LGE2024 Askofu Juda Ruwa'ichi atoa tamko kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Kanisa Takatifu la Mitume libarikiwe kwa kusema ukweli kuwasemea wananchi ambao ni Watanzania na waumini wao.
 
Ulikuwa naye hapo jijini, na unaelewa alivyo kubalika hapo, labda uwe ulikuwa bado hujazaliwa.

Wewe unayo matatizo, hili siyo swala la kuwa 'chawa' pekee. Kuna jambo haliko sawa unapo furahia waTanzania wenzako kuondlewa uhai, kwa sababu tu wanao fanya hivyo ni kundi lako.
Ujenzi wa cathedral ya kawekamo mwanza ulimfanya ahamishwe, sasa hivi cathedral inajengwa kwa kasi ya kutisha, sasa sijui alikuwa anafanyafanya nini mpaka Vatican ikaamua kumuondoa ghafla
 
Wewe uliweka tafsiri potofu kuhusu uhamisho huo.
 
Hakika haya mambo mwisho mbaya. Unatawala kwa nguvu watu wenye akili bila ridhaa yao hata Mungu anawaona anajua ukweli ni upi na uongo ni upi.
 
Kama Serikali haitaingilia kati na kuwashughulikia Hawa viongozi uchwara wa dini nchi itaingia kwenye machafuko muda sio mrefu. Huko Rwanda hawa Maaskofu wa Kikatoliki walihusika sana kwenye kuchochea na kisabisha Genocide. Serikali iwe makini!!!
Bila shaka Wewe ndio "mtoto wa shule" uliyeandikishwa na ccm kwenye huu uchaguzi. Maamayo .
 
Anza kumpuuza baba yako mzazi....
viongozi wa dini wanapoacha kuhubiri neno la Mungu na kuanza kuhubiri siasa za chuki na migawanyiko kama huyu ruwaichi na kitima, ni wa kupuuzwa tu gentleman,

wala haina haja kubabaika nao kabisa 🐒
 
Kwani hapa wataikosa? Kama ccm wanakaa madarakani kwa support ya vyombo vya dola unategemea hao maaskofu wakose support ya wananchi hapa kwetu?
Tupo, 2025 inakuja tuombe uhai......hii ni Tanzania,,,,....kiroho hii nchi ni tofauti sana na hayo mataifa mengine , tupo hapa
 
chadema inateswa na pepo muhemko na mkurupuko inatakiwa mafuta ya alizeti ya upako ili ipone mpasuko 🐒
Siku tukipata uhuru nchi hii ccm tutawakimbiza nchi hii, hamtoamini.
Mtakufa kwa maelfu, na mtalia na kusaga meno.
 
Wakuu,

Askofu Mkuu Jimbo la Dar na Mwenyekiti wa Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu Tanzania, Juda Thadeus Ruwa'ichi anatoa tamko sasa hivi kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa, Katika mkutano na Wanahabari unafanyika kwenye viunga vya 'Parokia ya Bikira Maria Mama wa Huruma Mji mpya Relini.

Askofu Ruwa'ichi ametaja baadhi ya mauaji ya wanasiasa na raia yaliyotokea hivi karibuni kuwa ni pamoja na yale yaliyotokea Novemba 26, 2024 huko Tunduma mkoani Songwe na Manyoni mkoani Singida sambamba na mauaji yaliyotokea jijini Dar es Salaam Novemba 27 mwaka huu, ambayo Kanisa hilo limetaja mauaji hayo yote kuwa ni ya kukusudia

"Mwanzoni mwa mwezi huu (Novemba 2024) kule Iringa na Bukoba waliuawa pia wanasiasa wawili (2), Tanzania tunaelekea wapi kwa kujenga tabia hii?, kitendo cha mauaji ya wanasiasa kinapaswa kulaaniwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria, hakuna mwenye mamlaka ya kumuuwa mwenzake, kutekeleza ama kudai haki za kisiasa wakati wa uchaguzi wakati wa uchaguzi sio vita ni ushindani"

Aidha, Kanisa Katoliki limesema tabia ya kuchukulia mauaji ya wanasiasa na raia kama vifo vya kawaida na vinavyopaswa kuzoeleka ni tendo baya sana linaloweza kupelekea kujengeka tabia ya kupoteza na kukosa ulinzi wa haki ya uhai kama ilivyo kwenye Ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

"Wapo waliokabidhiwa jukumu la kulinda Ibara hii, tunapoona mauaji haya yakiongezeka tunajiuliza maswali mengi juu ya uwajibikaji wa serikali kwa wananchi"

Kuhusu mweendo wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa liofanyika Novemba 27

"Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana maeneo mbalimbali ya nchi yetu inaonekana kwamba uchaguzi wa Serikali za Mitaa umegubikwa na mapungufu mengi, ambayo wengi ninyi kama wanahabari mnayajua. Shughuli zito kama hii ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa inapoenda kiholela hatuipendi nchi yetu, hatuwatendei raia haki na hatushughulikii raia wote".

"Viongozi mbalimbali wa dini walitoa matamko kuhusu mwenendo wa maandalizi kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, matamko yale yalikuwa ni tahadhali tufanye hilo zoezi kwa hali inayokidhi. Ni zoezi (niliite takatifu) katika nchi yoyote, Uchaguzi halali na haki ni zoezi takatifu la kiraia, kwahiyo ni lazima lifanywe kwa uzito, uangalifu na uadilifu unaotakiwa"

"Nchi yetu ni ya Siasa ya vyama vingi, hata kama tunaweza kuelekea kuwa na ulemavu wakujihisi kwamba ni nchi ya chama kimoja lakini Tanzania ni nchi ya Vyama vingini na raia Mtanzania kuwa mshiriki wa chama chochote hiyo ni haki yake kiraia hakuna raia yoyote ambaye amezaliwa nakufungamanishwa na CCM, CHADEMA au CUF na vingine, hivyo vyama vyote ni machaguo au maamuzi ya raia mwenyewe na raia anapoamua kwamba anataka kujihusisha anapaswa kuheshimiwa. Watanzania tuendelee kujenga utayari wakuithamini nchi yetu, kuipigania nchi yetu na kupendana, kushikamana na kutendeana haki"

Tumetamka mara kadhaa kwamba inabidi tujipange, tujipange kutazama nyanja mbalimbali zinazohitaji maboresho au marekebisho katika mwenendo wa siasa za nchi yetu, hilo sio haki ya Wanasiasa ni haki ya raia wote kuwa na mpangilio na mwelekeo wa kisiasa ambao unatendea haki na unalinda usitawi na unapania maendeleo ya nchi yetu. Mtu yeyote mwenye nia njema na nchi yetu hawezi acha kulipigia kelele hili na yeyote anayeona tamko kama hili linawameng'enya ni vizuri wakajitadhimini.

Hana lolote,Hawa Huwa wanapinga Kiongozi akiwa sio wa kutoka kwao so ni WA kupuuzwa.

Pili kuhusu matukio yaliyotokea ni Changamoto za kawaida za uchaguzi lakini asilimia kubwa uchaguzi umefanyika vizuri na Kwa Haki.

Mifano Wilaya niliko Chadema wanayoishabikia imeshinda viti 5 ,Huko CCM ingeshinda wangesema wameibiwa.

Upuuzi tuu
 
  • Nzuri
Reactions: UCD
Kama Serikali haitaingilia kati na kuwashughulikia Hawa viongozi uchwara wa dini nchi itaingia kwenye machafuko muda sio mrefu. Huko Rwanda hawa Maaskofu wa Kikatoliki walihusika sana kwenye kuchochea na kisabisha Genocide. Serikali iwe makini!!!
Unadhani hao maaskofu wa Katoliki ni sawa na askofu Gwajima au askofu Kakobe? Hao wana nguvu kuliko wanasiasa unaowajua.
 
Wakuu,

Askofu Mkuu Jimbo la Dar na Mwenyekiti wa Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu Tanzania, Juda Thadeus Ruwa'ichi anatoa tamko sasa hivi kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa, Katika mkutano na Wanahabari unafanyika kwenye viunga vya 'Parokia ya Bikira Maria Mama wa Huruma Mji mpya Relini.

Askofu Ruwa'ichi ametaja baadhi ya mauaji ya wanasiasa na raia yaliyotokea hivi karibuni kuwa ni pamoja na yale yaliyotokea Novemba 26, 2024 huko Tunduma mkoani Songwe na Manyoni mkoani Singida sambamba na mauaji yaliyotokea jijini Dar es Salaam Novemba 27 mwaka huu, ambayo Kanisa hilo limetaja mauaji hayo yote kuwa ni ya kukusudia

"Mwanzoni mwa mwezi huu (Novemba 2024) kule Iringa na Bukoba waliuawa pia wanasiasa wawili (2), Tanzania tunaelekea wapi kwa kujenga tabia hii?, kitendo cha mauaji ya wanasiasa kinapaswa kulaaniwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria, hakuna mwenye mamlaka ya kumuuwa mwenzake, kutekeleza ama kudai haki za kisiasa wakati wa uchaguzi wakati wa uchaguzi sio vita ni ushindani"

Aidha, Kanisa Katoliki limesema tabia ya kuchukulia mauaji ya wanasiasa na raia kama vifo vya kawaida na vinavyopaswa kuzoeleka ni tendo baya sana linaloweza kupelekea kujengeka tabia ya kupoteza na kukosa ulinzi wa haki ya uhai kama ilivyo kwenye Ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

"Wapo waliokabidhiwa jukumu la kulinda Ibara hii, tunapoona mauaji haya yakiongezeka tunajiuliza maswali mengi juu ya uwajibikaji wa serikali kwa wananchi"

Kuhusu mweendo wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa liofanyika Novemba 27

"Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana maeneo mbalimbali ya nchi yetu inaonekana kwamba uchaguzi wa Serikali za Mitaa umegubikwa na mapungufu mengi, ambayo wengi ninyi kama wanahabari mnayajua. Shughuli zito kama hii ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa inapoenda kiholela hatuipendi nchi yetu, hatuwatendei raia haki na hatushughulikii raia wote".

"Viongozi mbalimbali wa dini walitoa matamko kuhusu mwenendo wa maandalizi kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, matamko yale yalikuwa ni tahadhali tufanye hilo zoezi kwa hali inayokidhi. Ni zoezi (niliite takatifu) katika nchi yoyote, Uchaguzi halali na haki ni zoezi takatifu la kiraia, kwahiyo ni lazima lifanywe kwa uzito, uangalifu na uadilifu unaotakiwa"

"Nchi yetu ni ya Siasa ya vyama vingi, hata kama tunaweza kuelekea kuwa na ulemavu wakujihisi kwamba ni nchi ya chama kimoja lakini Tanzania ni nchi ya Vyama vingini na raia Mtanzania kuwa mshiriki wa chama chochote hiyo ni haki yake kiraia hakuna raia yoyote ambaye amezaliwa nakufungamanishwa na CCM, CHADEMA au CUF na vingine, hivyo vyama vyote ni machaguo au maamuzi ya raia mwenyewe na raia anapoamua kwamba anataka kujihusisha anapaswa kuheshimiwa. Watanzania tuendelee kujenga utayari wakuithamini nchi yetu, kuipigania nchi yetu na kupendana, kushikamana na kutendeana haki"

Tumetamka mara kadhaa kwamba inabidi tujipange, tujipange kutazama nyanja mbalimbali zinazohitaji maboresho au marekebisho katika mwenendo wa siasa za nchi yetu, hilo sio haki ya Wanasiasa ni haki ya raia wote kuwa na mpangilio na mwelekeo wa kisiasa ambao unatendea haki na unalinda usitawi na unapania maendeleo ya nchi yetu. Mtu yeyote mwenye nia njema na nchi yetu hawezi acha kulipigia kelele hili na yeyote anayeona tamko kama hili linawameng'enya ni vizuri wakajitadhimini.

Huyu Askofu hastahili heshima yoyote kwa yale aliyofanya Mwanza akiwa Askofu wa Jimbo hasa Bugando mpaka akasababisha Sister wa watu akajiua. Mimi simkubali kabisa ndio maana ha UCardinary akaukosa!! 🤣🤣
 
Unadhani hao maaskofu wa Katoliki ni sawa na askofu Gwajima au askofu Kakobe? Hao wana nguvu kuliko wanasiasa unaowajua.
Hakuna lolote usifikiri waumini wa RC tunafuata mkumbo wa Askofu tunajitambua!
 
Back
Top Bottom