Jambo moja kubwa aliloongea askofu, ambao ni ukweli mtupu:
Nchi hii, wasomi, wakiwemo wanasheria, ndio watu waoga kuliko wengine wote. Wengine hawajaishia tu kwenye uwoga, bali wamegeuka kuwa wanafiki wakubwa.
Jingine, tufahamu kuwa, hata katika ubaya, kunaweza kuchipua mema. Yaliyotokea awamu ya 5, yachukuliwe positively. Yanatuonesha mapungufu yaliyopo kwenye mifumo yetu ya kiutawala. Sasa tuzipe hayo mapungufu. Pa kuanzia, ni katiba mpya.
Kama awamu ya 6 kweli ina dhamira njema na Watanzania, na Taifa hili, basi iende haraka, tena haraka sana kwenye taratibu za kupata katiba mpya nzuri. Vinginevyo, yote yanayofanyika itakuwa ni cosmetics, kama Askofu alivyotamka.