#COVID19 Askofu Gwajima: Ni ujinga kuruhusu Taifa zima kuwa 'Experiment' kwa sababu tuna haraka ya Corona

#COVID19 Askofu Gwajima: Ni ujinga kuruhusu Taifa zima kuwa 'Experiment' kwa sababu tuna haraka ya Corona

Hivi Corona ipo au haipo kwa upande wa Tanzania?

Sasa hivi tunashuhudia chanjo! Wakati mwanzo Tanzania ilisema inafanya tafiti!

Majibu ya hiyo tafiti bado tu? Au kuna mengine nyuma ya pazia!

Na kama tafiti bado, kwanini Tanzania ikimbilie kwenye chanjo.

Kama Corona ipo siitangazwe tujue moja!

Kuliko kuficha ficha huku Watanzania wengi wakiendelea kupukutika.
Mbona wewe hujapukutika?
 
Gwajima awaachie kabisa kuingilia virologist epidimiologists watafiti na madaktari kazi zao aongelee mambo ya kiroho tu tena kwa kondoo wake.

Watu wapewe uhuru wanaotaka chanjo wachanjwe
wasiotaka waachwe.

Hizo conspiracies theories against Corona disease hazina mashiko.

Kuna Spanish Flu iliuwa watu 50 to 100 million ni virus wakati idadi ya watu duniani 1.8 billion miaka ya 1910 na muingiliano haukuwa mkubwa je hicho kirusi kilitengenezwa pia.

Watz tuache porojo Corona its real and kill instantly.
Dunia nzima mpaka majirani zetu wamefika mbali kwenye program za chanjo.

Vile vile kuna chanjo za Urusi
China US UK na nchi nyingine bado ziko ktk process nchi zote hizo separately zina agenda mbaya kwa man kind.

Hakuna kitu kibaya kama brainwashing au indoctrination watu wanaingiza siasa na porojo against professionalism.

Kibaya zaidi huyu virus anamutate ambayo ni hatari sana tuangalie good progress uko UK na US ambako kuna idadi kubwa ya vaccinated people death rate zimeshuka sana.
 
Jamaa amebaki kuwa a real member of parliament,
Kule Amerika wameshachanjwa zaidi ya 100,000,000. India wameshachanjwa karibia 160,000,000. Ulaya wamechanjwa kwa mamilioni vilevile. Sasa hivi karibu kila mtu, yaani taifa zima, kule Israel amechanjwa. Hao ni wajinga au Gwajima ndiye mjinga kwa kutojua anachoongea? Elimu ya covid na vaccine ni mbali mno na upeo wa akina Gwajima. Wawe na unyenyekevu wa kutambua hilo na kunyamaza
 
Namshukuru Mungu amenipa mibaraka mingi nikiwa hapa hapa, ima iwe ni ushamba, lkn iwe iwavyo, sichanjwi na simshauli mwingine aige Imani yangu!!

Nilichotaka kusema, Gwajima ametahadharisha kuhusu kamati iliyopewa kufanya utafiti wa hizi dawa na Corona, niliyemu quote alimshambulia Kwamba, mbona Chanjo za magonjwa mengine mengi tuluchanjwa, na Kwa nini sasa iwe ni kuhoji kuhusu ubora wa dawa hizi ilihali hatuna uwezo wa kujitengenezea?

Nikasema, mambo hubadirika, na hatuwezi kuishi kama tupo nyuma ya miaka Elfu iliyopita
Kma yanabadilika ina maana madhara ya Yellow card na Radiotherapy ama ARVs yatakoma ghafla?

Uzito mlioupa chanjo ya Covid ndio uzito huo huo utumike kupinga uwe wa CT scan pale muhimbili, mpinge ultra sound, mpinge ARVs na chanjo ya yellow card. Otherwise inakua ni kazi sifuri maana kma beberu ana nia ya kukumaliza si anatumia yellow card ambayo bila hiyo huruhusiwi kusafiri popote hta kenya tu hapo!!
 
Hapana. Tatizo ni kuwa Watanzania hatusomi! Tumebaki kulalamika kuwa hatuijui chanjo. Watu wote hadi Rais aliyetangulia mnasema hamjui! Data za majaribio ya chanjo zote zilikuwa zinatolewa mwaka mzima mwaka jana, na ripoti zote za phase ya mwisho ya majaribio, Phase 3 zilielezwa vizuri sana na kuchambuliwa na wataalamu huru kuanzia Desemba 2021. Sasa tuko Phase 4 ya monitoring, halafu asiyesoma anasema tusubiri wataalamu wetu waseme. Sijui hawa wataalamu watarudi Phase ya kwanza? Watu huko duniani wanatikisa vichwa tu jinsi tulivyoachwa maili maelfu. Jebu someni New England Journal of Medicine moate hizo ripoti za Pfizer, Moderna, Astrozeneca na J&J. Sisi wengine sasa hivi tunamalizia kusoma za Urusi, China, India (nazo zinatumika), na Soberana ya Cuba.
Unajua limitation walizosema kuhusu hayo majaribio?
 
Wataalamu wetu wafanye utafiti na kuja na chanjo otherwise tunaenda kugeuzwa soko tu.
Na hii ndio lengo hasa , Magufuli alichomolewa kwa sababu alikuwa anawaamsha wengi Afrika na dunia ,wakaona isiwe tabu ,ila kupitia korona tunarudishwa nyuma sana badala ya kufanya maendeleo ,unatumua fedha unazokopeshwa kujitibu
 
Kwanza tukubaliane homa ya manjano pia chanjo yake ina side effects nyingi na nimekueleza kwa takwimu za WHO watu zaidi ya laki 5 wamekufa kwa chanjo-related cases!! Kwahyo nachohoji kwanini hampigi marufuku na ile? Au ni double standard

2. China wametengeneza chanjo yao na juzi tu hapa WHO wameipa endorsement kuwa ipo effective. Kwanini sisi hatutengenezi yetu tumekalia kulaumu wazungu na chanjo zao? Mbona Russia au China hawalii lii juu ya mabeberu conceding chanjo?

3. Side effects zipo kwa dawa na cjanjo zote duniani hakuna dawa hata moja haina side effects kutokana na variation kwa hali za miili ya watu. So sio chanjo ya covid tu ndio yenye madhara..... Ndio maana nimetoa mfano wa Radiotherapy pale ocean road ile tiba ukiitumia inakumaliza kabisa baadhi ya viungo lakini haipigwi marufuku coz hakuna namna nyingine ila humu huwezi sikia mkijadili mnaaminishwa ni chanjo tu yenye side effects ila ARVs cjui Yellow fever vaccine na Radiotherapy aaah ni sawa tu!!
Watu laki 5 kwa miaka 70 (tokea chanjo ya YF ianze kutumika) na diniani in watu billioni 7, unajikuta vifo vya homa ya majano kidogo sana. Sasa unaweza kukadiria kama chanjo ya Corona inaweza kuuwa watu wangapi katika miaka 70 ijayo? Jibu ni gumu kwasababu hatujuwi madhara ambayo hizi chanjo za dharula yatazilita kwenye miaka ya usoni.

Kuna watu wamesha ambukizwa Corona na wengine kufa kwa Corona na huku wakuwa na chanjo zote mbili lakini takwimu hizo hazitolewe na WTO wala makampuni yanyotengenza hizo chanjo kwa kuofia kuvurukika kwa biashara yao na pia kutowatia hofu watu ambao bado haja chanjwa.

Sawa dawa na tabibu zote zina madhara yake (side affects), kakini hizo tiba hazikutegenezwa leo na kuuzwa kesho. Tunaonglea si chini ya miaka kumi kwa dawa kuwa salama kwa matumizi ya mwanadamu.

Na swala la mwisho kwanini nchi zinazo tengeneza hizo dawa wanalazimisha kwa nguvu nchi masikini wanunuwe chanjo zao na ukikataa wanakuwekea vikwazo vya uchumi?
 

CDC wanaendelea kusaka data na bado hawana data zenye uhakika kwa ngazi ya jamii.bado data ni za clinical trials.
Hapa tutajiuliza ni nini lengo la kukimbilia?

Katika hii study inaonesha jamii ya watu weusi waliopatiwa chanjo hiyo ya majaribio walikuwa wachache.
Pia waliojaribiwa wengi ni vikongwe miaka 65 na zaidi.

Swali??Umri wa mtanzania kufariki ni ngapi?je chanjo hii itaenda kkujibu tatizo lipi kwa sasa?
 
Naomba Mbowe aitwe bungeni ili aeleze faida ya hiyo chanjo. Nasikia alichanjwa huko majuu .
 
Ni upumbavu kuziba tundu la panya kwa mkate..

Kama hatutaki chanjo kutoka nchi za magharibi kama nchi tutatengeneza chanjo zetu au vipi na je kuna juhudi zimefanywa kusupport hilo kama walivyokua wanapamba zile Juice za NIMR?
 
Amesema, "Before we venture into what kind of vaccine we should take, tunatakiwa tuwe na wataalamu wetu wa hapa".
Kama wapo si wangekuwa wametengeneza chanjo, si rahisi kukosoa kazi ya mtu ambaye hujui amefikiaje mafanikio vinginevyo nawe uwe na ujuzi wa kufanya mbadala wake,

Hamis Kingwangwala ni mtaalamu wa afya lakini amekwenda kununuliwa na walewale tunaoamini ni chanzo cha tatizo lililopo, je utahesabu kuwa una mtaalamu wan dani hapo?
 
Hivi Corona ipo au haipo kwa upande wa Tanzania?

Sasa hivi tunashuhudia chanjo! Wakati mwanzo Tanzania ilisema inafanya tafiti!

Majibu ya hiyo tafiti bado tu? Au kuna mengine nyuma ya pazia!

Na kama tafiti bado, kwanini Tanzania ikimbilie kwenye chanjo.

Kama Corona ipo siitangazwe tujue moja!

Kuliko kuficha ficha huku Watanzania wengi wakiendelea kupukutika.
Tuanza na kenya,Uganda, Rwanda, wezentu wameishapata chanjo vipi ni madhara yapi wamepata mpaka mda huu, alafu why tunaogopa Sana chanjo ya c 19 ali Hali hepatitis vaccine tunadungwa kila siku ,Busara itumike chanjo zije anaetaka achanje asietaka Basi,
 
Kwakweli niko tayari kutokwenda hiyo ulaya wanayosema.
 
Back
Top Bottom