Askofu Mwamakula: Janga la Kariakoo sio kubwa kama La utekaji

Kwenye huu ujumbe, bila kuweka hisia pembeni huwezi kumwelewa askofu.
 
Tulia shoga wewe.
Nenda tabata kafumuliwe usiku huu
 
Aiseeee
 
Sijaelewa ana maana gani? Anaelewa uzito wa janga ni yule lililomfika sasa yeye limefika lipi kati ya hayo? Au anaongea kisiasa?
 
Kweli,utekaji ni jambo baya lakini sio "AJALI" mbaya kama kuangukiwa na GHOROFA!
Angejaribu kuhisi maumivu makali waliyopitia hawa wahanga,wengine wakatoka hai na wengine wakafariki,basi hekima ya "KIASKOFU" ingemtuma vingine,kama hakuongea wakati wote huko nyuma basi angeendelea kukaa kimya.
Ijulikane hatutetei utekaji Wala kupotea kwa watu,ila watu hawa hupotea kwa sababu mbalimbali,ikiwemo kugombana na mamlaka!
Marehemu wetu Kariakoo waliamka kwenda kazini kama kawàida,ghorofa likawaangukia na wakafa!
Wengine wanapambania Maisha Yao mpaka sasa!
Askofu anafanya makosa makubwa kujaribu kuhusianisha vitu hivi viwili tofauti sana ila si tofauti kabisa.
Taifa linahitaji faraja kwa sasa na si masimango.
 
Yuko
YUko sahihi.....TLS ilipublish report ya Forced Disappeaeances more than 90 individuals.
 
Kwamba utekaji si ajali mbaya?!

Unajua mateso wanayoyapitia wanaotekwa kuanzia wakati wanapotekwa hadi kufikia kuuawa?

Ukiachana na la mzee Kibao, uliwahi kuipata stori ya yule mzee (nimemsahau jina) aliyemgomea jiwe kutoa fungu la fedha kienyeji kwenye ofisi yake alivyotekwa akateswa vibaya (ikiwemo kulawitiwa) kwa siku kadhaa hadi kuuawa?

Mnajaribu kumpinga askofu tu kwa chuki zenu binafsi, ila alichokiongea tukiweka hisia kando yupo sahihi
 
Kizazi hiki nimedeli kwenye logic and argumentation.
 
Mimi na wewe wote hatukuwepo watu walipotekwa,Wala hatukuwepo kwenye Jengo kariakoo!
Sishindani na wewe.Ninachosema ni kwamba kama "Askofu" Angekuwa mtu fair kitaasisi asingelitoa lawama na kulinganisha mambo kama hivi!
Kwa nafasi yake anatakiwa kutenda Haki Kila upande!
Hakuna Serikali iliyowekwa Madarakani Ili kuteka watu,Wala hakuna anayefurahia utekaji!
Tukio hili ni AJALI iliyowakuta watu wengi kwa wakati mmoja,watu wamepoteza Mali na UHAI!.Ghafla sana!..Kuna familia zimefiwa mtu zaidi ya mmoja kwa mara Moja!
Askofu anapata wapi audacity ya kuongea haya!
Au askofu tumewaoverrate sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…