Askofu Mwingira kauliza swali. Karibuni kwa majibu

Askofu Mwingira kauliza swali. Karibuni kwa majibu

Kwani mashindano yalikuwa ya wizi wa kura au kufa na kupona? Maana alimpiga risasi kampiga risasi na Lissu hakujibu mashambulizi, alipoibiwa kura akataka kujibu mashambulizi(maandamano) ila majeshi yake yakamfelisha hayakutokea uwanja wa vita, basi Lissu akakimbia uwanja wa mapambano.
Ndiyo uwezo wako kiakili ulipoishia au umeamua kujitoa ufahamu?
Kama haukuelewa swali ni busara kuomba ufafanuzi.
Nje ya mada: Wewe ni Sukuma gang?
 
Kwani aliyepo awamu ya sita katokea kwenye wizi huo huo tunasema wa kura, ni mshindi au mshindwa?

Au ule msemo nyama ya nguruwe haram ila mchuzi halal?!
Hebu rudia kusoma swali halafu ulinganishe na utopolo uliouandika.
 
..kwanini mnahusisha kauli hiyo na mambo ya Ccm vs Cdm?

..Askofu hajataja mtu wala chama cha siasa.
Kila mtu atajibu hili swali kulingana na alivyolielewa.Mbona huwaulizi hao Pro CDM kwanini wamehusisha hilo swali na kifo cha JPM moja kwa moja au hujapitia comments zote?
 
View attachment 2496495

N.B. Naomba wote mnaotaka kutoa comment kwenye uzi huu mjibu swali la askofu na si vinginevyo
Hapa naona mtumishi 'ameteleza' kidogo.
Kufariki ni kushindwa?
Kama ni hivyo, hakuna binadamu ambae ni mshindi in the long run, wote tutakufa tu. Nadhani angesema tu kuwa binadamu wote mwisho wetu ni mmoja (kufa), hivyo tupendane na hakuna haja ya kuwekeana uadui katika hiki kipindi chetu kifupi hapa duniani.
 
Tafsri ya kufa sidhani kama askofu anaifahamu vizuri mimi naamini wote tutakufa ila kuna wataoshi baada ya kufa na kuna wataokufa milele. Sasa kwa kiongozi wa dini kusema kuwa kuna mtu amekufa na kuna mwengine yupo hai hiyo hakika kaitolea wap?
 
Wote wapo hai

Maana hata Kikwete alisingiziwa na chadema aliiba kura. Anyway kwa akili za wafuasi wa upinzani,Ccm itapeta miaka mingi sana

Maana saiv upinzani unapigana na hayati badala ya chama tawala. Dhambi zote tunadondoahea kwa hayati na sukuma gang,wengine wote waliobaki ni wasafi sana
 
Ooh,kumbe thamani ya uhai wa mtu inaendana na hadhi yake? Kwamba hao wanachama wa CDM waliokufa Arusha kwenye mkutano huna haja ya kuhoji kwa kuwa hawana hadhi kama ya Kiongozi wao?
Ndio ni hivyo mkuu, we huoni Lissu alikuwa anataka Rais wa nchi ndio amuhakikishie usalama wake alirudi Tanzania? Hivyo ni wazi usalama na uhai wa Lissu una thamani kuliko hao wengine. Watu hatuna hadhi sawa hapa duniani.

Huwezi kufanani uhai wa Lissu na sijui Akwilina au sijui Ulimboka sijui na watu gani huko.
 
Back
Top Bottom