#COVID19 Askofu Gwajima: Ni ujinga kuruhusu Taifa zima kuwa 'Experiment' kwa sababu tuna haraka ya Corona

#COVID19 Askofu Gwajima: Ni ujinga kuruhusu Taifa zima kuwa 'Experiment' kwa sababu tuna haraka ya Corona

Chanjo si unajikinga tu bila kujali ugonjwa upo ama haupo!! Ni precautionary motive tu na ndio alichosema Rais kwamba hata kma Covid Haipo Tz ila wave ikija lazima ikute mmejiandaa.
Kwahiyo Serikali ya Tanzania 🇹🇿 inafanya maamuzi kwa kufuata mkumbo na kuangalia mataifa mengine yamefanyaje ili kujikinga na COVID-19?
 
Conclusion ya hili Jambo ni Kuwa anae kwenda Nje mwenyewe achanjwe Covid -19 na anaekuja nchini pia awe amechanjwa, nimeenda kariakoo zaidi ya mara 200 tena kwenye msongamano na hakuna corona kwa nini ulazimishe watu wachanjwe bila kuwa na basis za maana? hakuna cha PHD gani inayoongoza WHO hao wote ni ma agents tu wa makampuni yanayofanya biashara. Ni waulize leo pale kariakoo wamevaa barakoa? wana covid19? kuna watu wanalazimisha na kulaumu serikali itangaze kuwa Tanzania kuna watu mili300 wana corona ndipo akili zao zifurahie, wakiambiwa ni wazima bado hawaridhiki, subirini simba na yanga muone kama kuna watu wana vaa barakoa, baada ya one week fanyeni tathimini kaya kwa kaya muone kama kuna maambukizi na watu wangapi wamekufa, by the way matangazo ya corona Jamiiforums yalifikia wapi?
 
Kwahiyo Serikali ya Tanzania 🇹🇿 inafanya maamuzi kwa kufuata mkumbo?
Kama mwendazake hakukiri sidhani kma SSH atakiri..... Siasa zetu ni unafiki tu kutafuta popularity hakuna anayeweza kusimamia ukweli.

Hata huyu Gwajima akipewa uwaziri atakua wa kwanza kusimamia chanjo kugawiwa
 
Mbunge wa Jimbo la Kawe, Askofu Josephat Gwajima ametaka kuwepo umakini wa kuchagua Chanjo dhidi ya Ugonjwa wa COVID-19. Amesema hayo akiwa Bungeni Dodoma leo wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Afya iliyowasilishwa na Waziri Dorothy Gwajima.

Amefafanua, "Mimi sipo kinyume na Chanjo za Corona wala Chanjo yoyote. Mtu asininukuu napinga Chanjo, hapana! Tanzania tulishachanjwa Chanjo ya Kifua Kikuu, Surua, Kifaduro na Polio".

Amesema ni kweli Tanzania ikikataa Chanjo inaweza kuwekewa zuio la kwenda Ulaya. Ameeleza, "Tunakabiliwa na uchaguzi mbaya sana, tuchanjwe kitu tusichokijua sawa sawa au tusichanjwe tuzuiwe kwenda Ulaya".

Ameiomba Wizara ya Afya kuangalia suala la Chanjo kwa umakini, akisema waangalie madhara ya sasa, ya siku zijazo na ya Taifa. Ameongeza kuwa, tatizo lililopo ni kufikiri kila kinachotoka Ulaya kinafaa.

Amesema, "Before we venture into what kind of vaccine we should take, tunatakiwa tuwe na wataalamu wetu wa hapa".
Kuna watu wa asikilize na kuikubali anachokisema huyu bwana....!? Si ndiye huyu huyu aliyekemea Corona akidai haitafika Tanzania
Gwajiboy kaongea point.
Ushauri wake ufanyiwe kazi
Hatutakiwi kuchukulia issue ya chanjo kama fashion lazima tujiridhishe na hii issue iwe ni hiyari ya mtu, isiwe lazima
Hivi kweli mtu ambaye hajui mambo anayoyaongea kuna watu wa amuamini na kumpigia makogi. Nimeshangaa mpaka waziri wa Afya na Naibu wake wanagonga Meza... This is shocking.

Rashid kwenye mchango wake anaonekana hajui vitu vingi
mRNA anaiita mRA,
CDC anaiita Center of Disease and Prevention and Control,
FDA anaiita Flag and Drug Authority
Hajui maana ya Generic name
Halafu huyo Edward Flaming anayemsema ndiye nani, mbona hatujamsikia popote,

Sasa mtu kama huyu ambaye hajui basic things atawezaje kusimama na kutoa ushauri. Yaani maneno ya mtaa I anayapeleka bungeni kuyaoa kama ushauri kwa serikali.

Kama nchi yetu ina wataalamu wa kuweka kuzianalyse hizo chanjo na kujua ipi ni bora kwa nini watengenezaji washindwe.....!!
 
Kwanza tukubaliane homa ya manjano pia chanjo yake ina side effects nyingi na nimekueleza kwa takwimu za WHO watu zaidi ya laki 5 wamekufa kwa chanjo-related cases!! Kwahyo nachohoji kwanini hampigi marufuku na ile? Au ni double standard

2. China wametengeneza chanjo yao na juzi tu hapa WHO wameipa endorsement kuwa ipo effective. Kwanini sisi hatutengenezi yetu tumekalia kulaumu wazungu na chanjo zao? Mbona Russia au China hawalii lii juu ya mabeberu conceding chanjo?

3. Side effects zipo kwa dawa na cjanjo zote duniani hakuna dawa hata moja haina side effects kutokana na variation kwa hali za miili ya watu. So sio chanjo ya covid tu ndio yenye madhara..... Ndio maana nimetoa mfano wa Radiotherapy pale ocean road ile tiba ukiitumia inakumaliza kabisa baadhi ya viungo lakini haipigwi marufuku coz hakuna namna nyingine ila humu huwezi sikia mkijadili mnaaminishwa ni chanjo tu yenye side effects ila ARVs cjui Yellow fever vaccine na Radiotherapy aaah ni sawa tu!!
Huwezi kujustify kuua eti kisa kuna namna nyingine ya kuua huko nyuma tuliyoikubali.. noo..
 
Uko sahihi. Viongozi wa juu kule WHO wako 21. Wote 21 wana elimu ya PhD ya magonjwa haya. Wanne (4) ni Waafrika. Wawili (2) ni Marekani na Carribean weusi. Kuna huyo mama wa Kihindi na mama mwingine wa kiarabu wa Saudia. Watu hao ni wasomi, na wengi ni wenzetu. Elimu halisi ya Gwajima ni Form IV. Anamcheka mwenziye Makonda, lakini hana ground ya kumcheka. Kusema tuache kusikiliza wataalamu unaowasema eti twende na Gwajima.....! Yule Rais aliyetangulia ameharibu akili za watu. Amewaambia wakatae elimu, warudi walivyokuwa babu zao, na watu wanamfuata hadi sasa. Zindukeni!
Naona mzee unaongea kwa hisia, ebu jaribu kuhoji kwa kutumia akili.. hatupaswi kuwategemea wasomi hata kufikiri.. unajuaje kama wamenunuliwa
 
Nchi gani imelazimisha chanjo zake zinunuliwe? Mbona Russia na China wametengeneza za kwao na WHO imewapa endorsement?

Okay unasema vifo laki 5 kwa miaka 70 ni halali ila vifo 50 kati ya watu million zaidi ya 30 waliochanjwa kwa Astra Zeneca ndio sample nzuri ya kudiscredit chanjo?

Kingine chanjo sio tiba na hapa ndio mnakosea.... Chanjo ni kama condom tu inazuia maambukizi ila yakipenya haiwezi kukuokoa tena!! Hata ARVs kuna watu wanatumia na bado wanakufa kwa maradhi ya VVU so its not a big deal to be honest

Chanjo zote za Corona zilizopo sokoni zina side effects ambayo haikuonekana wakati zinafanyiwa majaribio. Kitu ambacho kingeweza kuonekana kama wataalamu wangepewa muda wa kufanya utafiti na kuelewa jinsi mdudu wa Corona anavyojibadili. Sasa kwanini na sisi tusijipe huo muda kuona ni kinga gani inaweza kuwa salama kwetu kutokana na mazingira yetu na variant gani iliopo hapa. Tanzania ina vijana wengi ambao ni asymptomatic na wanakinga tayari mwilini ya vitamini D na C ambazo wanaweza kupambana na mdudu huyo bila hata wao kujuwa.

Unasema chanjo sio tiba, sawa, lakini chanjo hizo za Corona ziko tofauti kutokana na zinaingia mwilini kwako zikiwa na mdudu live wa Corona na zingine zikiwa na DNA ya mdudu wa Corona. Dhumuni ni kufundisha kinga ya mwili wako ikikutanda na mdudu wa Corona mwili unakumbuka na kuanza kupambana na huyo mdudu. Sasa kama unamatatizo mengine ikiwa pamoja na weak immune system huo mfumo unakuwa hatari kwako, sana bila utafiti utakuwa nani yuko salama nani hayuko salama?
 
Acha kupotosha watu aliyekudanganya Kenya na Rwanda wamepata shida na chanjo ni nani. Mmemponza ndugu yenu mpaka corona imemla kichwa
Labda hujasoma vizuri na kuelewa. Wakati wanapokea chanjo hizo na kuanza kuzitumia, nchi zingine zilikuwa zinasitishwa kutokana na hitilafu zilizojitokeza kwenye hizo chanjo ambazo wao walizipokea.
 
Huku mtaani kwetu sijui tutamvika nani maana kwa hiari ni ngumuuuu

Tena wanakuambia kabisa mbona tangu mwaka jana tunafanya kazi zetu kariakoo, tandika, ilala na hakuna mfanyabiashara aliyeumwa hiyo corona

Kamvika mtu ambaye ameshajihakikishia corona haiambukizwi kwa kutovaa barakoa uwe na sababu atakazoelewa
Kwani nyungu imefikia wapi ndugu zangu??
 
Huwezi kuwa na hoja katika eneo usilokuwa na ujuzi nalo. Kwamba wewe umeona hoja ya "microbaolojia na virusi" tokea kwa Gwajima asiyekuwa na mbele wala nyuma kwenye eneo hili? Wewe una akili au matope?

Haya si ndiyo mambo ya nyungu?

Kwenye masuala hayo, tunawasikiliza hawa:

"Akizungumza na Mwananchi, Mtaalamu wa maicobaolojia na virusi kutoka Chuo kikuu cha Muhimbili (Muhas), Dk Joel Manyahi alisema aina hiyo ya kirusi kina tabia ya kujibadilisha mara kwa mara."

Wenye bahati zao.

Kina Gwajima hata kama wakikaa kimya tu, kwenye masuala haya hawana tofauti na kina msukuma au hata wale very illitrates vijijini ambao hawakwenda shule kabisa.
Soma vizuri wewe lofa,huyo gwajima amesema hicho kirusi hakina tabia ya kujibadiliasha mara kwa mara!?.
 
Mkuu ww hujawahi kuamini Covid 19 ipo..... Nili conclude kwamba utaamini siku Ikimpata ndugu yako wa karibu akafia mikononi mwako ICU bila kupewa chance ya kumuaga ndio utakiri kuwa it's real.
Hilo unaongea wewe hata mimi sijawahi kutamka wazi wala kiishara kuonesha kuwa siamini corona, tatizo ni kwamba kuna mambo mengi yenye utata kwenye corona sasa inapotokea wengine kuhoji au kupinga ndipo tunaonekana hatuamini kuwepo corona.
Kwahiyo tatizo hasa si kuwa corona ipo au haipo bali haya yanayohusishwa na corona ndipo kwenye utata.

Wewe umejiamulia kuamini mambo kama yalivyo hujataka kuwaza nje ya box kama navyokujua kwenye masuala kama ya dini, hoja yako unafuata wataalamu ndio maana nikapendekeza usome hicho kitabu na si kwamba hicho kitabu kinasema hakuna corona.
 
Rais usisikilize vilaza wanauunga mkono chanjo chukua ushauri wa Gwanjima.
 
Huyu bwana askofu wa kanisa la ufufuo na uzima ajue katukosea sana kwa kutofanya juhudi yoyote ya kumfufua mwendazake, hali akidai karama hiyo anayo.

Ana nini bado cha kutuambia sisi kuhusiana na Corona au lolote jingine huyu?
Nenda kachanjwe Kama amekukosea
 
Tz au Afrika mashariki ni lini tumewai tengeneza chanjo, kati ya chanjo tunazopata kila siku ? WATU Kama GWAJIMA ni wapotoshaji tu wanafikili kila kitu ni Siasa,CDC inakwambia tiyari chanjo bora ipo ( ( mRNA ) WATU wanaleta mchezo kwenye Maisha ya WATU,serikali nyie tuletee sie tudunge achana na wakina GWAJIMA ,wanaoamini kwamba tz tuna centre iliyojuu technology,vifaa,na wataalam Kama CDC wakati daily mwakimbilia kenya kwa magonjwa yakawaida hata covid yenyewe mwakimbilia huko mkipata, chanjo ya nyungu ilishafeli,
 
Tz au Afrika mashariki ni lini tumewai tengeneza chanjo, kati ya chanjo tunazopata kila siku ? WATU Kama GWAJIMA ni wapotoshaji tu wanafikili kila kitu ni Siasa,CDC inakwambia tiyari chanjo bora ipo ( ( mRNA ) WATU wanaleta mchezo kwenye Maisha ya WATU,serikali nyie tuletee sie tudunge achana na wakina GWAJIMA ,wanaoamini kwamba tz tuna centre iliyojuu technology,vifaa,na wataalam Kama CDC wakati daily mwakimbilia kenya kwa magonjwa yakawaida hata covid yenyewe mwakimbilia huko mkipata, chanjo ya nyungu ilishafeli,
It's easier to fool people than to convince them that they have been fooled.
 
Rais usisikilize vilaza wanauunga mkono chanjo chukua ushauri wa Gwanjima.
GWAJIMA ajikite kwenye Mambo yaliyondani ya UWEZO wake Sio kujifanya anaijua kila kitu huku akipotosha kisa kajikunja google kasoma publication tuwili au to tatu alafu anafika bungeni na kuanza Mambo yake kwanza ajue pia Sio site utapata information zilizo sawa up to date kila siku kila mwezi kuhusu chanjo hizi
 
Huyu bwana askofu wa kanisa la ufufuo na uzima ajue katukosea sana kwa kutofanya juhudi yoyote ya kumfufua mwendazake, hali akidai karama hiyo anayo.

Ana nini bado cha kutuambia sisi kuhusiana na Corona au lolote jingine huyu?
Bwege limeshindwa kumfufua mwendazake linatuzengua tu....

Majitu kama haya yalipaswa kumsindikiza mwendazake huko aliko
 
Back
Top Bottom