Kuna upuuzi mwingi humu unasemwa - eti system ikitaka kukuua au kukufanya chochote haiwezi kushindwa!! Ni ujinga na uwendawazimi wa hali ya juu. Hivi system ni nini? Nani anaumda hiyo system?
Watu wanapoongelea system, wanaongelea TISS. TISS ni chombo cha Serikali, kija upungufu wa weledi, uzembe, na makosa mengi kama vilivyo vyombo vingi vya Serikali. Kwa nchi yetu taasisi za Serikali ndizo zinazoongoza kwa uzembe, upungufu wa ujuzi na weledi. Serikali yetu haijawahi kuwa na ufanisi wa jambo lolote. Kwenye biashara ilishindwa, kwenye utawala wa sheria imeshindwa, kwenye sera nzuri za uchumi imeshindwa, kwenye kutengeneza ajira imeshindwa, kwenye ujenzi wa uchumi imeshindwa, halafu ikawe na weledi wa hali ya juu huko TISS pekee?
Hawa watu wa TISS tunao mitaani mwetu, uwezo wao mdogo kimafunzo, kielimu na kiakili tunaufahamu. Ndiyo hao unasema wakitaka jambo, hawawezi kushindwa?