Askofu Kalikawe Bagonza: Tujiulize zaidi, CHADEMA wamejitoa au wametolewa?

Askofu Kalikawe Bagonza: Tujiulize zaidi, CHADEMA wamejitoa au wametolewa?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
Ameandika Baba Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza

*TUJIULIZE ZAIDI*

1. Hivi CHADEMA wamejitoa au wametolewa?

2. Hivi CHADEMA wamesusa au wamesuswa?

3. Hivi CHADEMA wameacha au wameachwa?

Wasomaji msinihukumu bila kunisikiliza. Maswali haya ni ya msingi kwangu.

- Media haiko na wapinzani
-Msajili hayuko na wapinzani
-Mahakama haiko na wapinzani
-Vyombo vya dola haviko na wapinzani
-Viongozi wa dini hawako na wapinzani
-Asasi za Kiraia haziko na wapinzani
-Bunge haliko na wapinzani
-Tume ya Uchaguzi haiko na wapinzani
-Wazee mashuhuri hawako na wapinzani
-Wana taaluma hawako na wapinzani
-Wasimamizi wa chaguzi hawako na wapinzani
-Walinzi wa amani hawako na wapinzani
-Waajiri hawako na wapinzani
-Mashirika yasiyo ya kiserikali hayako na wapinzani
-Wapinzani hawako na wapinzani.
-Hata mimi siko nao, naandika kujipendekeza kwao!

Hii inaitwa unyanyapaa (stigmatization) Kwa hiyo walichokifanya, kwa maoni yangu:

Hawakujitoa, wametolewa
Hawakususa, wamesuswa
Hawakuacha, wameachwa

Kimya cha makundi yote hapo, tafsiri yake ni kuwasusa, kuwaacha, kuwatoa katika mchakato wa kidemokrasia, na kupuuza madai yao. Walio wengi, wanaona ni salama ama kukaa kimya au kuwalaumu na kuwakejeli.

Watu, kundi au mtu aliye katika hali hii ya kuachwa, ni hatari kwa jamii, ni hatari kwa nafsi yake mwenyewe na mara nyingi hujikinai.

Baba wa Taifa aliwahi kusema,

"Amani ni tunda la haki. Palipo na amani kuna haki na palipo na haki kuna amani. Tanzania tuna amani lakini haina maana kuwa haki inatendeka. Kinachotokea ni kuwa, watu wana matumaini kuwa haki itatendeka siku moja. Watu hawa siku wakikata tamaa kuwa haipo, yatatokea maafa makubwa sana. Viongozi wana jukumu la kuhakikisha matumaini ya watu kupata haki hayapotei".

Dumisha Uhuru na Umoja,
Wake kwa waume na watoto,
_Mungu Ibariki Tanzania._
 
.
Ngoja waje praise team kama hawajakwambia uyo ni mamluki sio mtazania........!!!!!
IMG-20191106-WA0045.jpeg
 
Nikama Timu za mpira wa bongo,wanasajili wachezaji kwa gharama kubwa,makocha then wananunua referees na wachezaji wa timu pinzani ili washinde,sasa umewekeza vizuri kila kitu why uwe muoga kushindana uwanjani?
 
Sijawahi kuwaonea huruma chadema, ni watu wajinga kuliko ujinga wenyewe! Nafurah sana napoona chadema inakanyagwa kisawasawa
Demokrasia ni maridhiano na kuheshimiana Si ugomvi,mpira wa miguu kama refa anapendelea upande mmoja lazima upande mwingine ulalamike,nimekuwa nikichunguza siasa za miaka hii zimejaa chuki,enzi za miaka fulani bila kujali siasa watu walikuwa wanashirikiana,ila saizi mitaani ukionekana ni chama fulani,wa upande mwingine wanakuwa mbali nawewe.

Political tolerance ni muhimu kama Taifa,siyo lugha kama hizi
 
Back
Top Bottom