1. Janssen imefanyiwa majaribio South Africa na ilionyesha mafanikio makubwa kupambana na South African variant link hii hapa👇
Demonstrated strong neutralizing antibody activity against the Delta (B.1.617.2) variant Persistent immune responses through at least eight months
www.jnj.com
2. Pia unaposema kwamba hazikujaribiwa kwa mtu mweusi, wakati tunaambiwa majaribio yafanyike si tuligoma tukasema sisi sio nyani wa kufanyiwa majaribio ? Nchi zenye majority ya watu weusi ambazo zilifanyiwa trials nakumbuka ilikuwa South Africa na Kenya na tuliwadhihaki kuwa wamekubali kutolewa chambo.
3. Janssen vaccine haitumii mRNA technology na ndio maana ni rahisi kuletwa Africa , mRNA inahitaji uhifadhi wa joto la chini sana kitu ambacho ni ngumu kupatikana kwenye hizi nchi zetu
View attachment 1867812
View attachment 1867813
4. Hizo namba za efficacy kwa vaccines hazina maana inapotumika kulinganisha ubora wa chanjo kwa sababu efficacy figures zinapatikana katika trials, mfano Pfizer inaweza kufanyiwa trials kipindi maambukizi ni madogo nchi tofauti halafu ikaja AstraZeneca ikafanyiwa trials muda maambukizi yako juu na nchi tofauti...mpaka sasa hakuna research iliyofanyika kuangalia ipi ni chanjo bora zaidi. Kinachoangaliwa ni uwezo wa chanjo kumlinda mtu kama atapata maambukizi basi asiumwe ugonjwa mkali utakaopelekea yeye kulazwa ama kufariki , aliyepewa chanjo ana uwezekano mkubwa kuumwa kidogo sana ama kutokuumwa kabisa kama atapata maabukizi ya corona na hivyo kuufanya ugonjwa kutokuwa tishio.
5. Madhara ya chanjo ya Janssen ambayo yaliongelewa sana ni damu kuganda ambapo probability ni 0.000007% ( watu 7 kati ya milioni 1). Uwezekano wa damu kuganda iwapo utapata maambukizi ya CoVID-19 bila chanjo yoyote ni kama umelazwa hospitali ni 0.05%(mtu 1 kati ya 20) na kama upo nyumbani na ugonjwa wa usio mkali ni 0.01% (mtu 1 kati ya 100).
Tatizo taarifa zinaweza kubadilishwa kuweka hofu tu juu ya chanjo bila kuangalia hizo hizo risks zilizopo kama ukiachwa ukaambukizwa hiyo COVID-19.
Watu wamekunywa bupiji,nimricaf, covidol bila kujua humo ndani kuna nini, majaribio yamefanyikia wapi na side effects ni nini, wengine mpaka wamesababisha figo kufeli kwa kuchanganya mitishamba lakini hakuna aliyekuwa na wasi wasi nazo...jiulize hizo nyungu zina efficacy kiasi gani?