Askofu Gwajima: Nchi imekosa maono, kila Rais anakuja na lake, ipo siku tutajuta

Askofu Gwajima: Nchi imekosa maono, kila Rais anakuja na lake, ipo siku tutajuta

Ni wale wale tu wa kulialia. Anachoshindwa kuelewa ni kwamba SSH anakwenda nje ya nchi ili aweze kupata pesa nyingi zitakazokwenda kumalizia miradi iliyoachwa na JPM. Hivyo anaendeleza vision ile ile ya JPM.

Na sio haki kusema kila rais anakuja na la kwake, akumbuke kuwa kila rais anafanya kazi kwa kutekeleza ilani ya CCM, hajitungii tu kutoka kichwani kwake yale anayokwenda kuyafanya.
Sio haki vipi wakati tuliona Magufuli akiacha ya kikwete na kufanya yake? Ulikua hujaziliwa au umeamua kujitia upofu?
 
Ni bahati mbaya wengi hamjamuelewa Gwajima, kwanza kaongea mambo sensible sana. Hapa kuna point moja wengi hamjamuelewa, alichosema ni lazima huo mpango utungiwe sheria yake kama mnavyofanya kwenye budget ya kila mwaka. Gwajima anapiga spana kwamba lazima kuwepo na inforcement ya huo mpango/Dira ili atayekuja atakwe kufanya hivyo.

Askofu Gwajima ana maanisha kwamba lazima tuwe na sera zinazotabirika, zisiwe za kubadilika kila muhula. Mfano mpango wa miaka 100 kuhusu uwe na utekeleza wake na uainishwe kwa awamu 20 (100/5) kila awamu ipewe kipande cha kutekeleza bila kutoka kwenye mstari uliochorwa wa utekelezaji.
Mpango ungweza kuonyesha bwawa la mwl nyerere lingetekelezwa awamu say; ya 10 maaana yake awamu ya 5 isingekuwa na mandate kufanya hivyo, yenyewe ingetekeleza kilichopitishwa kutekelezwa kwenye awamu ya 5.
Hongera sana Gwajima umewatoa tongotongo japo wanakutuhumu kuwa wewe ni su....ma gn
Haya alitakiwa kuyasema awamu Ile ya 5, maana ndio awamu iliyogeuza meza ghafla na kuongoza Mambo ambayo hayakuepo, nchi ikalazimika kukopa mikopo mikubwa na deni likakua, miradi haijakamilika na deni ni kubwa
 
Askofu Gwajima ambaye ni Mbunge wa Kawe kasema nchi imekosa maono kwa kuwa kila Rais akiingia madarakani anaachana na ya mtangulizi wake, kuongeza hilo kamwe halitaweza kutuletea maendeleo

Gwajima amesema nchi inatakiwa kuwa na mikakati yake ya muda mrefu na kila rais anayeingia madarakani anaongozwa na mikakati na maono hayo na sio kuleta vitu vyake vipya, ama sivyo anaweza akaja Rais wa ajabu ambaye atavuruga kila kitu na hakuna atakeyeweza kumbana kwa kuwa hakuna maono.

Huyu msanii hebu apeleke wapiga kura wake Birmingham kwanza. Aache sanaa huko bungeni
 
Haya alitakiwa kuyasema awamu Ile ya 5, maana ndio awamu iliyogeuza meza ghafla na kuongoza Mambo ambayo hayakuepo, nchi ikalazimika kukopa mikopo mikubwa na deni likakua, miradi haijakamilika na deni ni kubwa
Hakuwepo bungeni angesema vipi?
Wakati ulikubaliwa ni sasa
 
Haya alitakiwa kuyasema awamu Ile ya 5, maana ndio awamu iliyogeuza meza ghafla na kuongoza Mambo ambayo hayakuepo, nchi ikalazimika kukopa mikopo mikubwa na deni likakua, miradi haijakamilika na deni ni kubwa
Pumbavu, alijiwekea mambo na wakati mnasema yeye Magufuli kafanya yote aliyoacha kikwete na Nyerere?

Kwa hiyo Leo tena mnampa miradi yote aliyoifanya ilikuwa yake
 
Askofu Gwajima ambaye ni Mbunge wa Kawe kasema nchi imekosa maono kwa kuwa kila Rais akiingia madarakani anaachana na ya mtangulizi wake, kuongeza hilo kamwe halitaweza kutuletea maendeleo

Gwajima amesema nchi inatakiwa kuwa na mikakati yake ya muda mrefu na kila rais anayeingia madarakani anaongozwa na mikakati na maono hayo na sio kuleta vitu vyake vipya, ama sivyo anaweza akaja Rais wa ajabu ambaye atavuruga kila kitu na hakuna atakeyeweza kumbana kwa kuwa hakuna maono.

Kwanza sijaelewa anaongea nini na ni kipi hicho kimebadilika hasa,angeenda na mifano.

Pili lazima kuwe na tofauti ya mawazo ya namna ya kutekeleza mipanga ya serikali..

Nachojua mimi serikali ina mipango ya miaka 5 mitano ambayo ndio inatakelezwa kwa kutumia sera tofauti tofauti na mipango tofauti tofauti..

Na sera lazima ziwe zinabadilika kulingana na nyakati kwa hiyo hapa anadanganya bila ushahidi.

Mwisho kuna mipango ya miaka 5 na vision 2025 sasa kama amezoea kudanganya mazuzu wake kule kijiweni kwake aendelee huko.
 
Pumbavu, alijiwekea mambo na wakati mnasema yeye Magufuli kafanya yote aliyoacha kikwete na Nyerere?

Kwa hiyo Leo tena mnampa miradi yote aliyoifanya ilikuwa yake
Kumbe alimalizia Katiba mpya? Alimalizia gesi Mtwara? Alimalizia kukuza kilimo?

Mambo ya kuhamia Dodoma yalikuwa na ulazima gani kufanya wakati hapohapo tulikuwa na miradi mikubwa ya Reli na Bwawa?

Kigongo Busisi ilikuwa kwenye ilani?
 
Huyu hakupaswa kuwa bungeni kabisa angeendelea na kazi yake ya kuchunga kondo za bwana, ila jpm kwa sabb za ukabila na ukanda kaleta wakina Tom and Jerry
Pamoja na MADHAIFU na upuuzi wake lakini,hii kauli yake ni sahihi!
 
Kumbe alimalizia Katiba mpya? Alimalizia gesi Mtwara? Alimalizia kukuza kilimo?

Mambo ya kuhamia Dodoma yalikuwa na ulazima gani kufanya wakati hapohapo tulikuwa na miradi mikubwa ya Reli na Bwawa?

Kigongo Busisi ilikuwa kwenye ilani?
Wizi mtupu
 
Mbona Tz tuna sera na mipango kazi mizuri tu shida ni "katiba" ya hii nchi imempa rais mamlaka ya kupenya kila kona na hakuna wa kumbabaisha.
Mfano hayati jiwe alizikomba pesa za mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kuikopesha serikali yake alipoona mifuko yote imechalala akaona isiwe tabu akaamrisha mara moja kuanzishwe mfuko mmoja tu wa hifadhi ya jamii, bado haitoshi akapitisha sheria mpya ya kikokotoo ya 25% na kufuta kabsa fao la kujitoa.
 
Askofu Gwajima ambaye ni Mbunge wa Kawe kasema nchi imekosa maono kwa kuwa kila Rais akiingia madarakani anaachana na ya mtangulizi wake, kuongeza hilo kamwe halitaweza kutuletea maendeleo

Gwajima amesema nchi inatakiwa kuwa na mikakati yake ya muda mrefu na kila rais anayeingia madarakani anaongozwa na mikakati na maono hayo na sio kuleta vitu vyake vipya, ama sivyo anaweza akaja Rais wa ajabu ambaye atavuruga kila kitu na hakuna atakeyeweza kumbana kwa kuwa hakuna maono.

Yeye anaongoza kanisa la peke yake kwa mda mrefu. Mbona hatuona Hayo maono huko kwake? Aache viongozi wetu watekeleze kazi zao kwa amani.
 
Ana point sana..

Ila sasa Rais huku afrika ni kama mfalme hivi..
 
Mpaka sasa sijaona Samia kwenda tofauti na mtangulizi wake kwa maana " framework" ya maendeleo tena zaidi Samia ameiboresha zaidi kwa kutekeleza majukumu ya ndani kwa kutengeneza good cooperation frameworks na mataifa mengine. Aliyetoka kwenye mpango wa marais waliopita ni JPM, maana kama asingehamisha magoli muda huu ingekuwa mikoa yote ishaunganshwa kwa lami na nusu au robo tatu za makao makuu ya Wilaya pia yameunganishwa na lami. Pia muda huu tungekuwa na mjadala wa iwapo Mtwara liwe Jiji au ...?
 
Kama sio umri wako mdogo,basi akili au ufahamu wako ni mbilikimo kabsa, wakati mwingine ni kupoteza mda kubishana na watu wenye mitizamo fyongo na akili zenye matege,ukitaka udhibitishe ushupavu na usahihi wa jpm,msikilize rais mstaafu mwinyi,msikilize hayati mkapa,msikilize pia rais mstaafu jakaya kikwete,wamewahi kutoa maoni gn juu ya uchapakazi wa jpm na ushupavu wake ktk maendeleo na uadilifu,
 
Ila ana point, acheni ushabiki, ikiwa kila Rais akija anafanya yake, au anaacha ya mtangulizi wake na kufanya mengine mapya, ni hatari sana, sbb kuna mambo ni uti wa mgongo wa nchi, sasa ukikuta labda haijakamilika na kuiacha njiani, ni kukosa mipango ya maendeleo endelevu
Hana hoja kama hakubali kuwa na KATIBA MPYA!!, Ili haya anayosema yafikiwe lazima tuwe na nyenzo/Taasisi imara zitakazosimamia sera za maendeleo ya muda mrefu.
 
..Ni mambo yapi yaliyoachwa? Maana kama ni miradi Mama Samia kwa kiasi kikubwa anajitahidi kumalizia miradi mikubwa iliyoachwa na marehemu huku pia akianzisha na mengine.
Unajitoa ufahamu siyo? Ni mjinga tu ndiye atakayesema Samia anaendeleza ya Magufuli. Samia anabomoa ya Magufuli kwa kasi ya ajabu. Hivyo vi-miradi vichache siyo dira ya nchi. Hapa watu wanazungumzia jinsi nchi inavyoendeshwa.
 
Hana hoja kama hakubali kuwa na KATIBA MPYA!!, Ili haya anayosema yafikiwe lazima tuwe na nyenzo/Taasisi imara zitakazosimamia sera za maendeleo ya muda mrefu.
Inabidi tuwaze kwa mapana. Gwajima maelezo yake yote yamelenga kwenye katiba mpya japo hajasema. Sijui kama ameacha kusema kwa sababu anaogopa au hajui kuwa anachotaka hakiwezi kufanyika bila katiba mpya lakini ukweli ni kuwa bila katiba yenye kutoa huo mwongozo, ni bure. Dira za namna hii zinapangwa kitaalam, kwa kuwashirikisha wananchi wa vyama vyote huku wakiongozwa na wataalam bila kuweka itikadi za siasa kabisa. Muafaka ukishafikiwa na majority wakakubali basi inabaki ni utekelezaji tu.
 
  • Thanks
Reactions: Exy
Ni wale wale tu wa kulialia. Anachoshindwa kuelewa ni kwamba SSH anakwenda nje ya nchi ili aweze kupata pesa nyingi zitakazokwenda kumalizia miradi iliyoachwa na JPM. Hivyo anaendeleza vision ile ile ya JPM.

Na sio haki kusema kila rais anakuja na la kwake, akumbuke kuwa kila rais anafanya kazi kwa kutekeleza ilani ya CCM, hajitungii tu kutoka kichwani kwake yale anayokwenda kuyafanya.
Unaona mazuzu haya! Nje ya nchi ndiko maendeleo yanakotokea? Niambia nchi ambayo imeendelea kwa sababu marais wake walikuwa wanasafiri sana nje! Nchi inajengwa na wananchi siyo fedha kutoka nje. Miafika ndiyo tulivyo, kazi kuwaza vya bure tu. Bila shaka wewe asili yako ni kutoka kwenye ule mkoa ambao wakazi wake husambaa nchi nzima kuomba omba ndiyo maana una mawazo fyongo namna hii.
 
Back
Top Bottom