Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kadinali ndio inakuwa Nini? Majukumu gani anakuwa nayo?
HAKUNA KISICHOWEZEKANA MKUU!!Sahau hiyo
umezurura(umetembea)Huyu mtu makini sana . Nimedhurula naye sana Trinidad and Tobago
Naaam! Hatari sanaaa.Another Rugambwa in the Cardinal position.
Hongera sana kwake na kwa Kanisa Catholic Tanzania.
Huyu asiwe mdini na mwenye kupendelea mtu wa dini yake kama Yule Mzee wa ajabu ajabu kutoka RukwaView attachment 2682944
Askofu mkuu Mwandamizi Protase Rugambwa
Mhashamu Protase Rugambwa sasa Mhadhama.
Baba Mtakatifu Fransisco amemteua Askofu mkuu Mwandamizi Protase Rugambwa kuwa Kadinali. Mhashamu Protase Rugambwa ni mwandamizi wa kiti cha uaskofu Jimbo kuu Katoliki la Tabora.
Hongera sana Mhashamu Rugambwa.
Taarifa toka Vatican
Sister Angela Rwekiza
-
Pia soma >
- Je, Protase Rugambwa ndiye Kardinali ajaye Tanzania?
--
KARDINALI MTEULE RUGAMBWA NI NANI?
▪︎Askofu Mkuu Rugambwa alizaliwa tarehe 31 Mei 1960 huko Bunena-Bukoba nchini Tanzania, akapata Daraja Takatifu ya Upadri kutoka mikononi mwa Mtakatifu Yohane wa Pili alipotembelea Tanzania tarehe 2 Septemba 1990 na kuwa Padri wa Jimbo Katoliki Rulenge-Ngara.
Kuanzia mwaka 2002 hadi mwaka 2008 alifanya utume wake kwenye Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu mjini Vatican. Baba Mtakatifu Benedikto XVI, tarehe 18 Januari 2008 akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Kigoma, na tarehe 26 Juni 2012 akateuliwa kuwa Katibu Mwambata wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu na Rais wa Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari na wakati huo huo kumpandisha hadhi na kuwa ni Askofu mkuu.
Tarehe 9 Novemba 2017 Baba Mtakatifu Francisko akamteua kuwa Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu. Baada ya kulitumikia Baraza kwa vipindi viwili na muda wake ulipogota ukomo, kadiri ya Katiba mpya ya Kitume inayojulikana kama “Predicate evangelium” yaani “Hubirini Injili” Juu ya Sekretarieti kuu “Curia Romana” na Huduma Yake Kwa Kanisa na Kwa Ulimwengu”.
Tarehe 13 Aprili 2023, Baba Mtakatifu alimteua Askofu Mkuu Protase Rugambwa kuwa Askofu mkuu wenye haki ya kurithi Jimbo kuu la Tabora, Tanzania.
Hana makuu,kadinal wetu tutaendelea kuwa naye Tabora.Mabosi wawili wanakaa pamoja mmoja ataenda kua Tabora na mwingine yupo Dar
Ruwaich alikuwa jauSheria za kanisa namba moja ni utii, napokea kwa furaha na kumshukuru Mungu kwa kupata kadinali kwa mara nyingine tena hapa Tanzania ila binafsi naona kama sio sawa hivi!
Waitu kyoma Ta Rugambwa Wiukayo Tata!wije omukyalo tukue akanyetooo