#COVID19 Askofu Gwajima: Ni ujinga kuruhusu Taifa zima kuwa 'Experiment' kwa sababu tuna haraka ya Corona

#COVID19 Askofu Gwajima: Ni ujinga kuruhusu Taifa zima kuwa 'Experiment' kwa sababu tuna haraka ya Corona

Nimefurahi askofu kamaliza na sentence ya kujaradia taifa letu...Amen🙏big up Askofu Gwajima!
 
Ficha ujinga wako kidogo usijionyeshe sana

Ujinga ni relative jombi. Wewe funika wa kwako. Who's Gwajima in relation to the specialists wa virusi kama hawa:

"Akizungumza na Mwananchi, Mtaalamu wa maicobaolojia na virusi kutoka Chuo kikuu cha Muhimbili (Muhas), Dk Joel Manyahi alisema aina hiyo ya kirusi kina tabia ya kujibadilisha mara kwa mara."

Mambo yenu na kina msukuma msukuma bakini nayo wenyewe.
 
Ujinga ni relative jombi. Wewe funika wa kwako. Who's Gwajima in relation to the specialists wa virusi kama hawa:

"Akizungumza na Mwananchi, Mtaalamu wa maicobaolojia na virusi kutoka Chuo kikuu cha Muhimbili (Muhas), Dk Joel Manyahi alisema aina hiyo ya kirusi kina tabia ya kujibadilisha mara kwa mara."

Mambo yenu na kina msukuma msukuma bakini nayo wenyewe.
Umebaki na akili za kuvukia barabara jitahidi wanao wasione ujinga wako
 
Gwajima ni mpotoshaji mkubwa sana mengi aliyoongea ni upotishaji mtupu watalaam waje kumkosoa mimi siyo mtaalam lakini huyu jamaa ni muongo mkubwa apuuziwe hivi dunia nzima na majirani zetu ni wajinga sana huyu Gwajima ambae sio mtaalam ndio yuko sahihi watz tumejazwa ujinga sana
 
Lkn pmj na kuwa askfu was ufufuo na uzima kajitaidi kwenda deeper Sana ktk swal hili hvyo naiagiza kamati na tume iliyoundwa na mam Samia ijikite pia kwenye oja yake
 
*

Mheshimiwa Spika, naomba nikushukuru sana, nimshukuru pia Waziri wa Afya Dr Dorothy Gwajima pamoja na Naibu Waziri.Kwa dakika chache sana nataka kuzungumza kwa habari ya Chanjo za Corona ( Corona Vaccine ).

Niseme kwa ufupi kwamba ‘Mimi sipo kinyume na Chanjo za Corona wala sipo kinyume na chanjo yoyote na kwenye mazungumzo yangu mtu asininukuu kwamba napinga chanjo HAPANA! ‘ Kwasababu tayari Tanzania tulishachanjwa; Chanjo ya kifua kikuu,Chanjo ya surua, Chanjo ya kifaduro, Chanjo ya polio na sasa zipo chanjo zinazoenedelea kama chanjo ya homa ya Ini , kwahiyo siko kinyume na chanjo kwasababu tayari zipo Tanzania na watu wanaendelea kuzitumia. Kitu ambacho nipo makini nacho ni aina ya Chanjo inayoitwa Chanjo ya Corona Virus ilivyokuja na study yake. Chanjo hii ni tofauti na chanjo nyingine zote ambazo zimekuwepo Duniani.

Dunia imekuwa na chanjo zinazoitwa Attenuated Vaccine. Attenuation maana yake kwamba Virus wa Corona wanapunguzwa nguvu,wanaondolewa properties halafu wanaingizwa ndani ya mwili wa Mtu, halafu antibodies wanareact immunity inatengenezwa, na hii ndio aina ya chanjo ambayo ipo miaka yote na siku zote; na chanjo hii kukamilika inagharimu miaka 8 mpaka 10. Lakini chanjo hii inayoitwa ya Corona ni chanjo ya mwendokasi miezi 2, miezi 3, miezi 4 tayari, Unapojaribu kuuliza kwamba Chanjo hii kwanini imekuwa haraka sana na wakati kuna magonjwa mengi kama Malaria na mengine ambayo tungetegemea wafanye haraka haraka kupata chanjo ili watu waokolewe.

Wanasema sababu ya kwanza ni kwa sababu teknolojia imeongezeka, sababu ya pili ni kuwa Wame mobilize resources kutoka kwenye makampuni mengi duniani na sababu nyingine ni kuwa Ugonjwa ni Pandemic... Na mimi sikatai. Lakini mheshimiwa Naibu Spika teknolojia ya chanjo hii inaitwa mRNA. mRNA ni aina ya chanjo ambayo wanachukua Genetic material ya Virus halafu wanaingiza kwenye RNA ya mtu baadae, Wanasema kuwa haitaingiliana na Gene lakini wanasema wanaingiza zinaingizwa kwenye Cell ya mtu. Mheshimiwa Naibu Spika Utu wa mtu... tofauti ya mtu na mnyama ni RNA, DNA na Genes huo ndio utu wa mtu unatofautisha mtu na mnyama. Chanjo hii inaingia hadi kwenye RNA, DNA na kwenye Genes kwenye UTU WA MTU, Hatujajua baada ya chanjo hii atazaliwa mtu wa namna gani baada ya miaka 10, baada ya miaka 5, baada ya miaka 6 hatujajua mpaka leo. Na bahati mbaya sana Mheshimiwa Spika nifunguke kidogo na hekima yako ikikuruhusu utaniongezea muda kama ukiisha kwasababu ya hoja yangu ina NATIONAL CONCERN.

Mashirika duniani kwa mfano Marekani, kuna shirika ambalo linaruhusu dawa zianze kupitishwa linaitwa CDC ( Centre Of Disease and Control Prevention), shirika lingine linaitwa FDA ( Food And Drug Authority ). Haya ndio mashirika ya kimarekani yana-authorize dawa zote kwa ajili ya matumizi ya Binadamu, Chanjo hizi zote tunazoziona hizi hazijawa authorized na mashirika haya lakini kuna kishirika kidogo ambacho kinaitwa Emergency Use Authorization. Hili shirika linahidhinisha dawa zote ambazo ni za dharura, ambazo zinatakiwa ziende haraka na sheria za hawa Emergence Use Authorization ni kwamba kwasababu Dawa haijafanyiwa utafiti wa kutosha miaka mingi kwahiyo inaruhusiwa Emergence kwasababu ya uhitaji wa dunia, madhara yatakayo wapata wale hayapo juu ya hii kampuni bali zipo juu ya mtumiaji Mheshimiwa Naibu Spika.

Sasa najaribu kuwaza kwamba nikiangalia mfano chanjo ambazo zipo tayari zimesharuhusiwa kuanza kwa mfano kuna chanjo ya kwanza inaitwa Johnson Johnson imeruhusiwa na Marekani ambayo tarehe 27 February 2021 ndio ilikuwa authorized na Emergence Use Authorization lakini kwenye Website yao hao watengeneza Chanjo wenyewe wanasema madhara au Side effect ya Chanjo hii kwanza ni kushindwa kupumua sawa sawa, ya pili kuvimba kwenye uso na koo, tatu mapigo ya moyo kwenda mbio sana, nne Bad rashes kwenye mwili, tano ni Dizziness na sita Damu kuganda kwenye mwili. Sasa kama watengenezaji wa chanjo wenyewe kwenye website wanaonyesha kuna shida hiyo ni vizuri sisi tuwe makini, najua Mheshimiwa Rais kwa hekima yake ameunda kamati ambayo inafuatilia jambo hilo lakini kama Mbunge nina haja ya kudiscuss na ku-alert kwamba wawe makini wanapochagua aina ya chanjo hizi.

Chanjo ya aina ya pili inaitwa AstraZeneca ambayo imetengenezwa na Oxford kule UK ( United Kingdom ) yenyewe kwenye website yao wanasema side effect ya kwanza ni Damu kuganda na ya pili ni Kifo na kwenye kifo hapa wanasema wanaweza kufa watu kama kumi kati ya mia lakini kwenye Website yao wanaonyesha kuwa death may occur. Lakini dunia bila kufanya research au bila kuwaza watu wamekimbilia kupata Chanjo kwa sababu ya woga wa Corona.

Nyingine inaitwa Moderna ambayo ni ya USA na nyingine inaitwa Pfizer ambayo ni ya Ujerumani; kwa ujumla wa chanjo hizi zote zinaonyesha side effect ya kuganda damu, kushindwa kupumua na kifo. Sasa ni kweli tukikataa chanjo tunaweza kuwekewa ban ya kwenda Ulaya kwasababu hatujachanjwa, tunakabiliwa na uchaguzi mbaya sana ‘ TUCHANJWE KITU TUSICHOKIJUA SAWASAWA AU TUSICHANJWE TUZUILIWE KWENDA ULAYA’ Naomba sana wizara ya afya wajaribu kuangalia kwa makini sana swala la Chanjo. Waangalie madhara ya sasa na madhara ya siku zijazo juu ya taifa na jambo hili nila muhimu sana na sana.

Mheshimiwa Naibu Spika niruhusu niongeze kidogo, matatizo ambayo tunayo sisi nikufikiri kila kinachotoka Ulaya kinafaa kwetu and this is the problem we face. Our Colonizers, Wakoloni wetu walitujengea ufahamu kuwa kikitoka kwao kinafaa lakini jana kuna mtu anaitwa Dr Edward ambaye ni moja ya watu walioshiriki kutengeneza moja wapo ya chanjo alikuwa ameandika barua kwa Raisi wa Marekani ninarecord anasema ‘Anashauri hizi chanjo ziachwe mara moja kwasababu madhara yake ni makubwa kuliko faida yake ya prevention’.

Kwahiyo ninaiomba serikali yangu sikivu na Wizara ya Afya before we venture on what kind of Vaccine we should take, tunatakiwa tuwe na wataalum wetu wa hapa Number moja, wa analyze content kwasababu haya majina ya chanjo ni Business names lakini kuna Generic names. The Generic names include the content, kuna nini ndani ya chanjo, wa analyze matatizo yatakayotupata sisi tutakaochanjwa na watoto wetu baadae kwasababu shida ikiingia kwenye DNA ,Gene na RNA ndio Utu wa mtu inasend message miaka ijayo mtu azaliwe wa namna gani. Madhara yanaweza yasiwe leo ila 20, 30 years to come tunaweza tukawa na Watanzania wasioweza kufikiri vizuri wasio na maamuzi mazuri na Taifa letu litashindwa.

Ninaomba sana Wizara ya Afya before we know which method we implement tufanye due diligence ya kuifatilia hii chanjo ni ya namna gani na pia tusome website. Nataka niongezee jambo moja kuwa anything kule Marekani au Ulaya kuna organization inaitwa EMA ( EUROPEAN MEDICINE AGENCY) ambayo yenyewe ina authorize dawa zote zinazotumika, hizi Agency zote yaani Agency ya ulaya na Agency za Marekani hazija authorize zenyewe. Zimewekwa kwenye hizi organizations zinazo authorize dawa za Emergency na matokeo ya ku-authorize Emergence huyu aliyetengeneza dawa hana madhara ni wewe mwenyewe utajijua mwenyewe. Na wanasema kuwa inatumika huku inafanyiwa uchunguzi, Mheshimiwa Naibu Spika ni ujinga kuruhusu taifa zima kuwa experiment ya majaribio eti kwasababu tuna haraka ya Corona. I know Corona is dangerous Yes but it is more dangerous for we to allow all the Nation yaani watanzania wote Milioni 50 wachanjwe eti ndio tuwe tunaangalia majaribio na matokeo alafu tunaripoti kwenye hizi institutions. Ninaomba sana hili swala liangaliwe kwa makini lifanyiwe kazi na mwisho wa siku “ KILA SILAHA ITAKAYOFANYIKA JUU YETU HAITAFANIKIWA”View attachment 1781232
Kama ili niende Ulaya au Marekani ni lazima nichanje chanjo basi Ulaya na Marekani ni kwa heri kwa maana hata iweje sitachanja hizi chanjo, kama kufa wacha nife lakini siwezi kufanywa mtu wa kufanyiwa majaribio na matajiri waliotengana . Shukrani kwa kichwa Gwajima kutuletea darasa murua, hata huku kwao wengi wamegoma kuchanjwa na wanaishi
 
Hivi huyu mbulula anasoma conspiracy theories anapeleka Bungeni. Hakuna kanuni inayozuia kuongea mambo yasiyo ya kiutafuti bungeni? Hivi hizi akili kumbe huwa ni za Kisukuma maana Hayati nae yalikuwa mawazo yake

Sent from my vivo 1915 using JamiiForums mobile app
Ili usiwe mjinga mpinge kwa utafiti wako usio na conspiracy theories
 
Huko kote walikubali kuwa kuna ugonjwa wa COVID-19 na walishachukua hatua zote. Iweje kwa upande wa Tanzania 🇹🇿?
Mkuu ila pamoja tz not covid 19 free country lakini Hata ingekua free on covid 19 lazima taifa kujikita na kuatayari katika hatua zote za prevention namanisha
Primary prevention
Second prevention
Tertiary prevention and no way as anation we can escape to take measures as far as covid is concerned
 
Homa ya manjano ile Vaccine yake imeua watu zaidi ya laki 5 directly kabisa tokea iwe introduced mbona sijasikia mkiipiga marufuku na ndio kwanza tunatumia hiyo kila tukisafiri nje!!

Mkatae kwa sababu tu hamtaki ila msijustify eti madhara cjui nini.... Coz ikiwa hivyo inapaswa mpaka Radiotherapy isitishwe pale ocean road maana ile madhara yake ni makubwa sana kwa kila anayetumia tiba ile.

Tuache double standard
Kaka acha kutangaza fujo. Hizoi lakhi 5 waliokufa shauri ya Yellow Fever Vaccine umepata wapi?? Una ushuhuda? Sidhani.
Soma hapa: "2 Of the hundreds of millions given the yellow fever vaccine since it was introduced in 1936, there have been just 62 confirmed cases and 35 deaths from vaccine-associated viscerotropic disease, according to a 2016 study. It’s likely that cases have been missed in poor countries, but because the condition is so serious it is unlikely to go unnoticed in rich countries."
(Chanzo: What are the risks of dying from having the yellow fever vaccine?)
Kuhusu chanjo ya Korona sijui lugha hii "sisi ni majaribio" inatoka wapi??? Kila chanjo kilichopo sokoni imetumiwa kwa watu milioni pale Ualya, Amerika na Asia.
Matokeo ni mazuri, tofauti kidogo katika kiwango cha kinga. Madhara ya kawaida kama kila chanjo. Kama kila chanjo milioni wamepata, milioni wamekingwa, wachache wamepata hasara. Sawa na chanjo zote zinazotumiwa nchini hapa.
 
Hivi huyu mbulula anasoma conspiracy theories anapeleka Bungeni. Hakuna kanuni inayozuia kuongea mambo yasiyo ya kiutafuti bungeni? Hivi hizi akili kumbe huwa ni za Kisukuma maana Hayati nae yalikuwa mawazo yake

Sent from my vivo 1915 using JamiiForums mobile app
Mabeberu wamewakaririsha mtu akija na hoja ya kisayansi kuchallenge chanjo zao wanawakatisha tamaa kwa kuziita conspiracy theories bila kwenda in details kujibu hoja kisayansi.
 
Huyu bwana askofu wa kanisa la ufufuo na uzima ajue katukosea sana kwa kutofanya juhudi yoyote ya kumfufua mwendazake, hali akidai karama hiyo anayo.

Ana nini bado cha kutuambia sisi kuhusiana na Corona au lolote jingine huyu?
Unaongea upumbavu mtupu
 
Mkuu ila pamoja tz not covid 19 free country lakini Hata ingekua free on covid 19 lazima taifa kujikita na kuatayari katika hatua zote za prevention namanisha
Primary prevention
Second prevention
Tertiary prevention and no way as anation we can escape to take measures as far as covid is concerned
Hebu tusome wote hapa kuhusu hii habari ya Waziri wa afya, Dorothy Gwajima:


Kulingana na taarifa hii, ina maana sasa hivi COVID-19 ipo Tanzania 🇹🇿!
 
Mabeberu wamewakaririsha mtu akija na hoja ya kisayansi kuchallenge chanjo zao wanawakatisha tamaa kwa kuziita conspiracy theories bila kwenda in details kujibu hoja kisayansi.
Leo ndio amejua kuna Sayansi baada ya kudanganya watu kwamba anafufua kwa muda mrefu

Angekuwa mwanasayansi wangemjibu Wanasayansi lakini huyo mwanasiasa Mchaga atasema Nini zaidi ya Porojo.


Sent from my vivo 1915 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom