Mshauri TL aache usanii!
Anataka ku-buy time na kupumbaza Watanzania, wakati huu akitafakari cha kufanya baada ya kushindwa kwa kishindo kikuu katika uchaguzi uliopita, ambao aliaminishwa kuwa angeibuka na ushindi mkubwa.
Na kutapatapa huku kunaashiria hamu na matamanio yake ya kukimbia nchi, kabla ya Mamlaka za kisheria nchini hazijaanza kushughulikia kadhia ya kushambuliwa kwake kwa risasi kule Dodoma, shauri ambalo liliachwa pending kwa vile shahidi mkuu aliyeshuhudia tukio hilo, ambaye ni dereva wake, akisita kuisaidia polisi na kuendelea kufichwa au kujificha.
Bila shaka kukimbilia ubalozini , ni karata mojawapo ya kufanikisha azama yake, akijua kuwa asingeweza kwenda nje ya nchi kwa njia za kawaida bila serikali kumzuia na kumtaka kwanza ashirikiane na vyombo vyake kushughulikiwa kadhia ya kushambuliwa kwake, ili sheria ichukue mkondo wake.
Asiwe na hofu za kusadikika kwani Watanzania wanamhitaji zaidi akiwa hai, na hakuna anayemhitaji akiwa mfu!...Ndio maana ushirikiano wake unahitajika sana wakati huu kuliko wakati mwingine, katika kutegua kitendawili cha kushambuliwa kwake.