Hii ilivyo kaa yenyewe, bila ya ufafanuzi juu yake yanaonekana kuwa kama ni maoni yako.Wenje si amesema atagombea u Makamu Mwenyekiti? Na inaelekea kuwa msimamo wake ni kuwa uchaguzi wa haki maana yake ni Lissu ashinde. Hii ni hatari sana maana anaweka mbegu za kukataa matokeo hapo baadae. Kwa kweli sio vizuri.
Amandla...
Sikuwa na nia ya "kuto kutendea haki" nilipo eleza hapo kwa sababu ya mkanganyiko unao jidhihirisha hapa.
Kwa ufafanuzi ulio toa, sasa unaeleweka vyema kabisa
Uchawa wa aina ya anao uonyesha huyo mchungaji, hauna tofauti yoyote na huu ulio enea kwa mama. Hawa ni watu wanao jitoa akili kichwani hata wasiwe na fikra za kuchambua chochote.
Haijalishi hawa wana tetea upande gani, wote ni wabovu vilevile.
Nakushukuru kwa ufafanuzi.Haujanitendea haki.
Hapa nilikuwa namzungumzia Askofu ambae alikuwa anahojiwa, sio Lissu. Sijui kwa nini umekimbilia kwa Lissu ambae hata sikumtaja. Ni askofu ndie aliyemuita Wenje muoga kwa kukimbia nchi, pamoja na mambo mengine. Nilichotaka kuonyesha ni jinsi ilivyokuwa rahisi kumpakazia mtu. Huyu anaongea kama mfuasi wa Lissu ambae ni Makamu Mwenyekiti. Wenje alitangaza nia ya kutaka kugombea umakamu Mwenyekiti. Hapo unaweza kujumlisha 2 na 2 ukapata 22. Huyu Askofu ametamka wazi kuwa katika uchaguzi wa haki, hamna anaeweza kumshinda Lissu. Hapo si kaunganisha uchaguzi wa haki na ushindi wa Lissu? Hajaweka nafasi ya Lissu kushindwa. Lissu amesema tofauti na huyu askofu. Lissu amesema kuwa hajawahi kuwa Mwenyekiti, na kama atashindwa katika uchaguzi wa haki, atabakia kuwa mwanachama wa CDM ambae hajawahi kuwa Mwenyekiti wa CDM. Haya ni maneno ya kujenga tofauti na ya hao wanaosema kuwa ni wafuasi wake.
Mimi sitashangaa kama akitokeza mwingine atakaesema kuwa haoni sababu ya Lissu kubaki CDM kama atashindwa kwenye uchaguzi. Najua ni hype ya uchaguzi lakini ni hatari. Hasa yanapoonekana dhahiri kumlenga mtu kama Mbowe ambae hajasema kuwa atagombea. Lissu anatakiwa awakemee watu kama hawa.
Amandla...