Askofu Gwajima: Nchi imekosa maono, kila Rais anakuja na lake, ipo siku tutajuta

Je bado Kuna sababu za yeye kuficha jambo ambalo lina masilahi n Taifa?. Kama hawezi kusema hivyo huo ni unafiki.
 
Magufuli ndiyo alikuwa mtu sahihi kuja kuiongoza hii nchi baada ya kuharibiwa na vibaka kwa miaka 30 isiyo na neema. Huyu Mama kaja kuiharibu tena kwa kurudisha useless viongozi wenye uchu na wizi wa mali za umma. Hatuna tena mwelekeo, yeye kazi yake ni kubwabwaja tu.
 
Mbona aliyepita aliacha yamtangulizi wake akaanzisha mapya na hakusema?
Tulieni nyie sukuma Gang zamu yenu ilishapita.

Ulitaka aendeleze UFISADI wa Kikwete sio? Ebu tumia akili kidogo kuwa Gwajima anawapa somo juu ya kuwa na Katiba mpya itakayokuwa na dira aya muda mrefu wa maendeleo ya nchi ambayo haitabadirika kufuatana na utashi wa mtawala!!!
 
Je bado Kuna sababu za yeye kuficha jambo ambalo lina masilahi n Taifa?. Kama hawezi kusema hivyo huo ni unafiki.
Ni kweli kabisa. Ni unafiki. Wanasiasa wengi au niseme watanzania wengi ni wanafiki. Unakumbuka siku ile Ndugai aliposema tusipende kukopakopa fedha? Gwajima alimwandikia msg akasema ''This is Ndugai I know...'' Alipoona Ndugai anashambuliwa akamkana na kusema hakuwa anamaanisha kumuunga mkono. Anyways, wanasiasa wanaangalia matumbo yao. Juzi Magufuli akiwa hai alikuwa anasifiwa mno lekini leo walewale wamebadilika na wanamkashifu, akiwemo aliyekuwa makamu wake, hivyo unafiki ni jadi.
 
JPM alikuwa anaiua hiyo nchi maana he was not a leader rather a non-programmed robot. Hao wanasiasa uliowarejea hapo huenda huwajui vizuri. Mimi nawajua vizuri sana hao. Walikuwa wakimpaka mafuta tu kwa mgongo wa chupa. Na ukitaka kujua umbilikimo wangu wa akili, just njoo hapa viunga vya Charles Bridge then uliza Dan Zwangendaba utapewa habari zangu.
 
Upo sahihi kabisa, nchi yetu inajiendea tu bila maono yenye kueleweka, kila mtawala anayekuja anajiona yeye ndiye mwenye kujua kila kitu hivyo hufanya atakalo.

Tumekuwa kama meli iliyopoteza dira, haijui inapolekea, hii inasikitisha sana.
 
Uongo, Kila Rais anayeingia Marekani huwa na sera zake.
Ni kweli ana hoja ndo sababu nchi kama Marekani rais anakabidhiwa national policy ambayo inampa direction ya nchi. Shida yangu ni moja tuu, je Magufuli angekuwa hai Gwajima angeongea haya?
 
Ni kiongozi gani Samia kamuweka ambaye Magufuli hakumuweka...Maana huyo Makamba kama ni mwizi kweli JPM alikuwa nae kwa kipindi kirefu tu kwenye baraza la mawaziri, hata Nape na mbarawa
 
Ningekuwa karibu ningemuuliza ubunge ulipataje

zungumzia point yake mjibu point aliyosema. ubunge aliupata kwa kura za wananchi mimi moja wapo nilimpa kura yangu na familia yangu na ndugu zangu woote
 
Yaani Gwajima anataka rais abanwe na maono badala ya katiba na sheria, na sera za nchi.

Aliyetukusanyia hawa mbuzi bungeni alituweza kweli.
 
Ni kweli ana hoja ndo sababu nchi kama Marekani rais anakabidhiwa national policy ambayo inampa direction ya nchi. Shida yangu ni moja tuu, je Magufuli angekuwa hai Gwajima angeongea haya?

Hii inatakiwa iwe kisheria kwenye katiba na vyama vya siasa vitengeneze sera zake kutokana hiyo jinsi ya kuitekeleza. Je sera ya shithole countries iko kwenye national policy za USA maana rais wa Trump aliitamka?
 
Tatizo ni MACHAWA yakifanikiwa kumuweka mgombea wao ,kwa mfano nyinyi SUKUMA GANG mkifanikiwa kumuweka mgombea wenu MH MWIGULU NCHEMBA 2025 nadhani atavuruga vyote
 
Gwajima alishapoteza sifa tangu siku ile alipokubali kuuza uaskofu wake kwa chakula cha dengu.
 
Huyu hakupaswa kuwa bungeni kabisa angeendelea na kazi yake ya kuchunga kondo za bwana, ila jpm kwa sabb za ukabila na ukanda kaleta wakina Tom and Jerry
Binafsi sikubaliani nae kwa sababu amesema hatuna vision wakati kwenye mfano kasema tunayo inayoishia 2025/2026..

Sasa anajua ilianza lini kutekelezwa? Point kuu ingekuwa kwamba hiyo vision itungiwe sheria isiache inaelea.

Mfano Nyerere aliacha tuu kwamba Serikali inatakiwa kuhamia Dodoma,alitunga sheria lakini hakuhamia.

Mwendazake alipohamia katungia sheria kabisaa kwamba hakuna option tena.

So vision zetu tuzipe nguvu za kisheria tusiache option ya utashi wa kisiasa hata kama zipo..
 
Ameshindwa kusema kwamba tatizo ni katiba mpya. Ameona akisema hvyo wenzie watamnanga lkn alimaanisha tatizo ni katiba itakayo tengeneza taasisi imara ambayo ndio itamuongoza mtu na siyo mtu kui guide taasisi
πŸ’ͺπŸ½πŸ‘πŸ½
 
Bwawa la umeme la Nyerere halikuwepo sio tuu kwenye ilani bali kwenye vision ya 2025/2026.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…