Askofu Gwajima: Tanzania inashindwa kuendelea mbele kutokana na kutokuwa na muendelezo wa utawala mmoja kwenda mwingine

Hatuna "sustainable development" yaani maendeleo endelevu...
 
Aliogopa kutaja umuhimu wa katiba mpya kwani hizo njozi zikiwekwa kwenye katiba hapatakuwa na mtu mwenye akili timamu (sio kama hayati JPM ama Ndugai) wa kuzipindisha.
 
Tusubiri alidai kawe haikustahili kua pale alipoikuta
 
Tunahitaji Katiba mpya na taasisi imara zenye kufunya mambo kwa muendelezo, tusitegemee mtu mmoja kuwa na muendelezo wa mambo ya kimaendeleo.
 
Kila Rais alieingia madarakani aliperfom vizuri sana kwa namna yake lakini namna hizi zao kama kila Mtu ana namna yake unategemea Nchi itaendeleaje kwasababu kila Mtu ana namna yake na namna ya mmoja ni kinyume ya namna ya aliyetoka tutaendaje?


Hiii inanipelekea kusema Ili tuendelee tunahitaji ajenda ya pamoja ya Taifa lote kwa namna gani sasa, tudefine maono ya Tanzania ya miaka 30 au 50, tuwe na vitu ambavyo sisi Watanzania tutaviita maendeleo sio lazima vitu hivyo viitwe maendeleo.


Marekani kwa mfano ujenzi wa maghorofa si maendeleo kwetu, tunaweza kusema maendeleo kwetu kila Mtanzania awe na maji salama na safi, tunaweza kusema maendeleo kwetu kila Mtanzania mwenye uwezo wa kusoma shule asome Chuo Kikuu na amalize asiwepo wa kutokusoma Chuo Kikuu, tunaweza kusema maendeleo kwetu sisi Wafanyabiashara wafanye biashara vizuri tuwe tunaexport.....Askofu Josephat Gwajima, Mbunge wa Jimbo la Kawe

Tusipofanya hivi tuna hatari kwasababu katiba yetu inampa nafasi kila Rais anayeingia madarakani kwa namna yake kwa hekma yake na kwa namna anavyotafsiri yeye maendeleo na siku moja tutakapopata Rais ambaye hayuko sawasawa tutaishia kulia, ni ombi langu tuwe na maono ya miaka 50 halafu anapoingia Rais lazima ilani ya Chama chake izungumze mambo ambayo sisi tumejiwekea kama maono ya Tanzania.

Mfano patakapotokea Rais akaanza kufanya mambo yake kuna Mtu wa kumuuliza hapa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Amiri Jeshi Mkuu kwamba hutakiwi kufanya haya lakini tutakapokuwa na vision ambayo imewekwa kwamba tunahitaji kufikia mambo kadhaa wa kadhaa na kila regime inapoingia iwe ya kijani au blue utatimiza yale ambayo sisi tumejiwekea kama maendeleo kwetu na maono ya Taifa letu.... Josephat Gwajima


Binafsi yangu naona hii hoja ni muhimu sana isipuuzwe.
 
Huo ukweli hajauongea kutoka moyoni.
Anataka muendelezo wa mambo ya Jiwe tu.
 
Kila zama na kitabu chake
 
Gwajifix anafikiri wabongo wote ni kama waumini wake!
 
Awamu ya kwanza ndio ilikua awamu ya viwanda,viwanda vilikua chini/mali ya umma.Hivi kuna kiwanda kimeanzishwa na serikali kwenye awamu ya tano au zilikua nyimbo tu.
 
tatizo kubwa now ni waziri mkuu KASSIM MAJALIWA,ampishe Mama awe huru na uongozi wake kwa AMANI.
 
tatizo kubwa now ni waziri mkuu KASSIM MAJALIWA,ampishe Mama awe huru na uongozi wake kwa AMANI.
 
HAWA WOTE WANARUDIA TU..!! na muunganiko huo uliisha kabisa kwenye serikali ya awamu ya 5... Ukifikia hatua ya kuwaona watangulizi wako wanawashwawashwa kila wanapoongea, maana yake unaona wewe ndo unayefanya vya maana... KIKO WAPI LEO?
 
Moja ya mchango bora kabisa ktk bunge hili...

Absolutely, YES. Nakubaliana na Rev. Gwajima 100%...

Namshangaa tu kidogo Rev. Gwajima ni kwanini hajatamka kuwa ili hayo yafanyike, kunahitajika kufanyika review Mpya ya mkataba kati ya watawala na watawaliwa yaani KUREKEBISHA au KUANDIKA KATIBA MPYA KABISA...

Ni kwa sababu tatizo analolisema Rev Gwajima, mzizi wake uko ktk Katiba ya mwaka 1977. Bila kutoka hapo, hatutakwenda popote...
 
Hii bandani ya Bagamoyo mbona mnatumia nguvu kubwa sana kuonyesha kama bila hiyo bandari basi nchi haitakuwepo? Watu wavivu siku zote hudhani watu wengine watakuja kuwaendeleza. Inakuwaje mnashabikia nchi kuuza kipande chake? Hamjui usalama wa nchi utakuwa mashakani kwa kukabidhi ufunguo wa mlango kwa wageni?
 
Ni kweli kabisa
 
Ni kutokana na kutokuwa na katiba imara. Rais akiwa madarakani anakuwa na nguvu nyingi zinazopelekea hata watangulizi wake wanapingwa waziwazi waliyoyafanya.

Kibaya zaidi huyo Rais huyo akiwa madarakani kwa katiba hii anafurahi kweli na kufanya anavyotaka na hayupo tayari kuibadilisha ambapo anakuja kujuta baadae.

Wanasahau kuwa moyo wa mtu ni kichaka, atajoonesha vizuri sana kuwa loyal kwako laini akishapata anachokitaka na akawa top utaona rangi zote.

Mifano ipo mingi mfano JK VS JPM, KABILA VS TSHEKED n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…