Mkuu Mstaafu, The Retired, kwanza its good to know, kuwa wewe ni mwana Kawe mwenzangu na ni kweli Kawe ina changamoto nyingi na uhitaji wa ambulance sii miongoni mwa changamoto za Kawe. Ungelisaidia sana jukwaa hili kama ungezitaja hizo changamoto ambazo Gwajima hataweza kuzitatua.
Mimi nilikuwepo pale Bunju, hiyo ya ambulance ni moja tuu kati ya mengi, Gwajima amezungumzia changamoto nyingi ikiwemo ya barabara, ajira kwa vijana, mikopo kwa vikundi vya vijana, kinamama na walemavu, amezungumzia kufungua chuo cha veta cha ufundi. Amezungumzia mambo mengi, makubwa mazuri
Kwa faida ya wengi, huyu hapa Gwajima msikilizeni
Kwa kumalizia, maadam wewe ni mwana Kawe na unazijua changamoto za Kawe, sasa kwa vile kuna mtu amekaa miaka 10 Kawe na anataka kuendelea, hebu utueleza amefanya nini Kawe kwa miaka yake yote 10 ili kustahili kuongezewa?.
Uchaguzi 2020 - Je, Halima Mdee amefanya nini Kawe kwa miaka 10 ya ubunge wake kustahili kuendelea? Sikia ya Askofu Gwajima, 28 Oktoba fanya uamuzi sahihi
Ujumbe kwa wana Kawe, kufanya kosa sii kosa, kosa kurudia kosa!. Kawe tumefanya sana makosa kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita, tarehe 28 October, tujitokeze kwa wingi kufanya kweli na kamwe tusirudie makosa!.
P