Askofu Mwamakula: Tundu Lissu aomba hifadhi Ubalozi wa Ujerumani baada ya vitisho vya uhai wake

Askofu Mwamakula: Tundu Lissu aomba hifadhi Ubalozi wa Ujerumani baada ya vitisho vya uhai wake

Kwenye ile press conference alisema atakuwa mstari wa mbele kuongoza maandamano.

Kuna vitu haviingii akilini. Polisi wamemlinda miezi mitatu asubuhi na mchana, halafu sasa hivi anawatuhumu kutaka kumuua!

Kama Tundu Lissu anaamini kuna mtu ana kisasi naye cha kumuua kiasi cha kuhitaji hifadhi ya Ubalozi wa kigeni, hakuwa na sababu ya kurudi nchini. Angebaki hukohuko.
 
Kwenye ile press conference alisema atakuwa mstari wa mbele kuongoza maandamano.

Kuna vitu haviingii akilini. Polisi wamemlinda miezi mitatu asubuhi na mchana, halafu sasa hivi anawatuhumu kutaka kumuua! Kama Tundu Lissu anaamini kuna mtu ana kisasi naye cha kumuua kiasi cha kuhitaji hifadhi ya Ubalozi wa kigeni, hakuwa na sababu ya kurudi nchini. Angebaki hukohuko.
Inafikirisha sanaaa
 
Kwenye ile press conference alisema atakuwa mstari wa mbele kuongoza maandamano.

Kuna vitu haviingii akilini. Polisi wamemlinda miezi mitatu asubuhi na mchana, halafu sasa hivi anawatuhumu kutaka kumuua! Kama Tundu Lissu anaamini kuna mtu ana kisasi naye cha kumuua kiasi cha kuhitaji hifadhi ya Ubalozi wa kigeni, hakuwa na sababu ya kurudi nchini. Angebaki hukohuko.
Mataga jinga kabisa weyeee
 
AMEANDIKA:

BABA ASKOFU EMMAUS BANDEKILE MWAMAKULA.

USALAMA WA MAISHA YA LISSU UKO HATARINI, AKIMBILIA KUPATA HIFADHI KATIKA UBALOZI WA UJERUMANI JIJINI DAR ES SALAAM!

Jana tarehe 5 Novemba 2020 nilizungumza na aliyekuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mheshimiwa Tundu Lissu ambaye anaishi Uhamishoni katika Ubalozi wa Ujerumani jijini Dar es Salaam. Tulikubaliana kuwa mimi kama Askofu na Mshauri wake katika Masuala ya Kiroho, niwajulishe Umma wa Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa kwa ujumla kuhusu hali ya Usalama ya Mheshimiwa Lissu.

Kupitia mazungumzo yale, Mheshimiwa Lissu alieleza kuwa mara baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, alianza kutishiwa maisha yake. Baada ya vitisho kuzidi kuongezeka, Mheshimiwa Lissu alipokea pia taarifa kutoka kwa 'wasamalia wema' waliomtahadharisha kuwa kulikuwa na 'maelekezo maalum' ya kutaka 'vijana wamalizane kabisa na Lissu' safari hii!

Baada ya kutafakari kwa kina taarifa za vitisho hivyo pamoja na taarifa kutoka kwa 'wasamalia wema', Mheshimiwa Lissu aliamua kwenda kutafuta hifadhi ya muda sehemu nyingine tofauti na nyumbani kwake jijini Dar es Salaam hatua ambayo ilionekana kama ni kuhatarisha usalama wa maisha ya watu wengine. Ndipo alipoamua kutafuta hifadhi katika Ubalozi wa Ujerumani jijini Dar es Salaam siku chache. Siku alipokwenda Ubalozini, alipowasili na akiwa nje ya Ubalozi akisubiri taratibu za Ubalozi pale Umoja House, Polisi waliokuwa katika magari mawili walifika pale Ubalozini na kumkamata na kwenda naye Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati (Central Police) jijini Dar es Salaam. Ndipo Maafisa wa Ubalozi waliamua kumfuatilia Mheshimiwa Lissu kwa nyuma na kusubiria pale Central, jambo ambalo liliwafanya Polisi waamue kumuachia kwa kuogopa kelele zaidi kutoka Jumuiya ya Kimataifa.

Mheshimiwa Lissu alinieleza kuwa Maafisa wa Ubalozi wameendelea kuwasiliana na Serikali ya Tanzania kupitia Mheshimiwa Palamagamba Kabudi kuhusu hifadhi yake, lakini Serikali hadi kufikia jana tarehe 5 Novemba 2020, Serikali ya Tanzania ilikuwa inasita kutoa kibali kwa Ubalozi unaoshughulikia masuala ya Lissu kwa kisingizio kuwa Lissu aombe ruhusa ya Kimahakama kwa kuwa anazo kesi Mahakamani. Hoja ya Serikali ilionekana kutokuzingatia au kutokujali tishio dhidi ya uhai wa Mheshimiwa Lissu.

Katika mazingira yaliyopo, tunaiomba na kuishauri Serikali itoe kauli kuhusu kumhakikishia usalama Mheshimiwa Lissu. Kukaa kimya kwa Serikali pasipo kutoa hakikisho lo lote la usalama kwa Mheshimiwa Lissu kutapelekea watu kufikiri na kuamini kuwa Serikali inahusika au iko nyuma ya vitisho dhidi ya maisha ya Lissu.

Ikumbukwe kuwa miaka mitatu iliyopita, Mheshimiwa Lissu aliwahi kulalamika mara kadhaa kuwa kuna watu walikuwa wakimfuatilia na kuwa maisha yake yalikuwa hatarini na haikupita muda mrefu akashambuliwa na risasi mchana jijini Dodoma na hadi sasa hakuna taarifa za kukamatwa kwa mtu ye yote kutokana na tukio lile.

Baada ya kutafakari kwa kina kuhusu hali halisi ya usalama wa Mheshimiwa Lissu katika mazingira ya sasa na baada ya kushauriana na wadau mbalimbali, imeonekana ni vema na ni hekima na usalama kwa Mheshimiwa Lissu kuendelea kuishi Uhamishoni katika Ubalozi wa Ujerumani jijini Dar es Salaam hadi pale itakapoamriwa tena hapo baadaye. Kwa sasa Mheshimiwa Lissu pamoja na baadhi ya Wasaidizi wake wapo katika Ubalozi wa Ujerumani ambapo wanaendelea kupata hifadhi.

Ninaandika haya kama Askofu Mshauri wa Mheshimiwa Lissu ili Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa wapate ufahamu kuhusu yanayoendelewa kwa Mheshimiwa Lissu, aliyekuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tunatoa wito kwa wote walio nyuma ya mpango wa kutishia usalama wa maisha ya Mheshimiwa Lissu kwa kuelekeza, kufadhili, kutuma au kutekeleza mpango huo kuacha mara moja kwa kuwa mkono wa Mungu na ulinzi wake upo pamoja na watu wasiokuwa na hatia (Zaburi 35 na Zaburi 121). Tunasisitiza kuwa mpango wa kutaka kumdhuru Lissu ni uovu hivyo waache mara moja (Ezekieli 33:1-20).

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani.
Hiki ni kichekesho cha mwaka! Hili nalo litapita! Commedian kutoka kusema kuwa akishindwa atawaingiza watz barabarani mpaka ujisalimisha ubalozi wa Ujerumani!!!
 
Tundu anatafuta kusikika tu wala hana la maana lolote, kama ni adui labda jamii yake inayo mzunguka yeye mwenyewe kwenye chama chake au amewahi kupindisha sheria kwa mtu kwenye makesi yao huko..nje na hivyo siamini serikali kuhangaika na mtu mdogo huyo,pia hua anapenda sifa tu kwenye mazungumzo yake mengi ambayo mala nyingi hayana lolote la maana
Jinga kabsa ww
 
Wapi nilipokulazimisha[emoji16][emoji16][emoji16]
Siwezi kukulazimisha unielewe mimi nimeandika ninachokijua ni uamuzi wako kuelewa au kuacha kama ambavyo sikukulazimisha usimpigie kura Tundu
Unaposema "najua umenielewa" una lazimisha coz sijakuelewa, hoja zako zinaelea sana.
 
Mkuu umebebwa na huli igizo la Lissu?

Si ni huyuhuyu wakati wa kampeni alidiriki hata kusema atarusha chopa yake bila kibali maana haogopi chochote?
Mzee kampeni zimeisha .. Saivi hawezi jaribu kusema ivo.. Litapita panga mzee bora aombe hifadhi tu..
 
NI KUKOSA BUSARA sana kusema Serikali inantafuta kumuua. MAMBO KAMA YAKO DIRECT HIVI SI ANGEMALIZWA UBELGIJI HIVI UFIKIRI WETU TUMEUPOZEA WAPI.
 
Kwenye ile press conference alisema atakuwa mstari wa mbele kuongoza maandamano.

Kuna vitu haviingii akilini. Polisi wamemlinda miezi mitatu asubuhi na mchana, halafu sasa hivi anawatuhumu kutaka kumuua! Kama Tundu Lissu anaamini kuna mtu ana kisasi naye cha kumuua kiasi cha kuhitaji hifadhi ya Ubalozi wa kigeni, hakuwa na sababu ya kurudi nchini. Angebaki hukohuko.

Amekula hela za kina Amsterdam na George Sorros. Anatafuta sababu.
Kama watu wangeandamana, jamaa angetisha. Ila watu wamegoma kuandamana. Anaanza kuleta hadithi za alinacha. Anyway, muache awajazie vyoo. Ndio maisha aliyoamua
One thing for sure, anajua sasa Tanzania ni habari nyingine. Asituchukulie poa kama alivyokuwa wanafikiria
 
Kumbe Tanzania inaweza kabisa kuzalisha viongozi wanaofanana Na Hitler.
 
Aibu gani Mr....?!!!

Aibu hii inamfaa Mr Lissu na si Serikali

Aseme tu amenogewa na maisha ya Ulaya anahitaji kuwa Mkimbizi

Ushauri wangu
Bora aende huko German au Belgium, akatafune maisha vzr na si kulichafua Taifa kwa maslahi yake binafsi
We inafaa ukalie cha kati
 
This is very sad!

Yaani mtu yupo uhamishoni ndani ya nchi yake?

Hapana kwa kweli. Hii haikubaliki hata kidogo.

Hivi kosa lake ni nini hasa mpaka watake kumfanyia unyama namna hiyo?

Hapana. Uovu huu lazima ukemewe na watu wote wenye mapenzi mema na Tanzania.

Totally unacceptable.

So mkuu. Unaamini kuwa Serikali ya TZ. Inawaza na kuweza kumuua Lissu kutoka amri ya juu. Tuwe serious for once katika maisha yetu. Hii Ni mbinu Lakini sio ya Serikali. Mana it is tooooooooooo open. No Government can be that stupid
Kwamba Kuna kikundi kinataka kuanzisha fujo kwa kupitia Lissu na hata kuweza kumwuua wala Sina ushahidi na ubishi nalo. Lakini to what END. Tuwape heshima viongozi wetu wa Serikali. Sio wapuuzi kihivvo. Gia za 2025 za bwana Amsterdam. Bila hata Lissu kujua. Naona Hasira za wengi za kushindwa uchaguzi na maandamano zinakuja kivingine. Please this is our country. Let us keep it safe.
 
Back
Top Bottom