Askofu Malasusa kwanini anataka tena Uaskofu Mkuu KKKT?

Askofu Malasusa kwanini anataka tena Uaskofu Mkuu KKKT?

Nimetazama usiku Upendo TV wakitangaza Askofu Malasusa akitangazwa kuwa Askofu mkuu mteule wa KKKT.
Niseme kweli ya moyo wangu, nilishangazwa sana na sura za maaskofu wengine kuonyesha kutokuwa na furaha tofauti na inavyotegemewa.
Nini sababu? Kwa sisi waumini wa Kilutheri ni vyema tuambiwe ukweli kumetokea nini huko katika mkutano mkuu?
Malasusa nakumbuka historia yaķe sio nzuri sana katika kanisa, kunakipindi baada ya kuingia Askofu Shoo alileta upingaji mambo kadhaa akawa kama ametengwa na wenzake kimyakimya.
Pia, wakati mwendazake akitenda mambo ya kikatili na uongozi usio wa kidemokrasia huyu Malasusa aliamua kuwa rafiki yake binafsi kwa mgongo wa Kanisa akiitumia Dayosisi ya mashariki na pwani.
Inaweza kuwa ni fikra zangu potofu, lakini kama kaingia madarakani kwa mbinu za dola ili kuliharibu kanisa la Mungu basi tutamuomba Mungu alirudishe mikononi mwake.
Mungu alinisuru kanisa, Malasusa alichafuka toka siku nyingi hata alipokuwa mkuu wa KKKT mambo yalikuwa hovyo.
Kuna siku nimeswitch upendo TV nilipokutana nae tu akihubiri nikabadilisha. Malasusa yuko kisiasa zaidi kuliko kiroho na siasa ndiyo iliyomrudisha hapo.
 
Shida ya kupata madaraka ukiwa kijana ndio hii malasusa alipata madaraka akiwa na miaka 46 na kumaliza akiwa na miaka 54......

Tamaa imemjia tena.
 
Uzuri kwa katiba ya KKKT, Mkuu wa KKKT hana mamlaka yoyote au uwezo wowote wa kumwambia au kumfukuza kazi Askofu Mkuu wa Dayosisi...., Labda Malasusa aingie abadilishe katiba na kujipa Mamlaka.

Ila kwa katiba ya sasa ni hekima tuu huwa inatumika kumuheshimu ila kila mtu kwenye dayosisi lake ana nguvu zake mwenyewe kama mfalme ambazo haziingiliwi na mtu yeyote yule...(Rejea katiba ya Dayosisi ya Mashariki na Pwani na Katiba ya Dayosisi ya Kaskazini)

Hivyo hata kama ameingia kwa mgongo wa fulani ni ngumu sana kusukuma Kanisa liende kama anavyotaka yeye maana Katiba haijampa mamlaka hayo...., Yeye ataendelea kupambana na Kimaro wake ila akitoka nje ya hapo ni kibano kikali
KKKT wamebadili katiba kwenye mkutano huu,kwa sasa watakuwa na katiba moja na sio kila usharika kuwa na katiba yake.
 
Kazi ya shoo ilikua kutetea kina Mbowe sijawahi kuona akitoka nje ya hapo...

Malasusa jitahidi kuwa mtetezi wa watanzania wote.
 
Mimi nilisema toka mwanzo kwamba selikali haiwezi kuruhusu Bagonza awe mkuu wa KKKT ndio sababu ya kupita kwa Malasusa!

Hiyo ni kazi ya kitengo
Tulikuwa tunamtegemea Dr. Abednego Keshomshahara ndio awe mkuu
 
Malasusa alishamaliza two terms za uaskofu Mkuu, baada ya mabadiliko ya katiba amegombea tena uaskofu Mkuu; je ana jambo jipya kwa taasisi hii yenye watu zaidi ya milioni nane NCHINI?

Endapo atapata, hakuna uwezekano akaikabidhi taasisi hii kwenye dola kama alivyofanya DSM akiwa mjumbe wa kamati ya amani? Kwanini asikubali kustaafu? Kama katika regime yake aliweza kumpa likizo mchungaji Kimaro, nini tutegemee kwa wachungaji walokole akirejea kwenye nafasi ya juu?

Je, akina Bagonza watabaki salama ndani ya kanisa? Hakuna uwezekano akashirikiana na Askofu wa Tanga ambaye kwa urgument na perception ni mwanamfumo kulifanya kanisa liondoke kwenye malengo yake liwe na mrengo wa kutetea dola?

Hapa ndipo maombi yanahitajika zaidi kuone kesho kabla haijafika
Siku Zote kanisa linaongozwa na Roho Mt sio mtu.Ikiwa kuchaguliwa kwake kunatokana na Mungu,tusinug'unuke tusiyetukaonekana tunapingana na Mungu.(matendi ya mitume 5:38)
 
Walutheri mmewekewa pandikizi la serikali,tegemeeni kkkt kuwa submissive kwa serikali sasa,kwenye nyeusi mseme nyeupeee, unapoambiwa serikali inamkono mrefu huwa mnaelewaje? Kipindi hiki inabidi makanisa yote yaongozwe na makada kulekea uchaguzi mkuu na katiba mpya
 
Back
Top Bottom