Askofu Mwamakula: Janga la Kariakoo sio kubwa kama La utekaji

Askofu Mwamakula: Janga la Kariakoo sio kubwa kama La utekaji

.

Haoni kwamba mtu kukaa chini ya ghorofa bila ya hewa bila ya kula chochote kwa siku tatu ni kitu kigumu sana.

Alikuwa na hasira na masuala ya utekaji leo kaamua kuja na uzi wa kulinganisha vitu visivyofanana kwa namna yoyote.
Kwahiyo kumshusha mtu kwenye bus na kumpiga risasi ni kitu kirahisi kwa mtendewa?!
 
.

Haoni kwamba mtu kukaa chini ya ghorofa bila ya hewa bila ya kula chochote kwa siku tatu ni kitu kigumu sana.

Alikuwa na hasira na masuala ya utekaji leo kaamua kuja na uzi wa kulinganisha vitu visivyofanana kwa namna yoyote.
Mlinganisho, na mfanano upo.
Hawa wote ni waTanzania, ambao maisha yao yanakatizwa karibu kwa njia zinazo fanana.
Waliopoteza maisha kwa kudondokewa na ghorofa, ni uzembe wa serikali kutofanya kazi zake ipasavyo. Wanao katizwa maisha na utekaji, ni serikali hiyo hiyo, aidha kwa kuzembea na kutotimiza wajibu wake kwa usalama wa wananchi wake, au kwa watendaji wake kuhusika moja kwa moja na uovu huo.
 
Leo ndo nimeona kumbe JF huwa tunapigana tu mikwara tu ya "Great thinker" kumbe wote tuna akili za facebook mnavojikuta watu fulani , cream fulani ya taifa iko JF hata kusoma between line mmeshindwa leo 🤣 Hisia zimewajaa

Mimi sioni kosa la mchungaji kwenye mazungumzo yake amezungumzia "tumeguswa" ila pia anatuamsha wananchi kama tulivyokua wamoja katika hili na tukalifanikisha inawezekana pia hata hili la utekaji tukiungana pamoja tukalikemea.

Kama viongozi walivyokaa pale usiku kucha wakatoa salamu za pole kwenye mitandao ya kijamii , mashirika na kampuni mbalimbali zikaonesha nia hadi kutoa michango , kama waziri mkuu alivyoagiza niffer akamatwe kwa haraka na alipokamatwa kila hatua inaandikwa humu. Media zote Tanzania wanahakikisha kila kipande hakiwapiti.

Mwisho mheshimiwa Rais mliona response yake kwenye ujumbe wake kuna neno "Naagiza" ila watu wakitekwa na kuuawa kikatili hizi nguvu na jitihada mbona kila kiongozi ananywea na hata wakiagizwa linaishia katikati tu. Hata kina millard ayo watatoa tu taarifa ile ya mwanzo wakijitahidi ni msibani.

Unaposema kuna mtu amepoteza watoto ni kweli ni jambo la uchungu nakubaliana nalo lakini kuna mtu amepoteza mwenzi , mume au mzazi kikatili kwa kutekwa na kuuawa ile picha ni maumivu makali pia !!

Tuamke.
 
Kwenye hili janga la kariakoo kuna familia zimepoteza watoto wao wapendwa, wanapomsikia askofu kama huyu wanajikuta wakilaani kauli zake.
Itakuwa ni kutokumuelewa Askofu anamaanisha nini. Askofu hajadharau ajali hiyo bali ameita janga tulilolipa uzito na kusahau kuwa hata huu utekaji ni janga kubwa pengine kuliko la Kariakoo maana walao hili lina matumaini ya uokozi kuliko la utekaji ambalo ndugu na jamaa hawana matumaini na hawajui ndugu yao yuko wapi, kafa au yu hai na katika mateso gani.
Kutotaka kumuelewa Askofu ni ubinafsi tuu au mihemko ya kiitikadi lakini ni ujumbe mzito ukivaa uhusika wa matukio yote mawili.
Jaribu kuwa mzazi wa Soka halafu mzazi wa kijana aliyekwama kwenye jengo Kariakoo halafu jipime ndio utamuelewa Askofu asemacho
 
Japo raia wote tunachukia utekaji lakini hoja yake haina mashiko.
Watu wameenda kukusanyika kwa sababu eneo la ajali linajulikana na linaonekana sasa kwenye janga la utekaji anataka raia wakakusanyike wapi?Je kuna eneo maalum ambako ndio utekaji unafanyika?Je wasiojulikana wana eneo maalumu ambako ndio wanakaa kuwawinda watekwaji?
 
“Juzi tumekuwa na janga pale Kariakoo, nchi imesimama kwa sababu ya janga la pale Kariakoo. Wote tumeguswa kwa ajili ya watu ambao tumetangaziwa 13 wamefariki, wale watu wamekufa wakati wanatafuta Maisha, wamekatishwa na kifusi kama Watanzania ni janga la kitaifa.”


“Lakini iweje mtu anachukuliwa, anachomolewa kwenye basi, anapigwa risasi au anauawa. Watu wanapotezwa, hili tunaliona kama sio janga la kitaifa. Kuna unafiki mkubwa sana katika nchi hii, hawa waliopotea wanatofauti gani na wale waliokufa pale Kariakoo, hawa waliopigwa risasi kuna tofauti gani na wale waliokufa pale Kariakoo. Iweje tubague maafa katika nchi hii. Utekaji unaendelea ambao ndio unatisha zaidi kuliko hata janga la Kariakoo.” – Askofu Mwamakula

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula ameeleza hayo leo Jumanne, Novemba 19, 2024 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Makazi ya Askofu yaliyoko mtaa wa Itunge/Iramba karibu na mtaa wa Ruaha eneo la Kituo cha Polisi, Rift Valley, Kimara Suka jijijni Dar es Salaam.

Mazungumzo ya Askofu Mwamakula yamejikita zaidi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2024, uchambuzi wa tamko la Baraza la Maaskofu wa Katoliki (TEC) na Tamko la Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), hali ya kisiasa ndani ya vyama vya siasa, tatizo la ajira nchini, utekaji, upotezwaji na mauaji ya wanasiasa na wakosoaji wa Serikali, maafa na uwezo wa Serikali kukabiliana nayo, mamlaka na uwezo wa Bunge katika kuisimamia Serikali; muelekeo na mustakabali wa madai ya Katiba Mpya, imani ya Watanzania kwa Serikali yao pamoja na imani yao kwa michakato ya chaguzi na demokrasia kwa ujumla.
Mwanakondoo ameshinda ,tumfuate.
 
Alichokiongea ni kukumbusha tu serikali kwamba maafa sio majengo kuporomoka tu. Washughulike na utekaji pia maana nalo ni janga lingine sio kujibu kifo ni kifo tu.
 
.

Haoni kwamba mtu kukaa chini ya ghorofa bila ya hewa bila ya kula chochote kwa siku tatu ni kitu kigumu sana.

Alikuwa na hasira na masuala ya utekaji leo kaamua kuja na uzi wa kulinganisha vitu visivyofanana kwa namna yoyote.
Kwamba na wewe huoni kuchukuliwa na watu wasiojulikana kupelekwa ununio na kuuwawa huku unaona mpaka kitobolewa macho na kumwagiwa tindikali ni kitu kigumu sana! ?
Hasira ni hulka ya binadamu yeyote hasa mambo yanapokwenda hovyo, unadhani kama sio FAM kituliza zile hasira pale Tanga sinyangekua maafa mengine ambapo mbwa waklngewararua waombolezaji kwa mwamvuli wa kumlinda Master?

Lazima kukubaliana kwamba Impunity is not an order of the day neither the part of our culture!
 
Haya ndio madhara ya kunywea wine chumbani yani watu wana majonzi yeye anaongea usenge kulikuwa na umhimu gani kuoanisha haya matukio
Kwamba unataka kusema Madam President alikunywa Mbege aliposema kifo ni kifo tu kwenye podium huku akijua kwamba familia ndugu na jamaa wa mzee Kibao walikua na majonzi juu ya kifo Cha kikatili alichofanyiwa mpendwa wao, yeye akaongea usenge. Kulikua na umuhimu Gani wa kuonaisha matukio ya nyuma na tukio lile wakati alishauhadaa umma kuwa ametaka uchunguzi wa haraka? Do you think critically?
Unapovuruga utaratibu wa mambo lazima uwe tayari kuishi katika utaratibu uliovurugwa
 
Yeye anazungumza kama nani!
Katiba ya jamhurinya muungano wa Tanzania pamoja na ubovu wake, inatoa Haki na uhuru wa kutoa maoni Kwa jambo lolote lenye maslahi ya umma ilimradi maoni hayo hayavunji katika.

Uhuru wa kutoa maoni na kujieleza ni mojawapo ya kanuni za Kidemokrasia ambapo Tanzania inajinasibu kuwa nchi ya Kidemokrasia na kama inavyoelezwa katika katiba hivyo.

Tanzania ni mwanachama wa Umoja wa mataifa na imeridhia maazimio na mikataba mbali mbali ya Umoja wa mataifa na hivyo watu wake na serikali Yale wanapaswa kuyalinda na kutasimamia. Moja wapo ya maazimio hayo ni kuhusu Haki za binadamu (UDHR (1948). Na miongoni mwa Haki hizo ni Hali ya kuishi, Haki ya kujieleza na kutoa maoni.

Miongoni mwa kanuni za Kidemokrasia ni kuruhusu kufanya kazi kwa Civil society organisations ambapo miongoni mwao ni Taasisi na mashirika ya Dini kama TEC na BAKWATA,.

Moja wapo ya majukumu ya taaisisi hizi katika jamii ya Kidemokrasia ni kuhakikisha serikali na viongozi wake wanawajibika Kwa watu na wanawajibika Kwa matendo Yao yawe mabaya au mazuri! Na katika kutekelezwa majukumu yake njia Moja wapo ni pamoja na kuita vyombo vya habari na kueleza maoni na Msimamo wao, juu ya Haki za watu na mambo mengine yanayohusiana ikiwemo Haki za Kidemokrasia!

Kwakua yeye ni Miongoni mwa viongozi wa mojawapo ya taaisisi hizi ambazo serikali Yako inazitambua kisheria kupitia ofisi ya msajili wao, basi unaweza kupata majibu kuwa ameongea kama nani na kwanini ameongea hayo!

Shuleni ni mahali pa kupata maarifa na sio mahali pa kujifunza uchawa na ujinga kama huo ulioliza.
 
Kwenye hili janga la kariakoo kuna familia zimepoteza watoto wao wapendwa, wanapomsikia askofu kama huyu wanajikuta wakilaani kauli zake.
Mkuu kosa la Askofu hadi asakamwe hivyo ni nini?? Askofu hajabeza vifo vya kariakoo infact ameonyesha kusikitishwa kwake. Mkuu unaposema kuwa familia zilizopoteza watoto wao zina uchungu. Kwani familia za wahanga wa utekaji wao hawana uchungu kupoteza wapendwa wao??

Mkuu Askofu anaishauri serikali kutenda haki katika kushughulikia uzembe uliopelekea janga la kariakoo na janga la utekaji. Janga la utekaji limeua watu wengi pia.

Askofu anasisitiza kuwa watekaji kama wale wa kilivya, walionekana mchana kweupe, mwenye jengo liloanguka, mhandisi na watoa vibali wa manispaa au Jiji wote washughulikiwe kwa mujibu wa sheria.
 
Back
Top Bottom