Askofu Kalikawe Bagonza: Tujiulize zaidi, CHADEMA wamejitoa au wametolewa?

Askofu Kalikawe Bagonza: Tujiulize zaidi, CHADEMA wamejitoa au wametolewa?

Tangu chadema wabadilishe gia hewani 2015 mimi siko na wapinzani kabsa
 
Naunga mkono hoja,kipindi cha JK walitetemesha nchi wao ndio wao na hawakuitumia nafasi vizuri walikua na chance kubwa mno. Huwezi kumtupa dr slaa kisa lowassa. Ukatibu mkuu huwezi kumtupa lissu na wenzie machachari kisa masinji sijui mashinji
Sijawahi kuwaonea huruma chadema, ni watu wajinga kuliko ujinga wenyewe! Nafurah sana napoona chadema inakanyagwa kisawasawa
 
CCM ndio waliokabidhiwa nchi na mabeberu, hakuna wa kuwatoa...

Ninyi wengine mlionewa tu huruma, mkapigwa changa la macho la siasa za vyama vingi...
 
Na hamu ya kutoa maoni sema sasa imekuwa taabu humu ukisema umtete meko unaitwa kijana wa Lumumba, ukisema utetee DJ unaitwa kijana wa ufipa yani kila upande wanataka kusikia maneno matatmu kuhusu wao sio machungu

Swali fikilishi tu je kususia uchaguzi ndo suruhisho?

Kusema hawawatambua wenge viti watakaochanguliwa ndio suruhisho?

Mara ngapi wamesema hawawatambui viongozi waliochangulia lakini baadae wanawaunga mkono mfano mzuri meko walikataa mtambua ila sasa hali ipoje bado hawamtambui au?

Ngoja nisikilize remix ya diamond ft magufuri baba lao😀😀😀
 
Ameandika Baba AskofuKalikawe Lwakalinda Bagonza

*TUJIULIZE ZAIDI*

1. Hivi CHADEMA wamejitoa au wametolewa?

2. Hivi CHADEMA wamesusa au wamesuswa?

3. Hivi CHADEMA wameacha au wameachwa?

Wasomaji msinihukumu bila kunisikiliza. Maswali haya ni ya msingi kwangu.

- Media haiko na wapinzani
-Msajili hayuko na wapinzani
-Mahakama haiko na wapinzani
-Vyombo vya dola haviko na wapinzani
-Viongozi wa dini hawako na wapinzani
-Asasi za Kiraia haziko na wapinzani
-Bunge haliko na wapinzani
-Tume ya Uchaguzi haiko na wapinzani
-Wazee mashuhuri hawako na wapinzani
-Wana taaluma hawako na wapinzani
-Wasimamizi wa chaguzi hawako na wapinzani
-Walinzi wa amani hawako na wapinzani
-Waajiri hawako na wapinzani
-Mashirika yasiyo ya kiserikali hayako na wapinzani
-Wapinzani hawako na wapinzani.
-Hata mimi siko nao, naandika kujipendekeza kwao!

Hii inaitwa unyanyapaa (stigmatization) Kwa hiyo walichokifanya, kwa maoni yangu:

Hawakujitoa, wametolewa
Hawakususa, wamesuswa
Hawakuacha, wameachwa

Kimya cha makundi yote hapo, tafsiri yake ni kuwasusa, kuwaacha, kuwatoa katika mchakato wa kidemokrasia, na kupuuza madai yao. Walio wengi, wanaona ni salama ama kukaa kimya au kuwalaumu na kuwakejeli.

Watu, kundi au mtu aliye katika hali hii ya kuachwa, ni hatari kwa jamii, ni hatari kwa nafsi yake mwenyewe na mara nyingi hujikinai.

*Baba wa Taifa aliwahi kusema,*

"Amani ni tunda la haki. Palipo na amani kuna haki na palipo na haki kuna amani. Tanzania tuna amani lakini haina maana kuwa haki inatendeka. Kinachotokea ni kuwa, watu wana matumaini kuwa haki itatendeka siku moja. Watu hawa siku wakikata tamaa kuwa haipo, yatatokea maafa makubwa sana. Viongozi wana jukumu la kuhakikisha matumaini ya watu kupata haki hayapotei".

Dumisha Uhuru na Umoja,
Wake kwa waume na watoto,
_Mungu Ibariki Tanzania._
Hapo penye mashirika yasiyo ya serikali ameongopa Sana ukweli hayo mashirika yamekua yakienda kinyume Sana na serikali hii, !!!

Lakini changamoto wanazo kutana nazo chadema zimekuwa ni hizo hizo , kwa sasa Anaye paswa kuongelea ni yule aliye na solutions za kukabiliana na hili na si KUBAINISHA changamoto

Ni hayo tu
 
Ameandika Baba AskofuKalikawe Lwakalinda Bagonza
#TUJIULIZE ZAIDI
1. Hivi Chadema Wamejitoa au Wametolewa?
2. Hivi Chadema wamesusa au Wamesuswa?
3. Hivi Chadema Wameacha au Wameachwa?
Wasomaji msinihukumu bila kunisikiliza. Maswali haya ni ya msingi kwangu.
- Media haiko na wapinzani
-Msajiri hayuko na wapinzani
-Mahakama haiko na wapinzani
-Vyombo vya dola haviko na wapinzani
-Viongozi wa dini hawako na wapinzani
-Asasi za kiraia haziko na wapinzani
-Bunge haliko na wapinzani
-Tume ya uchaguzi haiko na wapinzani
-Wazee mashuhuri hawako na wapinzani
-Wana taaluma hawako na wapinzani
-Wasimamizi wa chaguzi hawako na wapinzani
-Walinzi wa amani hawako na wapinzani
-Waajiri hawako na wapinzani
-Mashirika yasiyo ya kiserikali hayako na wapinzani
-Wapinzani hawako na wapinzani.
-Hata mimi siko nao, naandika kujipendekeza kwao!
Hii inaitwa unyanyapaa (stigmatization). Kwa hiyo walichokifanya, kwa maoni yangu:
Hawakujitoa, wametolewa
Hawakususa, wamesuswa
Hawakuacha, wameachwa
Kimya cha makundi yote hapo, tafsiri yake ni kuwasusa, kuwaacha, kuwatoa katika mchakato wa kidemokrasia, na kupuuza madai yao. Walio wengi, wanaona ni salama ama kukaa kimya au kuwalaumu na kuwakejeli.
Watu, kundi au mtu aliye katika hali hii ya kuachwa, ni hatari kwa jamii, ni hatari kwa nafsi yake mwenyewe na mara nyingi hujikinai.
Baba wa Taifa aliwahi kusema,
"Amani ni tunda la haki. Palipo na amani kuna haki na palipo na haki kuna amani. Tanzania tuna amani lakini haina maana kuwa haki inatendeka. Kinachotokea ni kuwa, watu wana matumaini kuwa haki itatendeka siku moja. Watu hawa siku wakikata tamaa kuwa haipo, yatatokea maafa makubwa sana. Viongozi wana jukumu la kuhakikisha matumaini ya watu kupata haki hayapotei".
Dumisha Uhuru na Umoja,
Wake kwa waume na watoto,
Mungu Ibariki Tanzania.
 
Hivi wewe askofu si ndiye yule aliepewa milioni sitini na lowasa ili akanunuwe gari la kiaskofu kupitia kwa gwajima?
 
Mwambieni atengeneze jukwaa au aitishe waandishi wa habari
 
Back
Top Bottom