Askofu Mkuu Mwandamizi Protase Rugambwa ateuliwa kuwa Kardinali

View attachment 2682944
Askofu mkuu Mwandamizi Protase Rugambwa​

Mhashamu Protase Rugambwa sasa Mhadhama.

Baba Mtakatifu Fransisco amemteua Askofu mkuu Mwandamizi Protase Rugambwa kuwa Kadinali. Mhashamu Protase Rugambwa ni mwandamizi wa kiti cha uaskofu Jimbo kuu Katoliki la Tabora.

Hongera sana Mhashamu Rugambwa.

Taarifa toka Vatican
Sister Angela Rwekiza

-
Pia soma >
- Je, Protase Rugambwa ndiye Kardinali ajaye Tanzania?

--
KARDINALI MTEULE RUGAMBWA NI NANI?

[emoji830]︎Askofu Mkuu Rugambwa alizaliwa tarehe 31 Mei 1960 huko Bunena-Bukoba nchini Tanzania, akapata Daraja Takatifu ya Upadri kutoka mikononi mwa Mtakatifu Yohane wa Pili alipotembelea Tanzania tarehe 2 Septemba 1990 na kuwa Padri wa Jimbo Katoliki Rulenge-Ngara.

Kuanzia mwaka 2002 hadi mwaka 2008 alifanya utume wake kwenye Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu mjini Vatican. Baba Mtakatifu Benedikto XVI, tarehe 18 Januari 2008 akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Kigoma, na tarehe 26 Juni 2012 akateuliwa kuwa Katibu Mwambata wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu na Rais wa Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari na wakati huo huo kumpandisha hadhi na kuwa ni Askofu mkuu.

Tarehe 9 Novemba 2017 Baba Mtakatifu Francisko akamteua kuwa Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu. Baada ya kulitumikia Baraza kwa vipindi viwili na muda wake ulipogota ukomo, kadiri ya Katiba mpya ya Kitume inayojulikana kama “Predicate evangelium” yaani “Hubirini Injili” Juu ya Sekretarieti kuu “Curia Romana” na Huduma Yake Kwa Kanisa na Kwa Ulimwengu”.

Tarehe 13 Aprili 2023, Baba Mtakatifu alimteua Askofu Mkuu Protase Rugambwa kuwa Askofu mkuu wenye haki ya kurithi Jimbo kuu la Tabora, Tanzania.
 
Wenye kanisa lenu naomba muongozo hapa huyu Laurean Rugambwa na Protasi Rugambwa si ndugu hawa?.

Kama ni ndugu inaonekana familia ya mzee Rugambwa hasa watoto wa kiume wana kitu gani cha ndani hadi waaminike wao tu?.
 
Kuna mtu nafikir hata mwez haujapita alisema kwamba huyu Protase Rugambwa atakuwa Kardinal nafikir hata mwez haujaisha
 
Yupo pia Novatus Rugambwa, ni balozi wa papa huko kwingineko duniani. Sijui ni ndugu hawa?
Wenye kanisa lenu naomba muongozo hapa huyu Laurean Rugambwa na Protasi Rugambwa si ndugu hawa?.

Kama ni ndugu inaonekana familia ya mzee Rugambwa hasa watoto wa kiume wana kitu gani cha ndani hadi waaminike wao tu?.
 
Hii ndiyo ile kusema ukikaa karibu na ua waridi, lazima unukie. Hongera nyingi kwa Muadhama Mardinali. Maana siyo kila nchi inapata bahati ya kuwa na Kardinali.

Kwa Tanzania tunastahili pongezi. Maana ni Kardinali wa 3 huyu tunapata.
 
Back
Top Bottom