PreGE2025 Askofu mkuu Ruwa'ichi: Tutende Haki Katika Uchaguzi. Tuachane na Uzalendo Uchwara

PreGE2025 Askofu mkuu Ruwa'ichi: Tutende Haki Katika Uchaguzi. Tuachane na Uzalendo Uchwara

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Tunapo azimisha Pasaka ya mwaka huu ni Pasaka ya pekee kidogo kwetu Watanzania hasa tukikumbuka kwamba huu ni mwaka ambao Watanzania watahusika katika masuala ya uchaguzi. Uchaguzi huo ambao utafanyika kwaajili ya kupata viongozi wa Taifa, wabunge na madiwani.

Kila Mkristo anapaswa kushiriki fursa hiyo akikumbuka yeye ni nani, lakini bila mazoea. Chaguzi zetu zimekuwa na historia yakuwa na uwalakini ninaomba mwaka huu chaguzi zetu ziwe bora, ziwe za haki, ziwe za ukweli na ziwe zinazozingatia maslai na manufaa ya raia wote. Tutende Haki Katika CHAGUZI – Tuachane na Uzalendo Uchwara.

Tumuombe Mungu aliyemfufua Bwana Yesu Kristo atuandalie maandalizi mazuri ya uchaguzi

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025


 
Tunapo azimisha Pasaka ya mwaka huu ni Pasaka ya pekee kidogo kwetu Watanzania hasa tukikumbuka kwamba huu ni mwaka ambao Watanzania watahusika katika masuala ya uchaguzi. Uchaguzi huo ambao utafanyika kwaajili ya kupata viongozi wa Taifa, wabunge na madiwani.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025


Uchawa ndiyo “Uzalendo Uchwara”!
 
Haki huinua Taifa na dhuluma huinua uovu na chuki miongoni mwa jamii.

Tukumbuke kuna maisha baada ya kifo ambayo hayana mwisho tena na kila mmoja atavuna sawasawa alichopanda
 
Tuache Uzalendo Uchwara , Kwa tafasiri ya kawaida Ndugu zangu, UZALENDO UCHWARA ni aina ya Uzalendo ambao watu mbele ya Vyombo vya habari hujifanya Wema, wanaipenda nchi , wanapenda haki, kumbe nyuma Yao Wana Matendo yalojaa Dhuluma, uonevu, Ufisadi, Upendeleo, Utafunaji wa Nchi na Mali zake, Ugawaji wa Mali Kwa Waarabu ,kuhamisha wa Masai, Deni la Taifa Kufikia Trillion 100, Uagizaji sukari nje kinyume na utaratibu, Kanuni na Sheria, utekaji ,uuaji mfano Mzee Kibao , Uchafuzi wa Uchaguzi n.k

Mengi mnayajua !!


Wakuu bahati nzuri Kwa Sasa Watanzania Tumesoma, tuna Elimu, Kwa pamoja walioko Ndani na Nchi na Nje ya Nchi, tuungane Kwa Umoja wetu kuhakikisha TAIFA LINAKUA NA HAKI.
 
Back
Top Bottom