Nani kasema hivyo? Video inataja dini tatu ambazo zinahusisha si chini ya asilimia themanini ya Watanzania wote. Kama ingekuwa udini, angetaja dini moja tu anayoipendelea. Ni dini ipi sasa hiyo unayoisema kwa kuwa zimetajwa dini tatu? Video imezitaja dini hizo tatu kwa kuashiria tu idadi ya Watanzania ambao inabidi kuwasikiliza. Msemaji akaenda mbali zaidi na kumtaja Mbowe, mwanasiasa mwenye wafuasi wengi; akamtaja Warioba, kiongozi kwenye masuala ya Katiba, msomi, mwanasheria aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo ya uwaziri mkuu; akamtaja Shivji msomi, mwanasheria, na mfuasi wa Mwalimu Nyerere; na akamtaja Slaa, aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki na Katibu Mkuu wa CHADEMA. Mifano yote hiyo ni kuonyesha tu upeo wa watu ambao inabidi kusikilizwa. Hiyo kauli ya udini inatoka wapi kama siyo wewe tu unayetaka kupoteza lengo kwa kuwaaminisha watu tofauti na mtoa mada kwenye video alivyodhamiria?