Askofu Mwamakula: Tundu Lissu aomba hifadhi Ubalozi wa Ujerumani baada ya vitisho vya uhai wake

Askofu Mwamakula: Tundu Lissu aomba hifadhi Ubalozi wa Ujerumani baada ya vitisho vya uhai wake

Lissu arudi zake nje Akatafute chuo au kazi nje afanye aachane kuzikomboa maiti. Ukimsaidia masikini dhidi ya watawala unahatarisha maisha yako, wote waliotaka kuwakomboa masikini waliuliwa martin luther, lumumba, Ken sarowiwa, tsvangirai, Jesus of Nazareth, Bob Marley, Luck dube, Mkwawa,Haile selasie, mitume 12 wa Jesus,nk.

Masikini waache wapambane na Hali zao kwani wao washazoea kuishi kimasikini masikini kinyonge kinyonge ukisema uwasaidie kwanza wanakuona adui.

Mfano polisi wako radhi kuitetea ccm inayowafanya wazidi kuwa masikini kuliko kumtetea mtu au watu wanaopambania umasikini wao. Hizi ni kanuni za usimsaidie masikini utahatarisha uhai wako
 
Hii inaenda kuwa U-turn kwenye siasa za Tanzania na hatma yake.

Nauona mwanzo mbaya wa hii serikali, Jana na Leo Aljazeera wameanza kurusha video za Zanzibar wanajeshi wakipiga watu, na kusema Magufuli kaapishwa kwa ushindi uliotawaliwa na wizi wa kura huku wakionesha kura zilizokamatwa na waliwahoji wasimamizi wa kimataifa ambao bila kumun'gunya maneno wamesema ulitawaliwa na udanganyifu.
 
Nimeona kuna uzi humu, kwa mujibu wa Askofu Mwamakula anasema Lissu yuko ukimbizini katika ubalozi wa Ujerumani kutokana na kutishiwa maisha.

Wajameni!

Hivi si ni Lissu huyu huyu alipowasili toka Ubelgiji alisema hadharani kwamba haogopi chochote maana tayari alishaonja mauti na hana cha kupoteza?

Si ni Lissu huyu huyu wakati wa kampeni alitaka kulala barabarani wakati alipozuiwa kwenda kukagua soko huko kibaha? Na alisema atalala hapo na wamfanye chochote maana baogopi?

Si ni huyu huyu Lissu wakati wa kampeni alikuwa anashuka kwenye gari na kutunishiana misuli na polisi na kwenda mbele ya mitutu ya bunduki na kusema fanyeni mnachotaka?

Si ni huyu huyu alikuwa anapanda usafiri wa mwendokasi na kwenda kununua nyanyaKkariakoo bila kuogopa chochote wakati kazuiwa kufanya kampeni?

Si ni huyu huyu alisema atarusha chopa yake toka KIA kwenda Dar hata kama hana kibali na wafanye chochote maana haogopi?

Iweje leo aseme kakimbilia ubalozini kisa vitisho?

Kwanini Lissu kama kazoea maisha ya Ulaya na anatamani arudi kuishi huko asitumie njia za kisheria kuomba vibali badala ya hivi vituko?
 
This is very sad!

Yaani mtu yupo uhamishoni ndani ya nchi yake!!??

Hapana kwa kweli. Hii haikubaliki hata kidogo.

Hivi kosa lake ni nini hasa mpaka watake kumfanyia unyama namna hiyo?

Hapana. Uovu huu lazima ukemewe na watu wote wenye mapenzi mema na Tanzania.

Totally unacceptable.
Kosa lake ni kutaka kuharibu shibe za watu
 
Wewe Askofu acha kuingilia rizki za watu, hii kazi ya uandishi wa habari ina wenyewe na wamesomea na tamko kama hili ilibidi wapewe wao na walipwe kama utaratibu unavyotaka ili na wao wapate riziki kama wewe unavyopata kanisani kwako kwa kuwaaminisha watu kua unawaunganisha na Mungu ingawa hata ww Mungu hakujui.

Cha msingi achana na siasa wewe endelea kupige mishe kanisani kwako. Haya maisha tu acha kuvamia vamia kazi za watu. Na haya unayoyaongea unaweza kuyathibitisha?? Kingine nikuulize mbona kama hunenepi hivi shida nn??? Acha roho mbaya hahaaa
 
Mkuu umebebwa na huli igizo la lisu?

Si ni huyuhuyu wakati wa kampeni alidiriki hata kusema atarusha chopa yake bila kibali maana haogopi chochote?
Kuna kipindi aliwahi kusema kuwa anafuatwa fuatwa na watu ‘wasiojulikana’.

Nikayachukulia poa hayo madai yake.

Muda mrefu haukupita, akashambuliwa.

Siwezi tena kuyapuuza madai ya kutaka kumtoa uhai wake.

Ni jambo la kiutu. Si la kisiasa hata kidogo.
 
HII NI NDIO HALI HALISI: Lisu arudi zake nje Akatafute chuo au kazi nje afanye aachane kuzikomboa maiti. Ukimsaidia masikini dhidi ya watawala unahatarisha maisha yako, wote waliotaka kuwakomboa masikini waliuliwa martin luther, lumumba, Ken sarowiwa, tsvangirai, Jesus of Nazareth, Bob Marley, Luck dube, Mkwawa,Haile selasie, mitume 12 wa Jesus,nk.Masikini waache wapambane na Hali zao kwani wao washazoea kuishi kimasikini masikini kinyonge kinyonge ukisema uwasaidie kwanza wanakuona adui.

Mfano polisi wako radhi kuitetea ccm inayowafanya wazidi kuwa masikini kuliko kumtetea mtu au watu wanaopambania umasikini wao. Hizi ni kanuni za usimsaidie masikini utahatarisha uhai wako: WAACHE WAFU WAZIKANE; MUNGU MWENYEWE ALISHAACHANA NA AFRICA SEMBUSE WEWE.
 
Idadi ndogo ya wapiga kura huku chama cha jiwe kikipata kura chache, kitendo hicho kimemuuzi jiwe maana anaona Lisu ndio kampotezea umaarufu bandia alioujenga kwa kutia watu hofu. Na ukizingatia jiwe anataka kujiongezea muda wa kukaa madarakani, anaona Lisu ndio kikwazo cha dhahiri. Namna pekee anaona ni kumuondoa duniani.
 
Wakati wa kampeni alifunga barabara akiwa Chato sasa nini kimemsibu? Au sababu amekuwa sio mgombea ni raia wa kawaida!
Screenshot_20201106-101541.png
 
Kuna kipindi aliwahi kusema kuwa anafuatwa fuatwa na watu ‘wasiojulikana’.

Nikayachukulia poa hayo madai yake.

Muda mrefu haukupita, akashambuliwa.

Siwezi tena kuyapuuza madai ya kutaka kumtoa uhai wake.

Ni jambo la kiutu. Si la kisiasa hata kidogo.

Ni kweli.
Mpaka ameomba asylum basi amejiridhisha kuwa tishio juu ya maisha yake ni real

Vitisho vya wapambe wa Jiwe juu ya maisha ya Lissu havijawahi kukoma, wanasema wazi kuwa maadam walimkosa mara ya kwanza, safari hii hawatamkosa tena!
 
Ameua wengi gizani mfano Ben Saanane, Azory na jaribio lililoshindikana kwa Lissu ila sasa na kuendelea hatajificha tena maana hana cha kupoteza ameshajua hapendwi hivyo tutarajie huyu kiumbe anaemtaja MUNGU kila wakati kuua watu wengi zaidi.
 
Japo awali ilikuwa hivyo ila kwa sasa huenda yapo maelekezo mahudisi. "Uchaguzi umekwisha" X3
 
Ni kweli.
Mpaka ameomba asylum basi amejiridhisha kuwa tishio juu ya maisha yake ni real

Vitisho vya wapambe wa Jiwe juu ya maisha ya Lissu havijawahi kukoma, wanasema wazi kuwa maadam walimkosa mara ya kwanza, safari hii hawatamkosa tena!
Kuna mambo mengine wala si ya kisiasa kabisa!

Tundu Lissu ana kilema cha maisha kilichotokana na jaribio la kutaka kumuua.

Lissu siyo mwendawazimu.

Kama alisema mara ya kwanza na baadhi yetu tukampuuza na yakatokea kweli.

Si vyema wala busara kuanza kumdhihaki sasa hivi anapotuambia maisha yake yapo hatarini.
 
Back
Top Bottom