Askofu Gwajima: Tanzania inashindwa kuendelea mbele kutokana na kutokuwa na muendelezo wa utawala mmoja kwenda mwingine

Askofu Gwajima: Tanzania inashindwa kuendelea mbele kutokana na kutokuwa na muendelezo wa utawala mmoja kwenda mwingine

Mbunge wa Jimbo la Kawe Josephat Gwajima akitoa mchango kuhusu hotuba iliyotolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema nchi nyingi za Kiafrika zimekuwa haziendelei kwa kasi ya maendeleo kutokana na kushindwa kutumia rasimali kwani inaendana na 'manpower'

Pia ameeleza kuwa Tanzania inashindwa kuendelea mbele kwa kasi kwasababu hakuna muendelezo wa Regime moja kwenda nyingine ambapo kila Rais anaingia madarakani na mipango yake hivyo huathiri maendeleo ya ukuaji wa mipango iliyoanzishwa.

Gwajima amtolea mfano Nyerere alietawala miaka 20 na kuacha viwanda 411, alipokuja Mwinyi aliboresha baadhi ya mambo lakini hakuendelea na wazo la viwanda na alipoingia Mkapa akauza vyote kwa kuvibinafsisha hivyo kukosa muunganiko kati ya 'regime' ya kwanza na regime ya tatu.

Gwajima amesema watakesha kama hamna huo muunganiko kwani hata Rais wa awamu ya nne hakushughulika na viwanda, bali mambo mengine lakini awamu ya tano akaamua kushughulika na viwanda, vilevile ambavyo awamu ya tatu ilivibinafsisha na kuviuza.

Gwajima amesema ni hatari kwasababu katiba inampa nafasi kila Rais anayeingia madarakani kwa namna yake, hekima yake na kwa namna anavyotafasiri yeye maendeleo.

Amesema siku moja atakapopatikana Rais ambaye hayuko sawasawa watu wataishia kulia na kutoa ombi la kuwa na vision ya kuwa na miaka 50 ya Taifa na anapoingia Rais lazima ilani ya chama chake izungumze mambo ambayo Taifa imejiwekea kama maono.

Gwajima amehoji endapo akatokea Rais ambae anafanya mambo yake yasiyo kwenye ilani kama kuna mtu wa kumuuliza mwenyekiti wa chama cha mapinduzi na Amiri Jeshi mkuu!



Hatuna "sustainable development" yaani maendeleo endelevu...
 
Aliogopa kutaja umuhimu wa katiba mpya kwani hizo njozi zikiwekwa kwenye katiba hapatakuwa na mtu mwenye akili timamu (sio kama hayati JPM ama Ndugai) wa kuzipindisha.
 
Nimesikiliza, jamaa kaongea point kubwa tangu Bunge lianze, kila Rais anakuja na mishe zake, anaharibu mfumo uliopo anaanza upya, mfano jiwe kaja kafumua fumua kila kitu , mfumo wa Elimu kafumua , mfumo wa biashara kaufmua ,mfumo wa utumishi kaharibu haribu huko na kabla hata hajaseti mambo akafa ....yaan mnarudi nyuma maili buku...Kwa kweli tunatakiwa tuwe na maono ya kimkakati aisee, kuwe na long run plan na short run plan, wakat wa uchaguz kila chama mbali na agenda zao lazima waonyeshe jinsi watakavyokamilisha agenda za kimkakati , na hapa ndo umhimu wa katiba mpya .....!!

Hatuwezi kuendelea Kwa kutegemea mawazo ya mtu mmoja kuwaza anayotaka yeye yawe..... Anaharibu lililopo na hata kuvunja katiba ili atimize anayotaka yeye , aaah..

Mfano mradi wa Bandari wa Bagamoyo Kwa namna yyte Ile ni wa muhimu, Bandari ya DSM tayari ipo congested na overwhelmed..... Ni heri tujadili kwamba tutafte wapi hela ya kujenga tuachane na wahisani wenye masharti magumu , na sio kuupiga chini moja Kwa moja .....!!
Tusubiri alidai kawe haikustahili kua pale alipoikuta
 
Tunahitaji Katiba mpya na taasisi imara zenye kufunya mambo kwa muendelezo, tusitegemee mtu mmoja kuwa na muendelezo wa mambo ya kimaendeleo.
 
Kila Rais alieingia madarakani aliperfom vizuri sana kwa namna yake lakini namna hizi zao kama kila Mtu ana namna yake unategemea Nchi itaendeleaje kwasababu kila Mtu ana namna yake na namna ya mmoja ni kinyume ya namna ya aliyetoka tutaendaje?


Hiii inanipelekea kusema Ili tuendelee tunahitaji ajenda ya pamoja ya Taifa lote kwa namna gani sasa, tudefine maono ya Tanzania ya miaka 30 au 50, tuwe na vitu ambavyo sisi Watanzania tutaviita maendeleo sio lazima vitu hivyo viitwe maendeleo.


Marekani kwa mfano ujenzi wa maghorofa si maendeleo kwetu, tunaweza kusema maendeleo kwetu kila Mtanzania awe na maji salama na safi, tunaweza kusema maendeleo kwetu kila Mtanzania mwenye uwezo wa kusoma shule asome Chuo Kikuu na amalize asiwepo wa kutokusoma Chuo Kikuu, tunaweza kusema maendeleo kwetu sisi Wafanyabiashara wafanye biashara vizuri tuwe tunaexport.....Askofu Josephat Gwajima, Mbunge wa Jimbo la Kawe

Tusipofanya hivi tuna hatari kwasababu katiba yetu inampa nafasi kila Rais anayeingia madarakani kwa namna yake kwa hekma yake na kwa namna anavyotafsiri yeye maendeleo na siku moja tutakapopata Rais ambaye hayuko sawasawa tutaishia kulia, ni ombi langu tuwe na maono ya miaka 50 halafu anapoingia Rais lazima ilani ya Chama chake izungumze mambo ambayo sisi tumejiwekea kama maono ya Tanzania.

Mfano patakapotokea Rais akaanza kufanya mambo yake kuna Mtu wa kumuuliza hapa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Amiri Jeshi Mkuu kwamba hutakiwi kufanya haya lakini tutakapokuwa na vision ambayo imewekwa kwamba tunahitaji kufikia mambo kadhaa wa kadhaa na kila regime inapoingia iwe ya kijani au blue utatimiza yale ambayo sisi tumejiwekea kama maendeleo kwetu na maono ya Taifa letu.... Josephat Gwajima


Binafsi yangu naona hii hoja ni muhimu sana isipuuzwe.
 
Huo ukweli hajauongea kutoka moyoni.
Anataka muendelezo wa mambo ya Jiwe tu.
Mimi huwa simkubali huyu jamaa lakini katika hili kaongea ukweli kabisa na hilo ndio tatizo letu. Tuchukulie mfano Dubai wao waliweka malengo wanataka kuwa number one kwa kila kitu hawataki number 2 kwa kila wanalofanya, kama ndege, airport, utalii na sijui bandari na mengi tu lakini sio kwamba ndio wamekuwa number one kwa kila kitu lakini hayo ndio malengo yao na kila mtu apiganie hayo. Sasa sisi kama Tanzania ni lazima tujiwekee vision je lipi tutakaloweza kututoa hapa na kutupeleka pale. Kama tunataka tuwe number one kwa kilimo Africa, tunataka tuwe nchi yenye elimu bora, afya bora na hii mifano tu basi iwe ni ilani ya kila chama iwe sharti mengine ya nyongeza kuboresha sawa tu lakini washindane sera za kutufikisha katika vision yetu. Naunga mkono hoja
 
Kila zama na kitabu chake
Du Wanapata shida sana na kifo cha mtukufu wanataka vyote alivyotaka mtukufu viendelezwe hata kama havina tija. Yeye mtukufu alivunja vunja vyote vya watangulizi wake na kuanza vyake ambavyo vilikuwa wala havufuati mpango wa taifa wa maendeleo wala CCM wala alichotaka kupeleka nchi nako hakujulikani. Rais wa sasa atafuataje kwenda kulingamiza Taifa la hasha nchi hii ni ya wote.
 
Gwajifix anafikiri wabongo wote ni kama waumini wake!
9we

Well said my friend!!!

Gwajima Josephat kaongea vyema kabisaaa, lakini given kwamba hoja yake ina lengo fulani lililojificha chini ya carpet kwa muda/kipindi hiki hiyo hoja yake hebu ikae pembeni tumuache Mh. Rais Samia Suluhu Hassan afanye yale anayoyaona yeye yanafaa kulifanyia Taifa kama walivyofanya watangulizi wake. Namuomba sana Gwajima aache kum-pre empty Rais wetu Samia.

Rais mstaafu Ally Hassan Mwinyi kipindi kileee alivyokwenda kumpongeza Hayati JPM kwa kazi nzuri anayoifanya alisema tumpe support JPM kwa yale anayoyafanya kwasababu kila zama na kitabu chake. Kwahiyo tumuache nae Rais Samia aandike kitabu chake kama walivyofanya watangulizi wake, tusimuingilie tafadhalini sana!!!

Halafu naomba nimkumbushe Gwajima Josephat kwamba kuwa na moja kitaifa ni wazo zuri lakini inategemeana na nyakati na majira pia. Kwa mfano, Kabla ya Mwl. Nyerere kugatuka mamlakani tulikuwa na mfumo wa chama kimoja lakini hali ikaja kubadilika na kuingia kwenye vyama vingi kutokana na nyakati.

Pia wakati wa Mwl. Nyerere tulikuwa na Public Enterprises lakini hiyo sera ikaja kubadilika kutokana na nyakati, tulikuwa na sera ya vijiji vya ujamaa lakkni ikaja kubadilika kutokana na nyakati.

Mwisho, hebu tumwache mama yetu Samia Suluhu Hassana tuone anatupeleka wapi kama tulivyowaacha watangulizi wake ukizingatia kuwa yeye amesema kipindi chake hiki ni awamu ya SITA.

Asante!
 
Awamu ya kwanza ndio ilikua awamu ya viwanda,viwanda vilikua chini/mali ya umma.Hivi kuna kiwanda kimeanzishwa na serikali kwenye awamu ya tano au zilikua nyimbo tu.
 
tatizo kubwa now ni waziri mkuu KASSIM MAJALIWA,ampishe Mama awe huru na uongozi wake kwa AMANI.
 
tatizo kubwa now ni waziri mkuu KASSIM MAJALIWA,ampishe Mama awe huru na uongozi wake kwa AMANI.
 
Kati ya michango Bora katika Bunge letu hili, ni huu, na bila Shaka tumechelewa Sana sababu ya kukosa miunganiko kutoka utawala A Hadi B n.k

Tukiweza hili, tutaondokana na mipango na vision ya mtu mmoja anayeitwa Kwa cheyo cha Raisi na badala yake itakuwa, maoni na mawazo ya wengi ndio yanaongoza nchi
HAWA WOTE WANARUDIA TU..!! na muunganiko huo uliisha kabisa kwenye serikali ya awamu ya 5... Ukifikia hatua ya kuwaona watangulizi wako wanawashwawashwa kila wanapoongea, maana yake unaona wewe ndo unayefanya vya maana... KIKO WAPI LEO?
 
Moja ya mchango bora kabisa ktk bunge hili...

Absolutely, YES. Nakubaliana na Rev. Gwajima 100%...

Namshangaa tu kidogo Rev. Gwajima ni kwanini hajatamka kuwa ili hayo yafanyike, kunahitajika kufanyika review Mpya ya mkataba kati ya watawala na watawaliwa yaani KUREKEBISHA au KUANDIKA KATIBA MPYA KABISA...

Ni kwa sababu tatizo analolisema Rev Gwajima, mzizi wake uko ktk Katiba ya mwaka 1977. Bila kutoka hapo, hatutakwenda popote...
 
Nimesikiliza, jamaa kaongea point kubwa tangu Bunge lianze, kila Rais anakuja na mishe zake, anaharibu mfumo uliopo anaanza upya, mfano jiwe kaja kafumua fumua kila kitu , mfumo wa Elimu kafumua , mfumo wa biashara kaufmua ,mfumo wa utumishi kaharibu haribu huko na kabla hata hajaseti mambo akafa ....yaan mnarudi nyuma maili buku.

Kwa kweli tunatakiwa tuwe na maono ya kimkakati aisee, kuwe na long run plan na short run plan, wakat wa uchaguz kila chama mbali na agenda zao lazima waonyeshe jinsi watakavyokamilisha agenda za kimkakati , na hapa ndo umhimu wa katiba mpya!

Hatuwezi kuendelea Kwa kutegemea mawazo ya mtu mmoja kuwaza anayotaka yeye yawe..... Anaharibu lililopo na hata kuvunja katiba ili atimize anayotaka yeye , aaah.

Mfano mradi wa Bandari wa Bagamoyo Kwa namna yyte Ile ni wa muhimu, Bandari ya DSM tayari ipo congested na overwhelmed na pia inaelekea kuwa beyond rehabilitation. Ni heri tujadili kwamba tutafte wapi hela ya kujenga tuachane na wahisani wenye masharti magumu , na sio kuupiga chini moja Kwa moja!
Hii bandani ya Bagamoyo mbona mnatumia nguvu kubwa sana kuonyesha kama bila hiyo bandari basi nchi haitakuwepo? Watu wavivu siku zote hudhani watu wengine watakuja kuwaendeleza. Inakuwaje mnashabikia nchi kuuza kipande chake? Hamjui usalama wa nchi utakuwa mashakani kwa kukabidhi ufunguo wa mlango kwa wageni?
 
Mbunge wa Jimbo la Kawe Josephat Gwajima akitoa mchango kuhusu hotuba iliyotolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema nchi nyingi za Kiafrika zimekuwa haziendelea kwa kasi ya maendeleo kutokana na kushindwa kutumia rasimali kwani inaendana na 'manpower'.

Pia ameeleza kuwa Tanzania inashindwa kuendelea mbele kwa kasi kwasababu hakuna muendelezo wa Regime moja kwenda nyingine ambapo kila Rais anaingia madarakani na mipango yake hivyo huathiri maendeleo ya ukuaji wa mipango iliyoanzishwa.

Gwajima amtolea mfano Nyerere alietawala miaka 20 na kuacha viwanda 411, alipokuja Mwinyi aliboresha baadhi ya mambo lakini hakuendelea na wazo la viwanda na alipoingia Mkapa akauza vyote kwa kuvibinafsisha hivyo kukosa muunganiko kati ya 'regime' ya kwanza na regime ya tatu.

Gwajima amesema watakesha kama hamna huo muunganiko kwani hata Rais wa awamu ya nne hakushughulika na viwanda, bali mambo mengine lakini awamu ya tano akaamua kushughulika na viwanda, vilevile ambavyo awamu ya tatu ilivibinafsisha na kuviuza.

Gwajima amesema ni hatari kwasababu katiba inampa nafasi kila Rais anayeingia madarakani kwa namna yake, hekima yake na kwa namna anavyotafasiri yeye maendeleo.

Amesema siku moja atakapopatikana Rais ambaye hayuko sawasawa watu wataishia kulia na kutoa ombi la kuwa na vision ya kuwa na miaka 50 ya Taifa na anapoingia Rais lazima ilani ya chama chake izungumze mambo ambayo Taifa imejiwekea kama maono.

Gwajima amehoji endapo akatokea Rais ambae anafanya mambo yake yasiyo kwenye ilani kama kuna mtu wa kumuuliza mwenyekiti wa chama cha mapinduzi na Amiri Jeshi mkuu!



Ni kweli kabisa
 
Ni kutokana na kutokuwa na katiba imara. Rais akiwa madarakani anakuwa na nguvu nyingi zinazopelekea hata watangulizi wake wanapingwa waziwazi waliyoyafanya.

Kibaya zaidi huyo Rais huyo akiwa madarakani kwa katiba hii anafurahi kweli na kufanya anavyotaka na hayupo tayari kuibadilisha ambapo anakuja kujuta baadae.

Wanasahau kuwa moyo wa mtu ni kichaka, atajoonesha vizuri sana kuwa loyal kwako laini akishapata anachokitaka na akawa top utaona rangi zote.

Mifano ipo mingi mfano JK VS JPM, KABILA VS TSHEKED n.k
 
Back
Top Bottom