Askofu jimbo la Mbinga: Amani ni tunda la haki

Askofu jimbo la Mbinga: Amani ni tunda la haki

Elice Elly

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
1,267
Reaction score
1,593
Mahubiri ya Askofu John Ndimbo (Kingenzu) katika Misa ya Christmas amesisitiza kuwa bila kutenda haki hakuna Amani.Amesema haki ya watu kuchagua viongozi wao,haki ya kuishi pia amesieistiza msamaha wa kweli.

Lakini amesema yeyoye anayempenda Mungu anawajali binadamu wenzake. Amesema pale mtu mmoja anapojitutumua na kujifanya kuwa karibu na Mungu anasababisha mazingira magumu kwa wengine. Amesema hata kama mtu huyo ni Mkubwa wetu anapaswa kujishusha.

Askofu Ndimbo amesema kila mmoja anapaswa kupalilia Amani toka moyoni mwake.amesema jukumu la kuleta Amani si la mtu mmoja pekee,awe Rais au Askofu,Bali la kila mmoja.

Amesisitiza kuwa itunzwe na Hatimaye ikue mpaka kimataifa.Amesema lazima tuhakikishe kuwa haki inatendeka kwa wanasiasa wote na RAIA wote.

Chanzo: TBC.
 
Ni kichaa tu ndiyo hufikiria kuwa amani ni tunda la ukatili na uovu kwa wanadamu wenzako
 
Tatizo hawa hawa viongozi wa dini wana wajua wavurugaji wa hii amani lakini wana wapa viti vya mbele kanisani na kuwa nafasi ya kusimama madhabahuni na kumdanganya Mungu. Zaidi wana wapa hata sakramenti takatifu wakati wana jua pasi na shaka hawa watu sio wasafi. Kemeeni kwa vitendo
Amani NI tunda la haki. Well said Shepherd. May this message pierce onto Magufuli's wicked soul

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo hawa hawa viongozi wa dini wana wajua wavurugaji wa hii amani lakini wana wapa viti vya mbele kanisani na kuwa nafasi ya kusimama madhabahuni na kumdanganya Mungu. Zaidi wana wapa hata sakramenti takatifu wakati wana jua pasi na shaka hawa watu sio wasafi. Kemeeni kwa vitendo
Hawawezi kuwatenga wazi wazi lakini atleast wanaweza kuwaonya kwa maovu yao.Baba Askofu ananirudishia amani
 
Presenter alishindwa kuzima japo akasingizia mitambo?? Najua hiyo misa haiwezi kufanyika.marudio leo jioni
Muunganiko wa mahibiri ulivyokuwa ilikuwa ni ngumu kuzima ,ni kama mahubiri yote Ujumbe ulikuwa ni huo.Labda naona baadaye ni ngumu kurudia Misa, wakirudia watakata mahubiri manake hakutumia lugha ya mkato ilikuwa ni lugha ya moja kwa moja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom