Nimetazama usiku Upendo TV wakitangaza Askofu Malasusa akitangazwa kuwa Askofu mkuu mteule wa KKKT.
Niseme kweli ya moyo wangu, nilishangazwa sana na sura za maaskofu wengine kuonyesha kutokuwa na furaha tofauti na inavyotegemewa.
Nini sababu? Kwa sisi waumini wa Kilutheri ni vyema tuambiwe ukweli kumetokea nini huko katika mkutano mkuu?
Malasusa nakumbuka historia yaķe sio nzuri sana katika kanisa, kunakipindi baada ya kuingia Askofu Shoo alileta upingaji mambo kadhaa akawa kama ametengwa na wenzake kimyakimya.
Pia, wakati mwendazake akitenda mambo ya kikatili na uongozi usio wa kidemokrasia huyu Malasusa aliamua kuwa rafiki yake binafsi kwa mgongo wa Kanisa akiitumia Dayosisi ya mashariki na pwani.
Inaweza kuwa ni fikra zangu potofu, lakini kama kaingia madarakani kwa mbinu za dola ili kuliharibu kanisa la Mungu basi tutamuomba Mungu alirudishe mikononi mwake.