Askofu Kalikawe Bagonza: Tujiulize zaidi, CHADEMA wamejitoa au wametolewa?

Askofu Kalikawe Bagonza: Tujiulize zaidi, CHADEMA wamejitoa au wametolewa?

Ameandika Baba Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza

*TUJIULIZE ZAIDI*

1. Hivi CHADEMA wamejitoa au wametolewa?

2. Hivi CHADEMA wamesusa au wamesuswa?

3. Hivi CHADEMA wameacha au wameachwa?

Wasomaji msinihukumu bila kunisikiliza. Maswali haya ni ya msingi kwangu.

- Media haiko na wapinzani
-Msajili hayuko na wapinzani
-Mahakama haiko na wapinzani
-Vyombo vya dola haviko na wapinzani
-Viongozi wa dini hawako na wapinzani
-Asasi za Kiraia haziko na wapinzani
-Bunge haliko na wapinzani
-Tume ya Uchaguzi haiko na wapinzani
-Wazee mashuhuri hawako na wapinzani
-Wana taaluma hawako na wapinzani
-Wasimamizi wa chaguzi hawako na wapinzani
-Walinzi wa amani hawako na wapinzani
-Waajiri hawako na wapinzani
-Mashirika yasiyo ya kiserikali hayako na wapinzani
-Wapinzani hawako na wapinzani.
-Hata mimi siko nao, naandika kujipendekeza kwao!

Hii inaitwa unyanyapaa (stigmatization) Kwa hiyo walichokifanya, kwa maoni yangu:

Hawakujitoa, wametolewa
Hawakususa, wamesuswa
Hawakuacha, wameachwa

Kimya cha makundi yote hapo, tafsiri yake ni kuwasusa, kuwaacha, kuwatoa katika mchakato wa kidemokrasia, na kupuuza madai yao. Walio wengi, wanaona ni salama ama kukaa kimya au kuwalaumu na kuwakejeli.

Watu, kundi au mtu aliye katika hali hii ya kuachwa, ni hatari kwa jamii, ni hatari kwa nafsi yake mwenyewe na mara nyingi hujikinai.

Baba wa Taifa aliwahi kusema,

"Amani ni tunda la haki. Palipo na amani kuna haki na palipo na haki kuna amani. Tanzania tuna amani lakini haina maana kuwa haki inatendeka. Kinachotokea ni kuwa, watu wana matumaini kuwa haki itatendeka siku moja. Watu hawa siku wakikata tamaa kuwa haipo, yatatokea maafa makubwa sana. Viongozi wana jukumu la kuhakikisha matumaini ya watu kupata haki hayapotei".

Dumisha Uhuru na Umoja,
Wake kwa waume na watoto,
_Mungu Ibariki Tanzania._
Ili changes ya kweli itokee anatakiwa atokee mtu mmko achomoe betri
 
Angalau kunawanao chambua haya maswala.
 
Mimi sioni kama humu nchini kuna amani,
Labda mioyo ya woga ndo inaashiria amani ipo
 
Unaelewa faida ya kuwepo kwa upinzani kama wa Chadema au unaongea tu uridhishe nafsi yako?

Sijawahi kuwaonea huruma chadema, ni watu wajinga kuliko ujinga wenyewe! Nafurah sana napoona chadema inakanyagwa kisawasawa
 
Unataka ushindani lakini hutaki kushindana, wakati huo huo unatuaminisha kuwa tunashindana! Basi shindana mwenyewe!
Nani anataka kwenda kukalia debe ? Tunataka kula ugali wetu na maharage siku ziende.
 
"Amani ni tunda la haki. Palipo na amani kuna haki na palipo na haki kuna amani. Tanzania tuna amani lakini haina maana kuwa haki inatendeka. Kinachotokea ni kuwa, watu wana matumaini kuwa haki itatendeka siku moja. Watu hawa siku wakikata tamaa kuwa haipo, yatatokea maafa makubwa sana. Viongozi wana jukumu la kuhakikisha matumaini ya watu kupata haki hayapotei".
Aliyoyasema baba wa taifa yatabakia kuwa kweli. Inasikitisha awamu hii chama kile kile alichoasisi mwalimu kinaona amani ni tunda la ubabe.
 
Ndo m
Nikama Timu za mpira wa bongo,wanasajili wachezaji kwa gharama kubwa,makocha then wananunua referees na wachezaji wa timu pinzani ili washinde,sasa umewekeza vizuri kila kitu why uwe muoga kushindana uwanjani?
Ndo mambo ya kamati za ufundi hayo, jamaa wanaamini hata ukiwa physically fit bado unaweza kutunguliwa tu kwa ujanja ujanja mwingine usio na maelezo yoyote, ni shida sana aisee..
 
Back
Top Bottom