Askofu Mwingira: Nimenusurika kuuawa mara tatu na watu wa Serikali

Askofu Mwingira: Nimenusurika kuuawa mara tatu na watu wa Serikali

Kuna vijana wanashangaa Mwingira kuwa na mali za bilioni 10.
Yaani mtu amehangaika ujana wake wote hadi uzee ule akose mali za 10B?
Kama wazazi na ndugu zenu hawana basi nyamazeni wengine wanazo,tulizeni matyakkoo.
 
NUKUU ZA ASKOFU MWINGIRA:

1. "Nimenusurika kuuawa mara tatu na watu wa Serikali."

2. "Mali zangu zenye thamani ya 10 bilioni yakiwemo Matrekta yaliteketzwa Shambani kwangu."

3. "Dereva wangu alihusishwa katika mauaji na nilipogundua nilimnyang'anya simu."

4. "Dada aliyetoa taarifa za mipango ya kuuawa kwangu aliuawa Rombo Hotel Shekilango Dar es Salaaam."

5. "Mwaka unaokuja Watanzania watakuwa Salama."


26/12/2021.

Stay tuned..
View attachment 2058518
Mtume na Nabii Josephat Mwingira ni Mtumishi wa Mungu na kiongozi wa huduma ya Efatha Ministries nchini Tanzania.

Pia, soma:

Uchaguzi 2020 - Askofu Mwingira: Lissu ni mshindi, hajajenga flyover wala reli. Watu wanamfuata

Anataka tu umaarufu, kwa lipi auawe na serikali, arudisha pesa alizoiba kupitia benki yake pale Mwenge, aache kuwatoza waumini wake anapowalazimisha walale kule Visiga na arudishea mashamba aliyopora kule Sumbawanga, huyu ni tapeli wa kidini sawa tu na akina Bushiri wa Malawi na wengineo wengi
 
Mimi siyo Mungu na siyajui ya sirini lakini Mwingira ni muongo na mtafuta huruma.
Unatambua dhuluma ya mashamba ya watu aliyopata kufanya?!
Nchi hii mwenye nguvu ndiye anafanya analoweza so issue za dhuluma huyo jamaa siyo wa kwanza labda kama una kisasi naye.
 
Kukemea nini dhuluma huku yeye mhuni mkuu, Mimi sio kahaba useme anaweza ni fata, tumieni akili nyie sio mihemko kuwa mtumishi hakukupi utakatifu, nasema hao wangemtaka akiisha asubuhi tu kwani gwajiboy na yule mdada si alitumiwa akamu record hukuona gwajiboy akihamia ccm.
Kwani muhuni haruhusiwi kulalamika?if you are neutral in situations of injustice,you have chosen the side of the oppressor.
 
Je unakubali kuwa tz ilikuwa na changamoto ya ufisadi,vyeti feki ,wauza madawa ya kulevya wizi wa mali za umma nk?
Kwa hiyo , kuwepo hayo ndio rais aamue kutumia sheria anazoziona yeye na sio sheria zinazomuongoza?hizo ni siasa za miaka ya 40, huko, na sio dunia hii, haya ufisadi aliumaliza?hao wa vyeti fake wote walifukuzwa?kiongozi unakuwa na double standard!!lile lilikuwa genge la wadhurumaji tu, na ndio sasa wana haha, na hii nchi isingekuwa na kutanguliza chama mbele, sasa hivi genge kubwa sana la wahuni lingekuwa segerea, kuungana na sabaya!!ila MUNGU FUNDI
 
Anataka tu umaarufu, kwa lipi auawe na serikali, arudisha pesa alizoiba kupitia benki yake pale Mwenge, aache kuwatoza waumini wake anapowalazimisha walale kule Visiga na arudishea mashamba aliyopora kule Sumbawanga, huyu ni tapeli wa kidini sawa tu na akina Bushiri wa Malawi na wengineo wengi
Bahati nzuri huyu alikuwa muwazi toka enzi za jiwe na hakumuogopa na ndio malipo yake hayo!!sio kakobe na gwajima, jibu hoja zake!!kubalini tu shetani lile limeshaondoka sasa na nyie mteseke kwani mlijua kabisa jamaa ndio kafika, na nyie ni kuimba mapambio tu kuwa atake asitake"sasa MUNGU KACHOMOA FUSE, MNASEMAJE?
ILA MUNGU NI FUNDI SANA!!!
 
Huyo Nabii wa kujiita ifikie hatua ajiheshimu.

Hivi unaanzaje kumkashfu Rais kwa tuhuma za kijinga namna ile?! Unamuita Rais shetani kweli?

Niseme wazi mm Rais Samia sifurahishwi na baadhi ya matendo yake lakini siwezi kamwe kumvunjia heshima kwa kiwango kile.

Hali kadhalika hugo nabii wa kujiita alivyo mjinga anataja hotel ya watu kwa kuituhumu kwa kashfa kubwa ya mauaji ilhali hana hata ushahidi!

Rombo hotel mshtakini mahakamani huyo mpuuzi.
Tuliza akili na viungo vyako vya mwiili na punguza mizuka unapoandika hapa JF.
Kesho ni siku ya kazi nenda kamfungulie kesi ili akupe ushahidi wake.
Tuliza matyaakko kama kutuliza akili umeshindwa!!!!!
 
Alipiga sana kelele, na ndio maana hata mashamba yake kule Rukwa, alifanyiwa sana figisufigisu, na awamu ya tano!!ki ukweli ile haikuwa serikali kabisa, na ndio ndio maana watesi hao sasa wanapata shida sana kwani hawakuamini kama ingeweza kumalizika kirahisi hivyo.
Hivi unajua hata sababu ya mashamba yale kuchomwa na wananchi? Au hata hujui nini kilimsibu kwenye yale mashamba unakurupuka tu
 
Kwani muhuni haruhusiwi kulalamika?if you are neutral in situations of injustice,you have chosen the side of the oppressor.
Na yeye aache uhuni mkuu maana sio msafi kunyooshea wengine vidole, pia Kuna maelfu ya mashamba alizulumu Raia huko Sumbawanga, asijifiche kwenye kichaka Cha dini kutafta huruma aisee.
 
Back
Top Bottom