndiyo suluhu ya tiba.
 
Ni kweli kabisa, akishinda ubunge muombe akununulie madaftari ili uende elimu ya jioni ukajifunze kuandika kwa usahihi, huku ukijikita zaidi kwenye somo la matumizi ya koma na nukta.
Naona umepata kichaka cha kujificha. Sawa mkuu nitafanya ivyo
 
Ambulance ina umuhimu, tena sana, lkn kwa mtu anayejitambua, acha hawa lumpen proletariats, class unconscious people, huwezi kumshawishi akupe kura kwa vile utaleta ambulance KAWE! Kwa Dar na foleni zake na poln ya Kawe, si kitu chenye ushawishi mkubwa kumgeuza mtu IMANI akupe kura! I can imagine unapeleka ambulance Kalebezo ambako kwenda hospitali ya wilaya Ukerewe kwa mgonjwa mahututi/mja mzito it can have an impact kwa mazingira ya vijijini kutoka kwenye dispensary! Siyo mjini kama Kawe! Do you see my point!?
Lazima kuwe na proportional kwenye kila kitu...hizo ambulance kwa kila kata zitakuwa zinapeleka wapi hao wagonjwa. Kabla ya kufikiria ambulance lazima kufikiria haya kwanza Elimu ya afya kwa watu wa eneo husika. Vituo vya afya vyenye wahudumu qualified. Vituo vya afya vyenye vifaa tiba vya kutosha.

Kumbuka ambulance sio taxi na gari maalum za kubeba wagonjwa wa dharura hivyo inatakiwa kuwa na mahitaji yote maalum pamoja na wahudumu wenye ujuzi husika.

Sasa kila kata ambulance zitakuwa zinapaki wapi kwa usimamizi wa nani? Zitakuwa zinahudumiwa na nani? Ambulance sio vinq'ora na maandishi makubwa ubavuni ile ni EMERGENCY LIFE SAVER TOOL...Sio tax kuwa unaweza kupaki hata kona bar
 
BIBI KIDUDE ALISHAWAHI PELEKA ATA BAJAJI KWENYE KATA IPI NDANI YA UTAWALA WAKE WA MIAKA KUMI?
MWAMBIENI BIBI KIDUDE ATUACHIE JIMBO HARAKA SAANAA.
Tumheshimu Bi Kidude (RIP), tusiwape watu wa ajabu ajabu majina ya mashujaa wetu!.
Tufanye kampeni za heshima na kistaarabu, Halima Mdee ni Mhe. Tumuite Mhe. Halima Mdee ila tumuulize
Uchaguzi 2020 - Je, Halima Mdee amefanya nini Kawe kwa miaka 10 ya ubunge wake kustahili kuendelea? Sikia ya Askofu Gwajima, 28 Oktoba fanya uamuzi sahihi
P
 
Anajua wazi kuwa huduma za afya ni hafifu wananchi wanasumbuliwa na maradhi kwani kila siku wanafurika kwa manabii ili waponywe, hivyo usimlaumu kwa kufichua chama chake kimeshindwa kuboresha huduma za afya badala yake kinajenga majengo ya zahanati na kudhani ndiyo suluhu ya tiba.
Lakini katika hali ya kawaida kabisa je inawezekana kweli kuweka ambulance kwenye kila kata? Hizi sio tax tukumbuke
 
Hapana hagombei kuwa mganga mkuu wa hospital. Anagombea nafasi ya ubunge ambayo mpaka sasa njia ni nyeupe ya kushinda.

Wewe jilishe matango pori kwani huzijui siasa za Kawe; kwani 2015 Kippi Warioba hakuteuliwa na ccm? Kilichompata Kippi ndio kinachomgoja Gwajima!
 
Kununua ambulance ni wajibu wa serikali na sio wa mbunge kwa pesa zake za mfukoni. Kama Gwajima anataka kununua ambulance kutokana na umasikini uliopo kawe, sio lazima apewe ubunge ndio afanye hilo. Huko kijijini anakotokea Gwajima kuna hali mbaya sana kuliko kawe, angewasaidia huko. Mlimbambikia kesi Halima ili ikifika wakati wa uchaguzi mseme alikuwa ni mzee wa mahakama? Bado mnaamini kuwa watu wamelala hivyo kiasi hawajui lolote?
Nafikiri yeye kama mkazi wa Kawe ametambua umuhimu wa Ambulance na mahitaji yake. Kusema kwamba atanunua Ambulance ni jambo jema ili kukabiliana na mahitaji ya watu wa Kawe. Kwamba ananunua kwa pesa zake hilo sio tatizo maana ni kuchangia maendeleo,maana sio kila kitu kinachotakiwa kufanywa na serikali lazima serikali iachiwe hayo majukumu. Hofu iliyokukumba ni baada ya kujua Halima hatashinda Kawe,habari za kubambikiwa kesi ni hearsays tu. Mahakama ndio chombo cha mwisho kutoa majibu juu ya hilo
 
Ni kweli kabisa, akishinda ubunge muombe akununulie madaftari ili uende elimu ya jioni ukajifunze kuandika kwa usahihi, huku ukijikita zaidi kwenye somo la matumizi ya koma na nukta.
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Lakini katika hali ya kawaida kabisa je inawezekana kweli kuweka ambulance kwenye kila kata? Hizi sio tax tukumbuke
Yeye mia yake ni kufikisha ujumbe kuwa serikali ya CCM ameshindwa kuboresha huduma za afya kiasi wananchi wanasumbuliwa na maradhi, kumbuka huyu ni nabii wa uponyaji anayajua mafuriko ya watu walioshindwa kupata bima ya afya badala yake wanajaa kanisani kwake awaponye.
 
Wewe umeona wapi ambulance ni tax? Comrade mbona unauliza maswali ya kijinga?

Naomba nikueleshe kwa weledi upate ufahamu utakaokusaidia mbeleni. Ambulance ni chombo cha kuokoa uhai kwa dharura hivyo sio gari ya mchezo kama gwajima anavyodhani ni gari inayohitajika kuwa na vifaa vingi ndani yake vya kuokoa maisha..SIO MALI...KUOKOA MAISHA
Kusema ataweka ambulance kila kata ya KAWE maana yake ni kwamba kata zote za kawe zina wananchi wanahitaji kukimbizwa hospital muda wote.

Sasa hizo ambulance utaegesha wapi? Zitasimamiwa na nani? Zitahudumiwa na nani? Hivi unajua ya kwamba mpaka mgonjwa apakiwe kwenye ambulance ni mgonjwa mahututi au ambaye anahitaji tiba ya dharura?

Ambulance sio gari ya kupaki mitaani kama zile gari za makampuni ya ulinzi..Ambulance ni kama kituo kidogo cha afya cha dharura kinachotembea kwa nia ya kumuwahisha mgonjwa sehemu atakapopata huduma zaidi
 
Yeye mia yake ni kufikisha ujumbe kuwa serikali ya CCM ameshindwa kuboresha huduma za afya kiasi wananchi wanasumbuliwa na maradhi, kumbuka huyu ni nabii wa uponyaji anayajua mafuriko ya watu walioshindwa kupata bima ya afya badala yake wanajaa kanisani kwake awaponye.
Mzugaji tu huyu nusu ya wagonjwa wake ni psychological problems kutokana na ugumu na changamoto za maisha na matango pori waliyolishwa na matangazo na wafuasi wake kuwa jamaa ni booonge la mponyaji.
 
Naomba nikueleshe kwa weledi upate ufahamu utakaokusaidia mbeleni Ambulance ni chombo cha kuokoa uhai kwa dharura hivyo sio gari ya mchezo kama gwajima anavyodhani Ni gari inayohitajika kuwa na vifaa vingi ndani yake vya kuokoa maisha..SIO MALI..
Mimi nayajua yote hayo uliyoandika hakuna kipya. Unajua jimbo la kawe lina kata ngapi?
 
Mimi nayajua yote hayo uliyoandika hakuna kipya. Unajua jimbo la kawe lina kata ngapi?
Kawe sio eneo la wagonjwa mahututi kwenye kila kata kwamba muda wote ambulance zinahitajika kuwawahisha hospital
 
Back
Top Bottom