Askofu Mwamakula: Janga la Kariakoo sio kubwa kama La utekaji

Askofu Mwamakula: Janga la Kariakoo sio kubwa kama La utekaji

Kwamba unataka kusema Madam President alikunywa Mbege aliposema kifo ni kifo tu kwenye podium huku akijua kwamba familia ndugu na jamaa wa mzee Kibao walikua na majonzi juu ya kifo Cha kikatili alichofanyiwa mpendwa wao, yeye akaongea usenge. Kulikua na umuhimu Gani wa kuonaisha matukio ya nyuma na tukio lile wakati alishauhadaa umma kuwa ametaka uchunguzi wa haraka? Do you think critically?
Unapovuruga utaratibu wa mambo lazima uwe tayari kuishi katika utaratibu uliovurugwa
kwani yeye hawezi kunywa?
 
Katiba ya jamhurinya muungano wa Tanzania pamoja na ubovu wake, inatoa Haki na uhuru wa kutoa maoni Kwa jambo lolote lenye maslahi ya umma ilimradi maoni hayo hayavunji katika.

Uhuru wa kutoa maoni na kujieleza ni mojawapo ya kanuni za Kidemokrasia ambapo Tanzania inajinasibu kuwa nchi ya Kidemokrasia na kama inavyoelezwa katika katiba hivyo.

Tanzania ni mwanachama wa Umoja wa mataifa na imeridhia maazimio na mikataba mbali mbali ya Umoja wa mataifa na hivyo watu wake na serikali Yale wanapaswa kuyalinda na kutasimamia. Moja wapo ya maazimio hayo ni kuhusu Haki za binadamu (UDHR (1948). Na miongoni mwa Haki hizo ni Hali ya kuishi, Haki ya kujieleza na kutoa maoni.

Miongoni mwa kanuni za Kidemokrasia ni kuruhusu kufanya kazi kwa Civil society organisations ambapo miongoni mwao ni Taasisi na mashirika ya Dini kama TEC na BAKWATA,.

Moja wapo ya majukumu ya taaisisi hizi katika jamii ya Kidemokrasia ni kuhakikisha serikali na viongozi wake wanawajibika Kwa watu na wanawajibika Kwa matendo Yao yawe mabaya au mazuri! Na katika kutekelezwa majukumu yake njia Moja wapo ni pamoja na kuita vyombo vya habari na kueleza maoni na Msimamo wao, juu ya Haki za watu na mambo mengine yanayohusiana ikiwemo Haki za Kidemokrasia!

Kwakua yeye ni Miongoni mwa viongozi wa mojawapo ya taaisisi hizi ambazo serikali Yako inazitambua kisheria kupitia ofisi ya msajili wao, basi unaweza kupata majibu kuwa ameongea kama nani na kwanini ameongea hayo!

Shuleni ni mahali pa kupata maarifa na sio mahali pa kujifunza uchawa na ujinga kama huo ulioliza.
Ujinga umekujaa umeandika gazeti ili ujisemee shule ulijifunza ujinga na kuhii unajua ushasema kila mmoja yupo huru kutoa maoni mbona wewe unanikataza ondoa ujinga mbele za watu!
 
Ujinga umekujaa umeandika gazeti ili ujisemee shule ulijifunza ujinga na kuhii unajua ushasema kila mmoja yupo huru kutoa maoni mbona wewe unanikataza ondoa ujinga mbele za watu!
Katika andiko lote wewe umeona Hilo Ndio la maana! Jambo la kijinga lazima lioneshwe kwamba ni la kijinga. Mambo mengine ni simple education tu hayahitaji PhD
 
Msisahau,
Janga la kuharibu uchaguzi ni kubwa pia zaidi ya poromoko la ghorofa kariakoo

Kama unatumia hisia kutafakari, hapa hautaelewa pia!
 
“Juzi tumekuwa na janga pale Kariakoo, nchi imesimama kwa sababu ya janga la pale Kariakoo. Wote tumeguswa kwa ajili ya watu ambao tumetangaziwa 13 wamefariki, wale watu wamekufa wakati wanatafuta Maisha, wamekatishwa na kifusi kama Watanzania ni janga la kitaifa.”

“Lakini iweje mtu anachukuliwa, anachomolewa kwenye basi, anapigwa risasi au anauawa. Watu wanapotezwa, hili tunaliona kama sio janga la kitaifa. Kuna unafiki mkubwa sana katika nchi hii, hawa waliopotea wanatofauti gani na wale waliokufa pale Kariakoo, hawa waliopigwa risasi kuna tofauti gani na wale waliokufa pale Kariakoo. Iweje tubague maafa katika nchi hii. Utekaji unaendelea ambao ndio unatisha zaidi kuliko hata janga la Kariakoo.” – Askofu Mwamakula

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula ameeleza hayo leo Jumanne, Novemba 19, 2024 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Makazi ya Askofu yaliyoko mtaa wa Itunge/Iramba karibu na mtaa wa Ruaha eneo la Kituo cha Polisi, Rift Valley, Kimara Suka jijijni Dar es Salaam.

Mazungumzo ya Askofu Mwamakula yamejikita zaidi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2024, uchambuzi wa tamko la Baraza la Maaskofu wa Katoliki (TEC) na Tamko la Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), hali ya kisiasa ndani ya vyama vya siasa, tatizo la ajira nchini, utekaji, upotezwaji na mauaji ya wanasiasa na wakosoaji wa Serikali, maafa na uwezo wa Serikali kukabiliana nayo, mamlaka na uwezo wa Bunge katika kuisimamia Serikali; muelekeo na mustakabali wa madai ya Katiba Mpya, imani ya Watanzania kwa Serikali yao pamoja na imani yao kwa michakato ya chaguzi na demokrasia kwa ujumla.
HUYU MSHE,,,,,,,,,,,,,,,,,,,DADEK YAANI NILITAKA NIMTUKANE TUSI KUBWA SANA SEMA LIMEPOTEA GAFLA ANAONGEA UJINGA GANI HAPA YAANI WATU WALIOKUFA KARIAKOO KWAKE SIYO BINADAMU ? SIJU HATA HUO UASKOFU NANI ALIMPATIA MTU MPUMBAVU NAMNA HII?
 
Ni mtazamo wake maana maumivu yake ni makali kwa pande zote mbili kwa wazazi ambao watoto wao wameangukiwa na vifusi na kwa wazazi ambao watoto wao wametekwa
SASA KWANINI ASEME UPANDE MMOJA UNAUMIA ZAIDI KULIKO WA KARIAKOO MIJITU MINGINE WALA HAIFAI KUKAA HAPA DUNIANI INAMALIZA HEWA YA BURE KAMA HILI JITU LINAJIITA ASKOFU
 
SASA KWANINI ASEME UPANDE MMOJA UNAUMIA ZAIDI KULIKO WA KARIAKOO MIJITU MINGINE WALA HAIFAI KUKAA HAPA DUNIANI INAMALIZA HEWA YA BURE KAMA HILI JITU LINAJIITA ASKOFU
Kwakweli kwenye utekaji watu wanaumia zaidi,

Mtu anatekwa, anateswa siku kadhaa au wiki kadhaa, mwisho wa siku anauawa kikatili,

Kwenye poromoko hakuna mateso ya wiki kadhaa Kama yule aliyetekwa
Ukuta ukikuporomokea unakufa papo hapo au baada ya dakika kadhaa

Utekaji ni endelevu,
Mtu yeyote atatekwa popote. Chance ya mtu kutekwa Tanzania ni kubwa kuliko ile ya kuporomokewa ghorofa

Utekaji umeua watu wengi kuliko ghorofa

Majanga makuu ya Taifa ni matatu tu

1, Katiba

2. Ajali barabarani

3. Utekaji

Ukiamua kuorodhesha majanga madogomdogo ya Taifa ni mengi ikiwa pamoja na kuporomoka ghorofa
 
HUYU MSHE,,,,,,,,,,,,,,,,,,,DADEK YAANI NILITAKA NIMTUKANE TUSI KUBWA SANA SEMA LIMEPOTEA GAFLA ANAONGEA UJINGA GANI HAPA YAANI WATU WALIOKUFA KARIAKOO KWAKE SIYO BINADAMU ? SIJU HATA HUO UASKOFU NANI ALIMPATIA MTU MPUMBAVU NAMNA HII?
Tumia akili kufikiri
 
Msisahau,
Janga la kuharibu uchaguzi ni kubwa pia zaidi ya poromoko la ghorofa kariakoo

Kama unatumia hisia kutafakari, hapa hautaelewa pia!
mihapase hawezi elewa hili.. ataishia kutukana.. na hii ni kutokana na janga alilopata la elimu duni kutoka kwa ccm.
 
Mkuu kosa la Askofu hadi asakamwe hivyo ni nini?? Askofu hajabeza vifo vya kariakoo infact ameonyesha kusikitishwa kwake. Mkuu unaposema kuwa familia zilizopoteza watoto wao zina uchungu. Kwani familia za wahanga wa utekaji wao hawana uchungu kupoteza wapendwa wao??

Mkuu Askofu anaishauri serikali kutenda haki katika kushughulikia uzembe uliopelekea janga la kariakoo na janga la utekaji. Janga la utekaji limeua watu wengi pia.

Askofu anasisitiza kuwa watekaji kama wale wa kilivya, walionekana mchana kweupe, mwenye jengo liloanguka, mhandisi na watoa vibali wa manispaa au Jiji wote washughulikiwe kwa mujibu wa sheria.
Serikali inaongozwa na watu kama yeye, kwanza atimize wajibu wake ipasavyo ili awe na uhalali wa kimaadili wa kushambulia hao wahanga wa Kariakoo, vidonda vya kupoteza wapendwa wao bado ni vibichi kabisa angalau angetulia kidogo akiuacha muda ukipita.
 
HUYU MSHE,,,,,,,,,,,,,,,,,,,DADEK YAANI NILITAKA NIMTUKANE TUSI KUBWA SANA SEMA LIMEPOTEA GAFLA ANAONGEA UJINGA GANI HAPA YAANI WATU WALIOKUFA KARIAKOO KWAKE SIYO BINADAMU ? SIJU HATA HUO UASKOFU NANI ALIMPATIA MTU MPUMBAVU NAMNA HII?
1. Watu wote waliokufa katika majanga yote mawili ni binadamu na ni watanzania ambao wamepoteza haki zao za kuishi ambazo ni zawadi kutoka kwa Mungu.
2. Vifo vyote viwili vimeacha majeraha na maumivu makubwa kwa ndugu jamaa na marafiki wa wale walipoteza maisha yao, ikizingatiwa kwamba wengine walikua ndio wanajitafuta kimaisha na wengine walishaanza kujitegemea.
3.Tofauti ni kwamba ile Sauti ya juu ya mamlaka ya nchi ambayo ina dhamana na wajibu wa kikatiba kulinda uhai wa watu na kuhakikisha kwamba watu wote wanakua salama wakati wote na kwamba kama ni majnga kama la kariakoo basi kuwe na utayari uliokamilika kukabiliana na majanga husika lakini hali ilikua tofauti.
4. Utofauti mwingine ambao naamini ulipswa hata wewe kunukuu hayo maneno hapo juu ni Tamko la namba moja kwamba kifo cha mtu aliyetekwa ni kifi kama kifo kingine tu na hakipaswi kupigiwa kelele kana kwamba ni cha ajabu sana, lakini naamini hukufanya hivyo pasina kujua kuna wakati litatotea tofauti.
5. Juhudi zinazofanyika Kunusru uhai wa watu wa kariakoo pamoja na faraja ya serikali zingetumika kuwatafuta wale wanaosadikika kutekwa na wale waliotajwa zingetumika hivi ni dhahiri huo mtanziko usingekuepo.
6.Tabia ya serikali zote duniani kuwa na impunity na kukwepa accountability huwafanya raia na wao kuishi mfumo huo wa maisha ambao ni hatari sana kwa jamii. Rejea Tundu Lissu na Juzi yule Mwenyekiti wa CCM kilolo.
7. Kosa la askofu hapa ambalo naliona hata mimi ni kusema janga la kariakoo sio kubwa kuliko la utekaji mitaarafu yote yamegharimu uhai wa binadamu.
 
Unafiki unaenda kuua nchi, kwa kweli kama asemavyo Askofu, Watanzania tumeonyesha ujinga wetu kwa kubagua matukio yanayoondoa uhai wa wenzetu!!

Ni kama vile Watanzania wote tunafahamu tayari kuwe serikali ndio inayoteka na kuua wananchi wake, hivyo kwa kuwa tunaichukulia serikali kama ni dude lililoshindikana tunaogopa kusema lolote au kukemea kwa umoja wetu pale mtu anapotekwa na kuuwawa.

Shame on us!!
 
Attachments

  • IMG_20241024_115541_382.jpg
    IMG_20241024_115541_382.jpg
    656.6 KB · Views: 1
Kwamba na wewe huoni kuchukuliwa na watu wasiojulikana kupelekwa ununio na kuuwawa huku unaona mpaka kitobolewa macho na kumwagiwa tindikali ni kitu kigumu sana! ?
Hasira ni hulka ya binadamu yeyote hasa mambo yanapokwenda hovyo, unadhani kama sio FAM kituliza zile hasira pale Tanga sinyangekua maafa mengine ambapo mbwa waklngewararua waombolezaji kwa mwamvuli wa kumlinda Master?

Lazima kukubaliana kwamba Impunity is not an order of the day neither the part of our culture!
Kulinganisha hayo madhila haswa kwa muda huu ni kosa kalifanya huyo Askofu, angesubiri muda upite wakati wafiwa wakiwa wameanza kupona majeraha ya kuondokewa na wapendwa wao.

Hakuna janga lenye afadhali siku zote maumivu ni lazima yatokee, lakini hekima kwenye maongezi humpunguzia au humuongezea mtu ile hali ya kukubalika au kukataliwa.
 
Naungana na wewe katika Paragraph ya pili ila ya kwanza nitakuuliza swali baada ya kukupa maelezo kwamba. Viongozi waliopewa dhamana katika jamii wanaposhindwa kujenga misingi ya kuheshimu taratibu jamii ilizojiwekea ili kulinda heshima na utu wa mtu, ni rahisi kwa wale wanaoongozwa kuanza kuiga utamaduni wa namna hiyo na kuufanya wa kawiada sana bila kujali unasababisha maumivu kiasi gani.
swali Langu, Je Rais wa nchi alisubiri muda upite wakati wafiwa wa Mzee Kibao wameanza kupona majeraha ya kuondokewa na mpendwa wao kabla ya kuja hadharani na kusema kifo ni kifo tu na kifo cha Kibao hakipaswi kustajabisha? wakati utaratibu mzima wa kumkamata mpaka kumuuwa unaelezwa uliponzia na watu waliohusika kutajwa hadharani? Lengo la Askofu ni kuwaonesha watawala na umma kwamba thamani ya uhai wa mtu haipaswi kupuuzwa hata kidogo. Nguvu inayotumika kariakoo ingetumika kuwatafuta watekwaji na watekaji watu wangelia pamoja lakini ni tofauti kabisa.
 
Swala la marehemu Kibao na swala la kuanguka kwa jengo kariakoo ni vitu tofauti japokuwa yote mawili ni majanga.

Unaleta ile hadithi ya swali la nyongeza bungeni, kwamba umeamua kuchomekea mada nyingine kwenye mada ya huu uzi inayojitegemea.
 
Back
Top Bottom