This is very sad!
Yaani mtu yupo uhamishoni ndani ya nchi yake?
Hapana kwa kweli. Hii haikubaliki hata kidogo.
Hivi kosa lake ni nini hasa mpaka watake kumfanyia unyama namna hiyo?
Hapana. Uovu huu lazima ukemewe na watu wote wenye mapenzi mema na Tanzania.
Totally unacceptable.
unajua kuzunguka mbuyu, but I know inside unawaza kitu tofauti na unachoandika hapa sema unaogopa kuwakasirisha lumumba wenzio, nimekuelewa usijali.Walimnyima pesa za matibabu na akarudi akiamini watampigia kura za Urais.
Vihoja vya upinzani haviishagi
Lissu hawezi kufungwa na wale mawakili wenu "mandazi", tatizo ni risasi tu.Wacha upelelezi ukamilike, kesi zake zote zisikilizwe na watanzania wajue ukweli. Mungu amlinde Tundu hadi apate haki yake na walimpiga risasi wajulikane ili iwe mwanzo wa watanzania na yeye mwenyewe kuijua serikali yao.
Mwakyembe na Magufuli walinusurika vifo lakini hawakuwahi kuwatuhumu wapinzani wala serikali sababu wanaelewa serikali haiwezi fanya upuuzi kama huo
🤣🤣🤣🤣🤣kipanga ampiga mkoloni🤣🤣🤣Ni kipigo cha kipanga ampiga mkoloni, naamini ushawahi kukisoma kitabu hiki shule ya msingi. Namshukuru sana Mungu kwa ushindi huu, Robert Amsterdam alikuwa anaiundermine sana Tz, sasa tumemnyosha na kibaraka wake. NEVER EVER MESS UP WITH TZ, TAIFA LA MUNGU HILI. ROBERT AMSTERDAM HAKUJIFUNZA KWENYE CORONA, NAAMINI MATOKEO YA UCHAGUZI HUU UTAKUWA FUNDISHO KWAKE. NAJUA WATAKUWA NA MIKAKATI YA KUSABOTEJI UTAWALA WA AWAMU YA 6, WATAJARIBU LAKINI BAADAE WATASHINDWA.
Kama na wewe hili umeliona basi wengine tunyamaze maana this is too much. Kama ningekuwa lissu ningeondoka nikaishi kwingine ambako ni salama zaidi.This is very sad!
Yaani mtu yupo uhamishoni ndani ya nchi yake?
Hapana kwa kweli. Hii haikubaliki hata kidogo.
Hivi kosa lake ni nini hasa mpaka watake kumfanyia unyama namna hiyo?
Hapana. Uovu huu lazima ukemewe na watu wote wenye mapenzi mema na Tanzania.
Totally unacceptable.
Hakuna anaetaka kumfunga rais wako.Lissu hawezi kufungwa na wale mawakili wenu "mandazi", tatizo ni risasi tu.
Issue ya Mwakyembe na Magufuli hapa ni tofauti, nakucheki tu unavyo force tukuelewe!
Labda utupe zawadi kwanza.
Hivi kama watu wana ‘mandate’ ya 84% ya wapiga kura, kwa nini wamnyanyase Lissu kiasi hicho?
That’s just wrong.
Kwa asilimia 84%Unaamini kwenye uchaguzi huu vibaraka na wanaowatuma wamepikea message clear bila chenga kutoka kwa umma wa watanzania?
Nimependa ulichoandika hapa; basing on that story itself, it seems usalama wa Lissu utaendelea kubakia mikononi mwa ubalozi wa Ujerumani mpaka pale serikali yetu itakapoamua either kumpa Lissu ulinzi binafsi, au kumpa kibali akaishi nje ya nchi...hili suala KIDIPLOMASIA limekaaje? linatatuliwa namna gani?
..kwasababu huku uraiani, pamoja na kudai kutishiwa maisha, Tundu Lissu anakabiliwa na kesi mbalimbali.
..hata kama Wajerumani wakiamua kumpa hifadhi ya ukimbizi, Tundu Lissu atatoka vipi humo ubalozini kwenda Ujerumani bila kukamatwa na serikali?
..vilevile, maofisa wa ubalozi wanatekeleza vipi majukumu yao huku wakiwa na "mgeni" ambaye hawakumtarajia ktk ofisi zao?
..tukio hili limenikumbusha tukio la Julian Assange aliyekaa kwenye ubalozi wa Equador London kwa miaka karibu saba.
..au tukio la Ethiopia 1991 ambapo viongozi wakuu wa serikali iliyopinduliwa walipewa hifadhi ktk ubalozi wa Italy nchini humo.
..mwisho, nakubaliana na sentiments zako, Nyani Ngabu, kwamba siasa zetu zina matatizo na tunahitaji kuzirekebisha.
cc Nguruvi3
Umeona mbali....Aseme hiyo ni mbinu ya kukimbia kesi zake...
Kama na mimi nimeliona?Kama na wewe hili umeliona basi wengine tunyamaze maana this is too much. Kama ningekuwa lissu ningeondoka nikaishi kwingine ambako ni salama zaidi.
Kuna tofauti kati ya demokrasia ya nchi ya Tanzania kwa ustawi wa Tanzania; na demokrasia ya Tanzania kwa ajili ya ustawi ulaya, amerika na asia..sidhani kama mambo haya yanatokea kwa bahati mbaya.
..You need to go back and listen to Jpm speeches when he was a Minister in JK's govt'.
..Utaona kabisa kwamba ni mwanasiasa / kiongozi ambaye hakubaliani na demokrasia ya vyama vingi.
..Baada ya hapo njoo sasa uangalie nini kimevitokea vyama vya siasa, na nini kimetokea ktk chaguzi zote ndogo, tangu Jpm aingie madarakani.
..Halafu linganisha na chaguzi ndogo wakati wa BWM, na JK. Then angalia kilichotokea ktk uchaguzi mkuu wa October mwaka huu.
..Kuna hotuba za Jpm ambapo anawasifia viongozi kama Muammar Gaddafi na Saddam Hussein.
Hoja zako nyepesi sana bibie, mlitaka vyama vingi wenyewe, kama hamvitaki vifuteni, kila siku unasema kuna tofauti ya demokrasia kati ya nchi zilizoendelea na zinazoendelea, sijui hizo aina za demokrasia ulijifunza wapi?Kuna tofauti kati ya demokrasia kwa ustawi wa Tanzania na demokrasia kwa ajili ya ustawi ulaya, amerika na asia
Ndio maana siku zote vibaraka na mabwana zao wakishindwa kutimiza mipango yao ya kuipata hiyo demokrasia kwa maslahi yao wanajificha nyuma ya wanachotuaminisha kuwa demokrasia kufanikisha uwepo wa vurugu au vita ili wapate wanachokitaka.
Jiulize ile demokrasia waliyoipigania watu wa ghaddaf wameipata?
Jiulize hao wadai demokrasia wameshindwaje kumaliza vita ya drc? Au wanasubiri mission ikamilike, nchi ibaki tupu ndio watulize ghasia.
Tundu anatafuta kusikika tu wala hana la maana lolote, kama ni adui labda jamii yake inayo mzunguka yeye mwenyewe kwenye chama chake au amewahi kupindisha sheria kwa mtu kwenye makesi yao huko..nje na hivyo siamini serikali kuhangaika na mtu mdogo huyo,pia hua anapenda sifa tu kwenye mazungumzo yake mengi ambayo mala nyingi hayana lolote la maanaAMEANDIKA:
BABA ASKOFU EMMAUS BANDEKILE MWAMAKULA.
USALAMA WA MAISHA YA LISSU UKO HATARINI, AKIMBILIA KUPATA HIFADHI KATIKA UBALOZI WA UJERUMANI JIJINI DAR ES SALAAM!
Jana tarehe 5 Novemba 2020 nilizungumza na aliyekuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mheshimiwa Tundu Lissu ambaye anaishi Uhamishoni katika Ubalozi wa Ujerumani jijini Dar es Salaam. Tulikubaliana kuwa mimi kama Askofu na Mshauri wake katika Masuala ya Kiroho, niwajulishe Umma wa Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa kwa ujumla kuhusu hali ya Usalama ya Mheshimiwa Lissu.
Kupitia mazungumzo yale, Mheshimiwa Lissu alieleza kuwa mara baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, alianza kutishiwa maisha yake. Baada ya vitisho kuzidi kuongezeka, Mheshimiwa Lissu alipokea pia taarifa kutoka kwa 'wasamalia wema' waliomtahadharisha kuwa kulikuwa na 'maelekezo maalum' ya kutaka 'vijana wamalizane kabisa na Lissu' safari hii!
Baada ya kutafakari kwa kina taarifa za vitisho hivyo pamoja na taarifa kutoka kwa 'wasamalia wema', Mheshimiwa Lissu aliamua kwenda kutafuta hifadhi ya muda sehemu nyingine tofauti na nyumbani kwake jijini Dar es Salaam hatua ambayo ilionekana kama ni kuhatarisha usalama wa maisha ya watu wengine. Ndipo alipoamua kutafuta hifadhi katika Ubalozi wa Ujerumani jijini Dar es Salaam siku chache. Siku alipokwenda Ubalozini, alipowasili na akiwa nje ya Ubalozi akisubiri taratibu za Ubalozi pale Umoja House, Polisi waliokuwa katika magari mawili walifika pale Ubalozini na kumkamata na kwenda naye Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati (Central Police) jijini Dar es Salaam. Ndipo Maafisa wa Ubalozi waliamua kumfuatilia Mheshimiwa Lissu kwa nyuma na kusubiria pale Central, jambo ambalo liliwafanya Polisi waamue kumuachia kwa kuogopa kelele zaidi kutoka Jumuiya ya Kimataifa.
Mheshimiwa Lissu alinieleza kuwa Maafisa wa Ubalozi wameendelea kuwasiliana na Serikali ya Tanzania kupitia Mheshimiwa Palamagamba Kabudi kuhusu hifadhi yake, lakini Serikali hadi kufikia jana tarehe 5 Novemba 2020, Serikali ya Tanzania ilikuwa inasita kutoa kibali kwa Ubalozi unaoshughulikia masuala ya Lissu kwa kisingizio kuwa Lissu aombe ruhusa ya Kimahakama kwa kuwa anazo kesi Mahakamani. Hoja ya Serikali ilionekana kutokuzingatia au kutokujali tishio dhidi ya uhai wa Mheshimiwa Lissu.
Katika mazingira yaliyopo, tunaiomba na kuishauri Serikali itoe kauli kuhusu kumhakikishia usalama Mheshimiwa Lissu. Kukaa kimya kwa Serikali pasipo kutoa hakikisho lo lote la usalama kwa Mheshimiwa Lissu kutapelekea watu kufikiri na kuamini kuwa Serikali inahusika au iko nyuma ya vitisho dhidi ya maisha ya Lissu.
Ikumbukwe kuwa miaka mitatu iliyopita, Mheshimiwa Lissu aliwahi kulalamika mara kadhaa kuwa kuna watu walikuwa wakimfuatilia na kuwa maisha yake yalikuwa hatarini na haikupita muda mrefu akashambuliwa na risasi mchana jijini Dodoma na hadi sasa hakuna taarifa za kukamatwa kwa mtu ye yote kutokana na tukio lile.
Baada ya kutafakari kwa kina kuhusu hali halisi ya usalama wa Mheshimiwa Lissu katika mazingira ya sasa na baada ya kushauriana na wadau mbalimbali, imeonekana ni vema na ni hekima na usalama kwa Mheshimiwa Lissu kuendelea kuishi Uhamishoni katika Ubalozi wa Ujerumani jijini Dar es Salaam hadi pale itakapoamriwa tena hapo baadaye. Kwa sasa Mheshimiwa Lissu pamoja na baadhi ya Wasaidizi wake wapo katika Ubalozi wa Ujerumani ambapo wanaendelea kupata hifadhi.
Ninaandika haya kama Askofu Mshauri wa Mheshimiwa Lissu ili Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa wapate ufahamu kuhusu yanayoendelewa kwa Mheshimiwa Lissu, aliyekuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tunatoa wito kwa wote walio nyuma ya mpango wa kutishia usalama wa maisha ya Mheshimiwa Lissu kwa kuelekeza, kufadhili, kutuma au kutekeleza mpango huo kuacha mara moja kwa kuwa mkono wa Mungu na ulinzi wake upo pamoja na watu wasiokuwa na hatia (Zaburi 35 na Zaburi 121). Tunasisitiza kuwa mpango wa kutaka kumdhuru Lissu ni uovu hivyo waache mara moja (Ezekieli 33:1-20).
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani.
Kuna tofauti kati ya demokrasia ya nchi ya Tanzania kwa ustawi wa Tanzania; na demokrasia ya Tanzania kwa ajili ya ustawi ulaya, amerika na asia
Ndio maana siku zote vibaraka na mabwana zao wakishindwa kutimiza mipango yao ya kuipata hiyo demokrasia kwa maslahi yao wanajificha nyuma ya wanachotuaminisha kuwa demokrasia kufanikisha uwepo wa vurugu au vita ili wapate wanachokitaka.
Jiulize ile demokrasia waliyoipigania watu wa ghaddaf wameipata?
Jiulize hao wadai demokrasia wameshindwaje kumaliza vita ya drc? Au wanasubiri mission ikamilike, nchi ibaki tupu ndio watulize ghasia.
Hakuna atakayemgusa. Yeye anajua kuna kesi. Akaamini akigombea mtaingia mitaani kuadamana na kesi zitafia hapo. Sasa mmemtelekeza kama mtoto Yatima. Lazima arudi kwa waliompa project. Issues ni anarudije?Lissu akiguswa hata na unyoya safari hii! , tusije kulaumiana huko mbele ya Safari maana maandiko ya Mungu yanasema Kisasi ni haki, Kisasi kitalipwa tu!
Wala siko huko unako waza. Na nimeelewa kuwa umetanguliza utu kuliko mapenzi ya chama au watu fulani. Nilichovutiwa kwa ulichoandika utu kuliko watu wengine wanaotanguliza hisia kuliko utu.Kama na mimi nimeliona?
Unataka kusemaje kwani?
Mimi ni mtu katili sana ninayefurahia madhila ya watu au?
Nipo miaka mingi humu. Nawe upo kwa muda wa kutosha!
Yaani kabisa hujawahi kuona sehemu yoyote ile nilipokemea maovu ya watu walio madarakani?
Mbona ni mara nyingi tu nimeshakemea waliotenda uovu dhidi ya Lissu.
Huwa mnanishangaza sana mnaposhangaa ninayoyaandika, kana kwamba huwa niko nje sana na common decency.
Au labda huwa huelewi ninayoyaandikaga humu?
Au una kumbukumbu fupi, labda?
Mtu kama JokaKuu au Missile of the Nation, hawezi kushangaa nilichokiandika hapo.
Natumai hata hiki nilichokiandika hapa, utakielewa.
Ukishindwa kukielewa, itakuwa ni majanga!!!!