Askofu Kalikawe Bagonza: Tujiulize zaidi, CHADEMA wamejitoa au wametolewa?

Askofu Kalikawe Bagonza: Tujiulize zaidi, CHADEMA wamejitoa au wametolewa?

Sijawahi kuwaonea huruma chadema, ni watu wajinga kuliko ujinga wenyewe! Nafurah sana napoona chadema inakanyagwa kisawasawa

Cdm yenyewe inafurahi sana inapopata watu wanaoichukia kama ww maana hapo ndio taasisi yao inapokamilika. Uzuri hauko mwenyewe unayeichukia sana cdm, kwani hata rais ni mwenzako katika wale wanaoichukia sana cdm, na anatumia madaraka yake kudhibitisha chuki hiyo dhidi ya cdm. Ila cdm ina watu kibao wanaoikubali, inachohitaji ni haki tu na wala hawana tatizo la ww au rais kuwachukia.
 
Unaelewa faida ya kuwepo kwa upinzani kama wa Chadema au unaongea tu uridhishe nafsi yako?

JPM mwenyewe ni tunda la kuimarika ushindani wa kisiasa 2010-2015. Kutokana na umaarufu waliopata JPM kupitia wizara ya ujenzi ccm iliona ndiye mtu wa kuivusha licha ya baadhi ya wakongwe kuamini kwambà hana karama ya kiuongozi wa kisiasa! Ushindani siyo vita ya kufa na kupona na kutumia mbinu haramu. Badala yake ni vita vya maneno ya kushawishi kupendwa na kupata ufuasi.
 
Ameandika Baba Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza

*TUJIULIZE ZAIDI*

1. Hivi CHADEMA wamejitoa au wametolewa?

2. Hivi CHADEMA wamesusa au wamesuswa?

3. Hivi CHADEMA wameacha au wameachwa?

Wasomaji msinihukumu bila kunisikiliza. Maswali haya ni ya msingi kwangu.

- Media haiko na wapinzani
-Msajili hayuko na wapinzani
-Mahakama haiko na wapinzani
-Vyombo vya dola haviko na wapinzani
-Viongozi wa dini hawako na wapinzani
-Asasi za Kiraia haziko na wapinzani
-Bunge haliko na wapinzani
-Tume ya Uchaguzi haiko na wapinzani
-Wazee mashuhuri hawako na wapinzani
-Wana taaluma hawako na wapinzani
-Wasimamizi wa chaguzi hawako na wapinzani
-Walinzi wa amani hawako na wapinzani
-Waajiri hawako na wapinzani
-Mashirika yasiyo ya kiserikali hayako na wapinzani
-Wapinzani hawako na wapinzani.
-Hata mimi siko nao, naandika kujipendekeza kwao!

Hii inaitwa unyanyapaa (stigmatization) Kwa hiyo walichokifanya, kwa maoni yangu:

Hawakujitoa, wametolewa
Hawakususa, wamesuswa
Hawakuacha, wameachwa

Kimya cha makundi yote hapo, tafsiri yake ni kuwasusa, kuwaacha, kuwatoa katika mchakato wa kidemokrasia, na kupuuza madai yao. Walio wengi, wanaona ni salama ama kukaa kimya au kuwalaumu na kuwakejeli.

Watu, kundi au mtu aliye katika hali hii ya kuachwa, ni hatari kwa jamii, ni hatari kwa nafsi yake mwenyewe na mara nyingi hujikinai.

Baba wa Taifa aliwahi kusema,

"Amani ni tunda la haki. Palipo na amani kuna haki na palipo na haki kuna amani. Tanzania tuna amani lakini haina maana kuwa haki inatendeka. Kinachotokea ni kuwa, watu wana matumaini kuwa haki itatendeka siku moja. Watu hawa siku wakikata tamaa kuwa haipo, yatatokea maafa makubwa sana. Viongozi wana jukumu la kuhakikisha matumaini ya watu kupata haki hayapotei".

Dumisha Uhuru na Umoja,
Wake kwa waume na watoto,
_Mungu Ibariki Tanzania._
Mmhh hujipendi nini, shauri ya wewe. Utapotea na hatutajua umepotelea wapi. Kukaa kimya ni bora kwa awamu hii ya 5 sikivu
 
Ningeshauri serikali waitishe Referendum nyingine waulize kama wananchi wanataka vyama vingi au la? hili kuondoa sintofahamu ya chuki,ubaguzi na uonevu iwe kama BREXIT YA UINGEREZA badala ya kutumia njia hatarishi ya kufuta vyama vingi bila ridhaa ya wananchi
 
Big respect askofu wangu,"na wapinzani hawako na wapinzani".
 
Aliyoyasema baba wa taifa yatabakia kuwa kweli. Inasikitisha awamu hii chama kile kile alichoasisi mwalimu kinaona amani ni tunda la ubabe.

Mwaka 1995 wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi Mwalimu alilazimika kufanya kampeni baada ya kuona msisimko mkubwa na Hamas ya uchaguzi wa vyama vingi. Hata hivyo kwenye kampeni hiyo Mwalimu alikwenda maeneo machache tu ya nchi. Pia katika mkutano yake aliwashawishi wapiga kura kuwa mgombea urais wa ccm alikuwa bora kuliko wote! Kwenye nafasi ya Ubunge na udiwani aliwaasa wapiga kura kuchagua mgombea wa chama chochote! Ndiyo kusema hakuifanyia ccm kampeni. Huyo ndiye Mwalimu Nyerere; statesman wa ukweli. Leo hii kwenye ngazi ya mtaa, kitongoji na kijiji wananchì wameporwa haki ya kuchagua kiongozi kutoka chama kingine cha siasa isipokuwa ccm tu!
 
Sijawahi kuwaonea huruma chadema, ni watu wajinga kuliko ujinga wenyewe! Nafurah sana napoona chadema inakanyagwa kisawasawa
Chama gani unataka kiwe chama kikuu cha upinzani maana chadema kimeshajitoa? Hata akija nani atakuwa kama mavi ya chooni kwako hivyo tawala mpaka uingie kaburini tuone kama utaikuta CCM huko inakusubiri.
 
Sijawahi kuwaonea huruma chadema, ni watu wajinga kuliko ujinga wenyewe! Nafurah sana napoona chadema inakanyagwa kisawasawa
Ni kama mimi nikiona mwanaccm kafa basi amani tele inanijaa moyoni!Bunge kuwa mtoa roho,nadhani mpaka huu tungepungua sana Tz maana ningefyeka CCM wengi sana!
 
Nchi hii watu wamejawa na hofu... mkuu wa wilaya kaambiwa mpinzani akipita kazi hana...

Tanzania inapitia wakati mgumu mno. Askofu huko uliko na ufunikwe na damu ya Yesu aliye hai, . Shetani hajawahi kushinda ila hutamba kwa muda tu.
 
Sijawahi kuwaonea huruma chadema, ni watu wajinga kuliko ujinga wenyewe! Nafurah sana napoona chadema inakanyagwa kisawasawa
Wewe ni miongoni mwa wapumbavu waliokubuhu wachache sana hapa duniani, wa kariba yako mpo wawili tu na nyote tunawajua.
 
Hakuna dhehebu ambalo nimeanza kulistukia kama dhehebu langu la RC. Kipindi cha Kikwete lilikuwa halichelewi kutoa matamko kumlinda Padri Slaa kumbe sababu kuu ilikuwa udini shenzykabisa
 
Kazi ipo
Screenshot_20191106-234500.jpeg
 
Back
Top Bottom