Askofu Niwemugizi amuomba Rais Samia asikubali kufananishwa na Mungu

“Nikikuombea uwe na afya njema na uwe mnyenyekevu lakini pamoja na madaraka hayo makubwa uliyonayo usikubali kamwe kulinganishwa na Mungu kwa namna yoyote ile usikubali."
Askofu ungemwambia tu bila kumficha, kuna watu wengi mno wamefungwa hadi maisha, wengive vifungo virefu na wengine wanasota magelezani - mambo ya UCHAGUZI Mkuu uliopita- ameshaombwa haya mambo kwa muda mrefu sana ila sijui nini kinamkwambisha.

Kuachilia ni sehemu ya ibada kwa mwanadamu, sijajua ugumu anaupata wapi, kama kuwaibia kura mmeiba, kama madaraka mnayo sasa jamani ndiyo muwatese hivi ?
 
hapa Tanzania ni vigumu ukiwa kiongozi ukatae misifa kwa sababu watu wengi wanafiki sana
hata Nyerere alisema kuna kipindi walimuingiza kingi, "Mwalimu ukistaafu nchi itabaki na nani ?"mwisho wa siku anasema aligundua walikuwa ni wachumia tumbo
Brother una akili sana hongera, Nyerere aliwahi kusema kabisa kwamba aliingizwa Chaka na wasaka fursa na hili lilimpata Magu alikuwa akizungukwa na machawa hadi kero
 
Nyerere hakuitwa mtukufu.
Enzi za Nyerere viongozi na watu wote walikuwa wanaitwa Ndugu.
Mtukufu na waheshimiwa mlianza kipindi cha Mkapa.
Hapana. Neno Mtukufu lilitumika sana kipindi cha awamu ya pili. Nakumbuka mwaka 1995 tena ilikuwa mwezi November kama sikosei siku Rais Mkapa (RIP) anataka kutangaza Baraza lake la Mawaziri la kwanza ndiyo ametoka tu kuchaguliwa October 1995 ndipo ALIPOLIPIGA MARUFUKU neno MTUKUFU baada ya MC (yule aliyekuwa anaendesha hiyo event sijui hata anatakiwa kuitwaje) alivyomuaddress kama Mtukufu Rais. MC alikuwa anamkaribisha ili ahutubie na kutangaza Baraza la Mawaziri.

Ndipo Mkapa aliposimama akasema kuanzia siku hiyo hataki kuitwa Mtukufu kwa sababu Mtukufu ni Mungu peke yake!!!. Since then hakuna Rais aliyetumia neno hilo ndipo tulipoanza kutumia MHESHIMIWA
 
Nani aliwahi kujifananisha na Mungu Tz?

Magufuri. Aliwahi kuitwa Mungu na Waziri Fulani na Wala hakukanusha. Pia amewahi kuitwa Yesu na mbunge mmoja wa CCM , tena kwa kusema jina la Magufuri libarikiwe.
 
Niwemugizi ni Desmond Tutu mwingine - ni mnyoofu kama rula. SSH hebu plz fanyia kazi ushauri wake upate thawabu
 
... kizazi cha lini wewe? Official salutation ya Nyerere ilikuwa Mwalimu or Ndugu or (rarely) Mheshimiwa na sio vingenevyo!
Mheshimiwa Nyerere alikataa, ilirudi wakati wa mkapa.
Ila Kuna hii wakati wa mawaidha... "Watukufu waislam"! Hii ni sawa?
 

Doctrine ya ukristo Ni utatu Mtakatifu. Mungu Baba, Mungu Mwana na Roho Mtakatifu.
 
Magufuri. Aliwahi kuitwa Mungu na Waziri Fulani na Wala hakukanusha. Pia amewahi kuitwa Yesu na mbunge mmoja wa CCM , tena kwa kusema jina la Magufuri libarikiwe.
No hiyo sidhani kama yeye alipenda. Ni kama Mama alivyokaa kimya kuacha Dkt Magufuli adhalilishwe sidhani kama anamaanisha hakumpenda
 
Haya yangefaa yasikiwe na wanaomtukuza
 
Baada ya jubilee Rais ataenda chato, mwenye akili na atambue
 
Mheshimiwa Nyerere alikataa, ilirudi wakati wa mkapa.
Ila Kuna hii wakati wa mawaidha... "Watukufu waislam"! Hii ni sawa?
Nadhani kwa mazingira ya ibada haina tatizo kuwa-address hivyo kwa ujumla wao (the people) ila sio mmoja mmoja.
 
Nyerere alitwa mtukufu rais mpk anang'atuka na hakuna lolote lililompata.

Ni unafiki wetu tu wanadamu tunaweza kutukuza kitu kwa mdomo lakini moyoni hakuna kitu.

Uzuri hilo neno liliisha ondolewa tangu awamu ya tatu.
Wakati wa Nyerere ilikuwa ni NDUGU
 
Hakuna binadamu asiyependa kutukuzwa awe mbunge au mchungaji,padre ,askofu ,shehe nk au mtu wa kawaida ndio maana hata maaskofu husujudiwa watu wanapobusu Pete yake hupiga magoti kuibusu Pete

Hivi sahihi mwanadamu kumpigia magoti mwanadamu mwenzie ville?

Na hupenda kuitwa Baba Askofu,baba padre au Baba mchungaji wakati hawakuwazaa
 
[emoji38][emoji38][emoji38] we jamaa kichwani mwako hamna kitu
 
Mkuu Achana naye huyo, ukute Anataka kupima watu watasemaje.
 
Huyu ni baadhi ya Maaskofu wachache sana Wakatoliki ninao wakubali wanajitambua.
 
Nyerere alitwa mtukufu rais mpk anang'atuka na hakuna lolote lililompata.

Ni unafiki wetu tu wanadamu tunaweza kutukuza kitu kwa mdomo lakini moyoni hakuna kitu.

Uzuri hilo neno liliisha ondolewa tangu awamu ya tatu.
Lakini mkuu, Nyerere aliikataa ile kauli mbiu ya 'Zidumu fikra za mwenyekiti'.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…