Askofu Gwajima: Nchi imekosa maono, kila Rais anakuja na lake, ipo siku tutajuta

INAPASWA KUWEPO CHOMBO CHA MPANGO WA NCHI NA SIO CHAMA. CHAMA KINACHOSHINDANIA KUONGOZA NCHIKITENGENEZE ILANI INAYOENDANA NA MPANGO WA NCHI NA SERIKALI YA CHAMA HICHO KUITEKELEZA MPANGO HUO. SIO CHAMA/ MTU KUKURUPUKA NA KUFANYA YAKE. HAPO KUNAKUWA HAKUNA MUUNGABIKO NA NIVURUGU NA KUPOTEZA FEDHA ZA NCHI BURE. CHOMBO HICHO KITAKUWA ESTABLUSHED KIKATIBA NA KITAKUWA KIZALENDO ZAIDI KWA NCHI. VYAMA VIWE KAMA MKANDARASI ANAYEHITAJI TENDA YA DHAMANA YA KUTEKELEZA MPANGO/ MALENGO YA NCHI
 
Ni bahati mbaya wengi hamjamuelewa Gwajima, kwanza kaongea mambo sensible sana. Hapa kuna point moja wengi hamjamuelewa, alichosema ni lazima huo mpango utungiwe sheria yake kama mnavyofanya kwenye budget ya kila mwaka. Gwajima anapiga spana kwamba lazima kuwepo na inforcement ya huo mpango/Dira ili atayekuja atakwe kufanya hivyo.

Askofu Gwajima ana maanisha kwamba lazima tuwe na sera zinazotabirika, zisiwe za kubadilika kila muhula. Mfano mpango wa miaka 100 kuhusu uwe na utekeleza wake na uainishwe kwa awamu 20 (100/5) kila awamu ipewe kipande cha kutekeleza bila kutoka kwenye mstari uliochorwa wa utekelezaji.
Mpango ungweza kuonyesha bwawa la mwl nyerere lingetekelezwa awamu say; ya 10 maaana yake awamu ya 5 isingekuwa na mandate kufanya hivyo, yenyewe ingetekeleza kilichopitishwa kutekelezwa kwenye awamu ya 5.
Hongera sana Gwajima umewatoa tongotongo japo wanakutuhumu kuwa wewe ni su....ma gn
 
Mbona aliyepita aliacha yamtangulizi wake akaanzisha mapya na hakusema?
Tulieni nyie sukuma Gang zamu yenu ilishapita.
Ya mtangulizi wake yapi? Ya kutalii duniani kila wiki?
 
Mbona nchi ilishadondokea pua kitambo tu na yeye Gwajima ni mbunhe wa zao linalotokana na nchi kutokuwa na raisi mwenye maono
 
Planning System bila Planning Commission!!!!!
 
Anza kudai katiba mpya🐒🐒🐒
Your browser is not able to display this video.
 
KWAni ni dhambi kuhamia Taifa lingine?

Huko majuu hapana .

Ndo maana napambana wangu wakaishi huko majuu alafu wajifunze unyonyaji wa huko wake wawanyonye ndugu zao huku .

Ova
 
Huyu alishaleta treni aliyoahidi? Alishapeleka Wana kawe Burmingham ?
 
Mbona aliyepita aliacha yamtangulizi wake akaanzisha mapya na hakusema?
Tulieni nyie sukuma Gang zamu yenu ilishapita.
Ni wale wale tu wa kulialia. Anachoshindwa kuelewa ni kwamba SSH anakwenda nje ya nchi ili aweze kupata pesa nyingi zitakazokwenda kumalizia miradi iliyoachwa na JPM. Hivyo anaendeleza vision ile ile ya JPM.

Na sio haki kusema kila rais anakuja na la kwake, akumbuke kuwa kila rais anafanya kazi kwa kutekeleza ilani ya CCM, hajitungii tu kutoka kichwani kwake yale anayokwenda kuyafanya.
 
Nadhani wengi tumemuelewa Gwajima vizuri sana isipokuwa watu wanataka Gwajima aseme wazi kwamba hiyo dira ya nchi iwe imo katika sheria za nchi !! Hapo automatically atakuwa ameigusa katiba !! Yeye hapo amepakwepa !!!
 
Mambo haya alianzisha Jiwe, sukuma gang hata mmoja hakuna aliyefungua mdomo wake. Sukuma gang muda wenu umeishapita.
 
Imefika nchi iwe na dira. Kuwe na serikaliambayo mipango yake ni madhubuti na utawala wake hauingiliwi na wanasiasa kwa sababu wao wanapita tu
 
Hivi kuhamia Dodoma na Bwawa la Nyerere zilikuwa kwenye ilani ya CCM?
 
Mbona aliyepita aliacha yamtangulizi wake akaanzisha mapya na hakusema?
Tulieni nyie sukuma Gang zamu yenu ilishapita.
Nako mbona alilisemea sana bungeni hilo,hata kipindi cha mwendazake alilisema sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…