Askofu Mwamakula: Mpendwa Mama Samia Suluhu Hassan, mambo yafuatayo ni muhimu

Baba Askofu mi na familia yangu tunaelewa mchango wako katika kulipigania taifa hili,uliyoongea hapo akiyafanyia kazi hakika ataongoza miaka 10 Ila akikengeuka anajua Mungu..........
 
Hiyo ndio kauli mbiu ya kanisa la Moravian Duniani.

Ni kama ''Tumsifu Yesu Kristu'' kwa Roman Catholic au ''Wabillah Tawfiq'' kwa Waislam

''Mwanakondoo Ameshinda, Tumfuate''

'' Our Lamb has Congured, Let us follow him ''

'' Vicit Agnus Noster, Sum Sequamur ''

'' Unitas fratrum, Jednota Bratriska ''
 
Walilifahamu hilo walipopendekeza jina 2015.

Yaonekana kila kitu kilipangwa na yaonekana hata yeye alikuwa akifahamu hilo.

Ila kashikashi za chuki kutoka pande zote za dunia ndizo zimechangia kwa kiasi kikubwa.
Yeah watu waweza kuchangia kifo cha mtu. Kumsema vibaya wakimsema vibaya
 
Na kawaacha masikini kweli kweli!

CCM msirudie hili kosa tena la kuleta mtu mwenye ugonjwa usiotibika.

"Lowasa ni mgonjwa hata mwezi amalizi" Alisikika Samwel sitta na celina kombani huku jiwe akiruka tmk wanaume na kupiga pushup Kumdhihaki Lowasa.
Maisha yetu ni funzo kwa tulio hai.
 
Yeah watu waweza kuchangia kifo cha mtu. Kumsema vibaya wakimsema vibaya
Ogopa Sana kuombewa mabaya na mahakama ya Jamii. Watu wakikulaani Mungu hawezi kuwa upande wako. Baraka na laana ya mtu imo ndani ya ulimi wake.
 
Maandishi yako ni mazuri, lakini yanaelezea kitu kimoja tu: aongoze, asitawale, na afuate katiba na sheria za nchi. Marehemu alitawala kwa matakwa yake na kuisigina katiba. Suluhu upinzani wake mkuu ni CCM, chama kusichotaka aina yoyote ya mageuzi endelevu, kisicho simamia au kukubali siasa za ushindani.
 
Reactions: BAK
Hakuna kiongozi dhaifu, bali walikuwa chini ya kiongozi 'haambiliki' na wakabuni mbinu ya kuishi, ya kumsifia na kumpamba hata akiharibu.
 
Mkuu hii nimeiona mahali nikaipenda na kuamua kuileta hapa jamvini. Mwandishi ni Askofu Mwamakula.
 
Pia walikuwa wakimjaza uongo wa kila aina kwa kujua nini alikuwa anataka kusikia. Hivyo walichojali ni matumbo yao na si maslahi ya Nchi.
Hakuna kiongozi dhaifu, bali walikuwa chini ya kiongozi 'haambiliki' na wakabuni mbinu ya kuishi, ya kumsifia na kumpamba hata akiharibu.
 
Kitendo cha kutumia task force kuwapora wafanyabiashara mali zao pesa zao Madini yao na wengine kufungiwa Account zao biashara zao huku baadhi wakiikimbia Nchi mpaka sasa kilikuwa kitendo Hatari na huenda laana kubwa imetokea huko.
Na Majaliwa usimsahau, hakuwahi msaidia marehemu. Zama fulani mfalme aliugua kichaa. Aliamuru kuuwawa wazibua vyoo na mitaro, akidai hawana akili. Waziri mkuu alimwambia,' hewala mfalme, lakini nasi tujiandae kuuawa. Maadamu tunakula na kunya, vyoo na mitaro vitaziba, na kila azibuaye ata uawa, hatimae tutabaki sisi na atakaepangwa kuzibua nae atauawa' mfalme kichaa yakamwingia na kufuta amri. Majaliwa wetu hakuwahi kuthubutu, mpaka hatua ya mwisho kuongopa kuwa jpm ni mzima wa afya.
 
Viongozi waliopo wajifunze utawala bora. Ndugu wa jpm wana majonzi makubwa, masimango yanayo elekezwa kwa marehemu kwa utawala wa kidhalmu alio utekeleza yana watesa zaidi.
 
Central line imefanyiwa ukarabati mkubwa. Hela ya SGR ingetumiwa kujenga madarasa na kuajiri walimu, leo ajira kwa kada hiyo ingekuwa historia. Na karibu 10% ya hela hiyo hurudi serikali I kama payee.
 
Huyu kijana Sabaya watu wanavyomlaani vibaya, karma itamshugulikia kama ilivyomshugulikia baba yake aliyetangulia..
 
Atekeleze haya haraka iwezekanavyo ili tuweze kupunguza nyasi kwenye njia ya kuelekea msalani zilizomea kwa kipindi cha miaka takribani 6 iliyopita.


Unataka kusema Watu walikuwa hawaendi choo kwa takriban miaka 6 ndiyo sababu nyasi zikaota katika njia ya chooni ??!🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…